NIMSAIDIEJE MKE WANGU (msaada tafadhari)

NIMSAIDIEJE MKE WANGU (msaada tafadhari)

Toffee

Member
Joined
Apr 21, 2013
Posts
80
Reaction score
25
"Habari Wakuu"

Tunaishi nyumba ya kupanga, kwa miaka minne tangu tuoane na mke wangu
tumefukuzwa mara mbili, na mpaka sasa bado hali ni tete:

NYUMBA ya1, Ndani ya miezi sita tuliketi zaidi ya mara mbili kuzungumzia tofauti zao
kati ya mke wangu na Ma mwenye nyumba.
Hatimae huyo Mama alisema; Kijana kabla hujaoa tumeishi nawe vizuri ila sasa!
nisionekane kuku vurugia ndoa yako tafuta nyumba uhame. kama tatizo liko kwangu
lita kua limekwisha.
Tuliamua kutafuta nyumba na yeye awe na kazi, tukiamini hata mashoga inaweza
kuchangia migogoro, baada ya kupata nyumba tukahama.

NYUMBA ya2, Tulifungua duka la rejareja, alishindwa si kuuza wala kusimamia maana hata
mdogowake aliingia kuuza na kisha pesa kutia mfukoni mwake.
Niliamua kuacha kazi yangu kwa muda na kukaa mwenyewe. Ndipo nilipo gundua
kumbe hata hapo teari manenomaneno ya shaanza na Ma mwenye nyumba.
Tumeketi zaidi ya mara mbili na hatimae tulifukuzwa.

NYUMBA ya3 Kaanzisha mahusiano na msichana wa kazi wa Ba mwenye nyumba.
Nilimshauri aachane nae hakusikia, baba mwny nyumba nae alituonya kusiana na
ukaribu wao lakini bado unaendelea.
Sasa huyo Binti ni mjamzito na inasemekana kutokana na ukaribu wao, hata mke wangu
amechangia. Mama mwny nyumba kafikia hatua yakumwambia mmewe tuhame.
Tuna mtoto mmoja mwenye miaka mitatu, nakosa amani sababu ya mke tuu.
(Naomba ushauri wenu tafadhari.)
 
Aisee pole sana. Huyo mama/mkeo ni mkorofi wapo watu wa aina hiyo. Sijui hata namna ya kuanza kukushauri ngoja nifikirie
 
kwani umeshajua kwa nini mkorofi, yaani katika maneno yake nini anapenda kusema zaidi? na ulipomkarisha chini nini anakisema? mara nyingi maneno ya mtu ndio njia ya kujua tatizo lipo wapi, na je yeye pia analeta pesa nyumbani au anakusubiri wewe tu?
 
si ujenge mkuu hata room mbili....utaishi maisha ya kipastoralist hadi lini?
na huyo mkeo mrudishe kwao miezi sita akafundwe mweee..
mfupa uliomshinda fisi utauwezea wapi..mwishoni utahamishwa hata nchi kisa mke...na wewe upo tu ....kuwa mume acha uboya..
 
++

Jiwe lisilotulia halifai kwa ujenzi
Mtahama mara ngapi? Jaribu kukaa vizuri na huyo mke,,zungumza nae.Pengine anahitaji msaada wa ushauri tu Hakuna mtu mwenye aleji na kila mtu hata vichaa wana tabasamu zenye kuvutia watu wawatazame.
Nakutakia wakati mgumu lakini wenye mafanikio.

++
 
wanawake kama hao wapo........,
huku kwetu kuna huyo mama kila siku wanafukuzwa kwenye nyumba kisa maneno
mi nimekuja mtaani nikamsikia maneno yake,sa hivi amehamia hapa nnapoishi keshaniongelea wee
mpaka amechoka sema mi sina time tu tungekuwa tushadundana.

kila siku wanakaa vikao harekebishiki,maana anajifanya anajua in and out ya kila mtu.
endelea tu kumvumilia......,ila siku wakija kumsuta na matarumbeta anaweza kupunguza
lakin kuacha hawezi inakua hulka yao.
 
kwani umeshajua kwa nini mkorofi, yaani katika maneno yake nini anapenda kusema zaidi? na ulipomkarisha chini nini anakisema? mara nyingi maneno ya mtu ndio njia ya kujua tatizo lipo wapi, na je yeye pia analeta pesa nyumbani au anakusubiri wewe tu?

