Nimsaidieje binti huyu?

Nimsaidieje binti huyu?

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,618
Najua wanaMMU mko powa hamjadhulika na NYINYIEM

Ni wiki mbili sasa tangu nimempokea binti nyumbani kwangu ambaye alijieleza kwamba mama aliyekuja naye toka Kigoma kamtelekeza kwenye nyumba ya wageni. Kwa uwa mama watoto anabanwa na kazi nyingi za hapo nyumbani tuliona vyema kumpokea na kuishi naye kama msichana wa kazi.

Nikiwa job nikapigiwa cm na mama watoto eti binti huyo kajifungua salama. Nilipofika nyumbani nikafanya mahojiano na huyo binti anasema nimsaidie aendelee kuishi nyumbani kwangu na akiimrika kiafya ataendelea na kazi kama kawaida; nimemshauri nimpe nauli arudi kwao Kigoma anadai hawezi kurudi, anadai nikimpa nauli anaenda kujiunga na ombaomba mjini, Nimsaidieje huyo binti?
 
Msaada kama huwa hauna ushauri, sasa usipomsaidia wewe amsaidie nani?? weka imani mbele Mungu atakusaidia ila make sure unatoa taarifa serikalini kuhusu kuishi naye!!
 
Ahsante kwa ushauri wako; lakini ni kweli ukimchukua house girl lazima utoe taarifa serikalini?
 
Msaada kama huwa hauna ushauri, sasa usipomsaidia wewe amsaidie nani?? weka imani mbele Mungu atakusaidia ila make sure unatoa taarifa serikalini kuhusu kuishi naye!!

kaa nae kdg mtt akipata nguvu msafirishe kwao akamtafute bb wa mtt alee mwanae.....mimi mahausi gelo washanitenda sana hadi sina hamu nao, hata ukimfanyia ubinaadamu leo kesho anaweza akakuibia na kuondoka huku katekeleza watt wko wadogo nyumbani.....ni wau ambao inabidi uishi nao kwa akili sna
 
Kuwa makini unless utapata tutorial ya kuibiwa
 
kaa nae kdg mtt akipata nguvu msafirishe kwao akamtafute bb wa mtt alee mwanae.....mimi mahausi gelo washanitenda sana hadi sina hamu nao, hata ukimfanyia ubinaadamu leo kesho anaweza akakuibia na kuondoka huku katekeleza watt wko wadogo nyumbani.....ni wau ambao inabidi uishi nao kwa akili sna

Naona ugumu kumtimua, hata wife anakahurumia sana. Lakini najiuliza maswali mengi, hivi hakakujua kuwa mimba ni kubwa ya kujifungua???? Kanadai aloaleta alianza kukatafutia wanaume kakawakataa ndo maana akakatelekeza.
 
alijifungulia nyumbani?
angekufa je ungefanyaje?

wewe ndio kituo cha kuzuia omba omba mjini?

Kaka maswali magumu hayo na majibu yake ni magumu pia,

Alijifungulia kwenye dispensary ya serikali.
Kuhusu mimi kuwa kituo cha ombaomba sio kweli, mi nilimkubalia aishi kwangu kama mfanyakazi wa ndani tu.
 
Najua wanaMMU mko powa hamjadhulika na NYINYIEM

Ni wiki mbili sasa tangu nimempokea binti nyumbani kwangu ambaye alijieleza kwamba mama aliyekuja naye toka Kigoma kamtelekeza kwenye nyumba ya wageni. Kwa uwa mama watoto anabanwa na kazi nyingi za hapo nyumbani tuliona vyema kumpokea na kuishi naye kama msichana wa kazi.

Nikiwa job nikapigiwa cm na mama watoto eti binti huyo kajifungua salama. Nilipofika nyumbani nikafanya mahojiano na huyo binti anasema nimsaidie aendelee kuishi nyumbani kwangu na akiimrika kiafya ataendelea na kazi kama kawaida; nimemshauri nimpe nauli arudi kwao Kigoma anadai hawezi kurudi, anadai nikimpa nauli anaenda kujiunga na ombaomba mjini, Nimsaidieje huyo binti?

