Nimsaidieje ndugu yangu na Kansa inayomsumbua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimsaidieje ndugu yangu na Kansa inayomsumbua

Discussion in 'JF Doctor' started by Sir, May 6, 2010.

 1. S

  Sir Member

  #1
  May 6, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba msaada hata wa mawazo niweze kumsaidia ndugu yangu ambaye kansa inamsumbua

  Mwanzo ilikuwa breast cancer, surgery ikafanyika ocean road hospital ikifuatiwa na matibabu mengine kama chemotherapy na mionzi.

  Baadae ikagundulika kuwa sehemu nyingine kama ini vimekuwa affected na akaanza dozi nyingine ambayo inaendelea hivi sasa, therapy for 6 times each month.

  Lakini sasa hali inakuwa si nzuri, baada ya dozi ya pili, mgonjwa anakosa hamu ya kula completely na nguvu zinamuishia kabisa huku tukiambiwa tujitahidi tumpe chakula kusudi apate nguvu ya kuendelea na dozi.

  Nina imani kuna wazoefu wa case kama hizi, naomba ushauri wowote,
   
 2. w

  wasp JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama wewe unamwamini JEHOVA ambaye ni Mungu wa Abraham, Isaka na Yakobo basi muombee huyu ndugu yako kwa Bwana maana yeye anasema "Mimi ndimi BWANA nikuponyaye" (Kut.15:26)
   
 3. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2010
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sir pole!
  Ni jambo la kusikitisha,lakini kwa habari ambazo si rasmi ile kitengo cha mionzi OCRI inasemekana ile machine ya OCRI haiwezi ku focus kwenye sehemu yenye tatizo na matokeo yake ndio kama hayo yaliyompata mgonjwa wako,kwa kutaka kutibu kimoja unakuja kukuta umepata tatizo lingine.
  Ndio maana watu wengi wamekuwa wakiwa na feeling kuwa ukichomwa na mionzi ndio chanzo cha kufa kwa sababu unakwenda una tatizo la titi, angalia kama hivyo unatoka na tatizo la ini.

  Na kwa wataalamu wanasema sehemu pekee yenye machine ambayo iko (precise) iko south africa (ambayo sio latest) lakini latest na affordable machine iko India.
   
 4. T

  Tall JF-Expert Member

  #4
  May 12, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  ni PM kwenye e mail yangu tuongee pia weka na namna yako ya simu.
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  kwa Ushauri wangu hebu jaribu kutumia hii Dawa kuzuia hiyo Kansa isiweze kuenea mwili wote huku Madoctor wakijaribu kupata Uvumbuzi wake Dawa yenywe ni hii hapa Upate Vitunguu Saumu kwa wingi sana Uvisage upate maji yake kwa kipimo cha kijiko kimoja cha kulia wali kila siku awe anakunywa kutwa mara tatu kabla ya kula kitu yaani Asubuhi mchana na usiku kwa muda wa miezi 6 basi kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu atapona na kuondoka kabisa hiyo Kansa Mwilini mwake jaribu kisha utaniambia mimi Matokeo yake.Na pia Mgonjwa awe anakunywa sana Juise ya Karoti kutwa mara tatu yaani Glasi tatu kwa siku Atapona KwaUwezo wake Mwenyeezi mungu asante.
   
 6. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,017
  Trophy Points: 280
  Amen, lililo gumu kwa binadamu kwa Mungu ni jepesi, ombeni kwa imani, hakika atapona ndugu yenu. Mungu awape nguvu
   
 7. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,017
  Trophy Points: 280
  Asante kwa ushauri na maelekezo mazuri Ndg. MM, Mungu akubariki nawe kwa kutumika kama msaada katika maisha ya waja wake
   
 8. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  1.Tiba mbadala itasaidia.Kuna hao NATURAL THERAPY CENTER wana dawa nzuri unaweza kujaribu.
  2.Kufunga na kuomba ni muhimu.
   
 9. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  pole sana maombi pia yatamsaidia, ndio nasikia matatizo ya ORCI mie ndungu yangu aliondoka na moyo umekuw mkubwa pia kinga ilishuka sana ila pamoja na maombi alipopimwa tena wameona hana tatizo (cells za cancer) na anaendelea vizuri tu miaka 6 sasa toka apigwe mionzi.
  Kipindi cha matibabu ya mionzi ni kigumu sana maana wanatapika kila kitu, pia wanashindwa kula kabisa ila mu mtie nguvu na matumaini kwa maombi na akisimama mionzi mbidiishe kula.
  Karoti na vitunguu saumu juice zake zinaleta kinga maana inapungua sana.
   