alete pesa nyumbani wapi
mara nyingi wanawake kama hao wanakuaga wapo tu nyumbani wanapika
na kupakua.......,ko hata mda wa kupiga majungu anakua nao
 
si ujenge mkuu hata room mbili....utaishi maisha ya kipastoralist hadi lini?
na huyo mkeo mrudishe kwao miezi sita akafundwe mweee..
mfupa uliomshinda fisi utauwezea wapi..mwishoni utahamishwa hata nchi kisa mke...na wewe upo tu ....kuwa mume acha uboya..

Duuuuh_umeanza ushauri vizuri_lakn hapa mwishoni umerusha mawe makubwa.....mzima lakn_smile...?
 
Take it from my Father NEVER EVER REASON WITH A WOMAN!!!!!!!! A battle with a woman is a lost battle before fighting! Ukimshinda unamuonea, akikushinda unamuogopa na hukohoi mbele yake! Either way you are doomed!

Swala ni rahisi tu hilo mbona!

1. Mpe onyo kali tena mbele ya wazazi wake, na useme bayana akirudia hata chembe unamrudisha kwao. (Nuhakika atarudia tu kujifanya mtu mzima hatishiwi nyau!)

2. Mkiambiwa muhame mrudishe kwao ake huko hata miezi 6 ukitanabaisha bayana umechoshwa na ukosefu wa nizamu wa mkeo. Ukimfata waambie wote akirudia tena Talaka! coz ushamuacha miezi 6, akili zitakaa fresh.

3.Sababu anakupima na kukujaribu, kitu unamwambia asifanye anafanya na wewe uwe unarudisha majaribu yake pia maksudi! Kama hivo unamuuliza kistarabu nilikwambiaje kuleta kidomodomo? Akijibu jeuri, humpi pesa ya kujinafasi na sababu unamwambia ana kiburi, Humpi mpka anyooke!

Vinginevo atakukalia mpaka kichwani huyo bidada. Chukua Rula umnyooshe!
 
Duuuuh_umeanza ushauri vizuri_lakn hapa mwishoni umerusha mawe makubwa.....mzima lakn_smile...?
sasa unamshauri nini igwe...mi nachukia mwanaume anaetawaliwa na mwanamke...kama vipi unapiga chini fasta
 
si ujenge mkuu hata room mbili....utaishi maisha ya kipastoralist hadi lini?
na huyo mkeo mrudishe kwao miezi sita akafundwe mweee..
mfupa uliomshinda fisi utauwezea wapi..mwishoni utahamishwa hata nchi kisa mke...na wewe upo tu ....kuwa mume acha uboya..

hapo sasa si hadi awe na hiyo ela ya kujenga room 2.......,
kama hana ....?
 
ndio tatizo la wanawake waliopatikania JF,unaoa mwanamke humjui vizuri,hujakaa nae kumsoma tabia zake.pole sana,cha msingi jitahidi ujenge nyumba yako labda atapunguza ukorofi
 
hapo sasa si hadi awe na hiyo ela ya kujenga room 2.......,
kama hana ....?
na kwa huyu mwanamke hatokaa anunue hata tofali la sample maana akijikusanya kidogo tu hela zote zinaishia kwa madalali si unajua masharti ya upangaji mpya?
 
sasa unamshauri nini igwe...mi nachukia mwanaume anaetawaliwa na mwanamke...kama vipi unapiga chini fasta

Good girl......

Off topic_hebu fanya mpango wa kurudisha kale ka_avatar ka..zamani please...mmmh?
 
ndio tatizo la wanawake waliopatikania JF,unaoa mwanamke humjui vizuri,hujakaa nae kumsoma tabia zake.pole sana,cha msingi jitahidi ujenge nyumba yako labda atapunguza ukorofi
wewe mwanamke wa jf muda wote yupo busy na keyboard muda wa umbea tutoe wapi!
kwanza wanawake wa hapa nadhani ndo tupo hot sokoni uliza..wenye bahati zao ndo wanatupata.kama vipi jaribu kama utapata kitu hapa...
 
Leo naona hautaki utani_ngoja nisubiri kesho labda utakuwa normal.
 
Back
Top Bottom