POLE SANA!Mungu awasaidie. Jipe moyo, mkumbuke Mungu aliyemuumba uyo nduguyo kuwa anao uwezo wa kukumponya kabisa...kama aliweza kuumba mwili mzima, hawezi kushindwa visehemu vichache tu vya mwili wake. sitaongea mengi kwasababu inaniuma kusikia hivyo, ushauri wangu, fanyia kazi ushauri wa madaktari, na pia uwe unatembea kwenye maombi makanisani. doesnt matter unasali hapo au vipi, uko kwenye tatizo hivyo tafuta makanisani kama vile mtu anavyotafuta dhahabu machimboni bila kujali kama amezaliwa machimboni.
Neno la Mungu lina sema, mwenyewe aliyachukua magonjwa yetu yote na madhaifu yetu yote, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. kilichomshinda mwanadamu Mungu hawezi kushindwa.
ukiwa unatumia dawa, usiweke imani kuwa hizo dawa ndo zinakuponya, weka imani kuwa Mungu ndo anakuponya kwasababu Mungu ndiye anayewapa wanadamu maarifa hata ya kuwa madaktari kutumika mahospitalini kwaajili yetu, na anaweza kuponya kwa namna zote, kwa njia ya dawa na pengine bila hata dawa kama akiamua..ndo maana nasema JARIBU KILA SEHEMU hadi upate pale Mungu alipopanga kukutana na wewe atue mizigo yako, pengine amepanga kumponya pasipo dawa akawa anasubiri ufike kwa watumishi wa Mungu ili Mungu ATUKUZWE KUPITIA HAPO, huwezi jua..so nenda makanisani kila mahali, omba wachungaji wawaombee mpone na ilo pepo liondoke kabisa kwenye ukoo wenu na kizazi chote...
Neno la Mungu linasema "nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona", hivyo ukimtafuta Mungu kwa bidii zako zote, nakuhakikishia utamwona Mungu na nduguyo atapona kabisa kabisa, Mungu anaweza kufanya jambo lolote na makusudi yake hayawezi kuzuiliwa na ugonjwa tu... ukimwamini na kumtafuta kwa moyo wako wote...
shetani anao uwezo wa kuweka kansa kwenye mwili wa mtu, na chochote kile vilevile, na Yesu amemshinda shetani na Yesu anao uwezo wa kuondoa ugonjwa wowote aliouweka shetani..kumbuka magonjwa yote hutoka kwa shetani si kwa Mungu..mwovu haji ila kuua kuchinja na kuharibu.... cha maana, Mwamini Bwana Yesu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako wewe na huyu mgojwa, kateni shauri la kuokoka leo,..Yesu hawezi kuja bila kumwalika..ufunuo 3;20 anasema Tazama nasimama mlangoni nabisha hodi, mtu akifungua mlango nitaingia kwake nitakula pamoja naye naye pamoja name..mwambie Yesu umefungua mlango aingie...Yesu akiingia, atakusamehe dhambi zako zote na atakuponya magonjwa yako yote..zaburi 103 inasema, Bless the Lord Oh my soul, and all that is whithin me praise his Holy Name, don't forget his rightiousness, he forgives all your iniquities and heals all your diseases...(nimetoa kichwani kama nitakosea quotation)...akikusamehe dhambi ndo huwa anakuponya magonjwa yako yote, ndo maana alipowaponya watu wengine kipindi kile aliwaambia tu "jitwike godoro lako dhambi zako zimesamehewa" na watu hao hata kabla hajataja kwamba wamepona, walisimama na kuwa wazima....
Nenda kwenye kanisa la Gwajima kule kawe, nenda kwenye kanisa la mwingira, kakobe, nenda kwenye kanisa la agape, nenda kwenye kanisa la siloam kule mbezi makonde, nenda kila sehemu rafiki yangu ukimtafuta Mungu akuponye.wewe usisikilize watu hapa tupo kutafuta uponyaji, watu wa Mungu siku zote huwa wanatukanwa na kusingiziwa mengi, hata Yesu walisema ni wa belzebub, usisikilize watu wanavyowasema watumishi wa Mungu...mambo mengine hayaponi hadi ukutane na mtu anayetumiwa na Mungu kama ilivyokuwa kwa Eliya na Elisha...Mungu awasaidie..na huu uwe ushauri kwa wengine pia...Mungu na akuponye kwa Jina la Yesu Kristo, sawasawa na imani yako.