 10. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,017
  Trophy Points: 280
  Ushuhuda mzuri huu. Asante Mama Joe
   
 11. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Amen asante Mokoyo huu ni ugonjwa unaokatisha tamaa sana bila kumhusisha Mungu wengi wanashindwa, inahuzunisha sana ukitemebelea ORCI, sura zimekata tamaa, laiti wangeamka na kumtafuta Mungu!
   
 12. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #12
  Jun 16, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  POLE SANA!Mungu awasaidie. Jipe moyo, mkumbuke Mungu aliyemuumba uyo nduguyo kuwa anao uwezo wa kukumponya kabisa...kama aliweza kuumba mwili mzima, hawezi kushindwa visehemu vichache tu vya mwili wake. sitaongea mengi kwasababu inaniuma kusikia hivyo, ushauri wangu, fanyia kazi ushauri wa madaktari, na pia uwe unatembea kwenye maombi makanisani. doesnt matter unasali hapo au vipi, uko kwenye tatizo hivyo tafuta makanisani kama vile mtu anavyotafuta dhahabu machimboni bila kujali kama amezaliwa machimboni.

  Neno la Mungu lina sema, mwenyewe aliyachukua magonjwa yetu yote na madhaifu yetu yote, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. kilichomshinda mwanadamu Mungu hawezi kushindwa.

  ukiwa unatumia dawa, usiweke imani kuwa hizo dawa ndo zinakuponya, weka imani kuwa Mungu ndo anakuponya kwasababu Mungu ndiye anayewapa wanadamu maarifa hata ya kuwa madaktari kutumika mahospitalini kwaajili yetu, na anaweza kuponya kwa namna zote, kwa njia ya dawa na pengine bila hata dawa kama akiamua..ndo maana nasema JARIBU KILA SEHEMU hadi upate pale Mungu alipopanga kukutana na wewe atue mizigo yako, pengine amepanga kumponya pasipo dawa akawa anasubiri ufike kwa watumishi wa Mungu ili Mungu ATUKUZWE KUPITIA HAPO, huwezi jua..so nenda makanisani kila mahali, omba wachungaji wawaombee mpone na ilo pepo liondoke kabisa kwenye ukoo wenu na kizazi chote...

  Neno la Mungu linasema "nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona", hivyo ukimtafuta Mungu kwa bidii zako zote, nakuhakikishia utamwona Mungu na nduguyo atapona kabisa kabisa, Mungu anaweza kufanya jambo lolote na makusudi yake hayawezi kuzuiliwa na ugonjwa tu... ukimwamini na kumtafuta kwa moyo wako wote...

  shetani anao uwezo wa kuweka kansa kwenye mwili wa mtu, na chochote kile vilevile, na Yesu amemshinda shetani na Yesu anao uwezo wa kuondoa ugonjwa wowote aliouweka shetani..kumbuka magonjwa yote hutoka kwa shetani si kwa Mungu..mwovu haji ila kuua kuchinja na kuharibu.... cha maana, Mwamini Bwana Yesu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako wewe na huyu mgojwa, kateni shauri la kuokoka leo,..Yesu hawezi kuja bila kumwalika..ufunuo 3;20 anasema Tazama nasimama mlangoni nabisha hodi, mtu akifungua mlango nitaingia kwake nitakula pamoja naye naye pamoja name..mwambie Yesu umefungua mlango aingie...Yesu akiingia, atakusamehe dhambi zako zote na atakuponya magonjwa yako yote..zaburi 103 inasema, Bless the Lord Oh my soul, and all that is whithin me praise his Holy Name, don't forget his rightiousness, he forgives all your iniquities and heals all your diseases...(nimetoa kichwani kama nitakosea quotation)...akikusamehe dhambi ndo huwa anakuponya magonjwa yako yote, ndo maana alipowaponya watu wengine kipindi kile aliwaambia tu "jitwike godoro lako dhambi zako zimesamehewa" na watu hao hata kabla hajataja kwamba wamepona, walisimama na kuwa wazima....

  Nenda kwenye kanisa la Gwajima kule kawe, nenda kwenye kanisa la mwingira, kakobe, nenda kwenye kanisa la agape, nenda kwenye kanisa la siloam kule mbezi makonde, nenda kila sehemu rafiki yangu ukimtafuta Mungu akuponye.wewe usisikilize watu hapa tupo kutafuta uponyaji, watu wa Mungu siku zote huwa wanatukanwa na kusingiziwa mengi, hata Yesu walisema ni wa belzebub, usisikilize watu wanavyowasema watumishi wa Mungu...mambo mengine hayaponi hadi ukutane na mtu anayetumiwa na Mungu kama ilivyokuwa kwa Eliya na Elisha...Mungu awasaidie..na huu uwe ushauri kwa wengine pia...Mungu na akuponye kwa Jina la Yesu Kristo, sawasawa na imani yako.
   
 13. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #13
  Jun 16, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Naamani kamanda wa jeshi la washami ilibidi amfuate elisha mbali kwa safari ndefu ili akapone ukoma, alifunga safari kabisa pamoja na kwamba naamani alikuwa na uwezo wa kubaki kwake home na kumwomba Mungu peke yake(kwasababu Mungu yupo kila sehemu), hadi pale alipomfuata Elisha aliyekuwa mpakwa mafuta wa Bwana ndo alipna, kumbe Mungu ndio alikuwa amemwekea hapo ndo iwe pa uponyaji wake ili hadi leo hii sisi tusome ushuhuda wake na kumtukuza Mungu aliye hai. ndo maana nasema, huwezi jua ni wapi Mungu ameweka uponyaji wako, huwezi jua ni wapi Mungu ametaka wewe utokee/breakthrough, mwombe Mungu akuonyeshe huku ukimtafuta kwa moyo wote na kumwomba aonekane kwako kama alivyoahidi, ataonekana kwako, kwa familia yako, na kizazi chako chote.

  mwenyewe Yesu alipokuwapo hapa duniani, kila alipoenda alitenda mema, aliponya wagonjwa, alifufua wafu, alitenda miujiza mingi,na aliwaachie kazi hiyo ya kufungua watu toka kwenye vifungo vingi, watumiishi wake watakaomwamini leo hii..aliwapa mamlaka ya kuponya magonjwa, kufufua wafu na kutenda miujiza mikubwa kuliko hata ile aliyoitenda yeye...mwaminini Mungu enyi kizazi cha leo, Upendo wake ni wa ajabu mno, anatupenda kila iitwapo leo, hata kama wakati mwingine unahisi kama Mungu hakuoni au yuko mbali nawe, anakwambia kwa sauti ya upole here I am, wakati mwingine tunajichanganya na kufanya maovu, tukifikiri Mungu ametutupa na kututapika kabisa, lakini kwa huruma anasema njoo mwanangu, yasikilize maneno yangu ili upate kula mema ya nchi. Yeye ni Mungu anayetuma malaika kuwalinda wale wote wanaourithi wokovu/wanaookoka, yeye ni Mungu asiyelala wala hasinzii, hata tukipita kwenye bonde la uvuli wa mauti, kifo kikiwa kinanuka, Yeye yupo kutuokoa hukohuko..

  alishinda mauti, mauti imeshindwa kwa Mwokozi wa ulimwengu Yesu Kristo, haina nguvu tena kwao walio ndani ya Kristo Yesu(hata kama tutaonekana tumekufa, tumechukuliwa tu kwenda kupumzika kifuani pa Mungu wetu, tunao uhakika wa uzima wa milele ndani yake), ndio maana hata mtu aliyekufa anaweza kufufuka kwa Jina la Yesu kama Mungu ameamua iwe hivyo. Mkuki wake ubavuni uliotoa maji na Damu isiyo na hatia, ni ishara kuwa aliishinda mauti kwaajili yetu, kwani ilionyesha amekufa, na siku ya tatu akashinda mauti kwa kufufuka kwake. cancer haina uwezo wa kutuua, magonjwa yoyote yale hayana nafasi kwetu kama tukikimbilia kwenye huu mwamba ulio imara....lakini kama tukimwacha na kumkataa Mungu, shetani atarusha magonjwa na madudu yoyote apendavyo...
   
 14. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  uwe unatuambia maendeleo ya mgonjwa, tunakuombea ndugu!
   
Loading...