Kwanza, hongera kwako na kwa mkeo kwa roho ya huruma na ukarimu!
Hapo nilipobold penye nyeusi pamenichanganya sana, sijui ni uzee wangu au miwani ndo inasababisha nisione vizuri. Kwenye mstari wa kwanza niliobold ulisema umlimchukua ili kumsaidia na kumfanya awe msaidizi wa kazi za ndani. Sasa hapo nilipobold mara ya pili, ukaandika kuwa binti anaomba kuendelea kukaa kwako. Hapo penye nyekundu unafikiria kumpa nauli arudi kwao baada ya kujifungua.

Nimejiuliza kipuuzi maswali yafuatayo:
  • Wakati unamsaidia hukujua kuwa ana mimba na yuko karibu kujifungua?
  • Wakati unafikiria awe msichana wa kazi ulisahau kuwa ana mimba na atajifungua?
  • Kwa nini reaction ya kumrudisha imekuja baada ya yeye kujifungua, umekerwa na nini?

Anyway, nakushauri kaa na mkeo na kufanya maamuzi ambayo mnayaona hayatayumbisha nyumba au uhusiano wenu. Ni vzr kumsaidia kama uwezo huo mnao maana ni mwanadamu anayehitaji msaada, lakini msaada wenu usije kugeuka kuwa ni chanzo cha matatizo. Vitisho vyake visiwaharibie mipango yenu ndani ya nyumba, na huruma zenu pia zisizidi uwezo wenu.
 
Be very careful Mkuu, Sheria inamaana yeke. Tafadhali sana waone Ustawi wa jamii watakupa ushauri mzuri na kuweka rekodi ya kiserekali kuwa huyo binti na Kachanga chake wanaishi na wewe. Siombi mabaya lakini Kuna (1) Vifo (2) Migogoro na baba mtoto na familia ya huyo binti --Ukidharau hili siku moja itakula kwako mkuu.

Ni vizuri sana kumsaidi binadamu mwenzako. Likini fuata sheria husika ili uwe na amani na kulinda familia yako.
 
Story yako inakuwa kama vile imerukaruka matukio na imenipa maswali.

Kama ni kweli huyo msichana ulimpokea wiki 2 zilizopita kama ulivyojieleza ni dhahiri kwamba alikua na tumbo kubwa hivyo ilikua ni rahisi kumtambua kwamba huyo msichana ana mimba.

Je wewe au mkeo hamkumuona huyo mwnamke kwamba ana mimba?

BTW kama hamkuona kwamba ana mimba au kama mlimuona na mkamridhia kwa jinsi alivyo ni sawa tu. Ila ni vyema mkashauriana na mkeo katika hilo ili kuweza kulibariki jambo ili hata baadae kusitokee maneno yasiyo na tija.

Ila kama hamjatoa taarifa katika Serekali ya mtaa ni vyema mkafanya hivyo na pia kufanya taratibu za kumjua binti vizuri kuhusu familia yake na huko alipotoka ili baadae likitokea la kutokea mjue pakuanzia.
 
Usimtelekeze kisa kazaa kitoto. Lea kijukuu na Mungu atakujalia. Si bure huyo kaleta mibaraka nyumbani kwako na lazima atakuwa amekuja na riziki yake kutoka kwa Mungu, pengine kubwa zaidi kuzidi hata ile ya kwako siku zote, believe me!
 
Ahsante kwa ushauri wako mkuu;
Maswali yote majibu yake nafikiri akina mama mwalijua hilo, sisi wababa ni tofauti sana. Binti huyu alikuwa haoneshi dalili zozote za kuwa na mimba, kwa sababu kana mwili mkubwa kidogo kalionekana kama ni kanene tu; hivyo wote tulishangaa kitendo cha kujifungua kwake.
 
Usimtelekeze kisa kazaa kitoto. Lea kijukuu na Mungu atakujalia. Si bure huyo kaleta mibaraka nyumbani kwako na lazima atakuwa amekuja na riziki yake kutoka kwa Mungu, pengine kubwa zaidi kuzidi hata ile ya kwako siku zote, believe me!

Maneno ya namna hii ndo anayonambia mke wangu; ila mimi nahisi inaweza fika mda kakaondoka na kutuachia mtoto.
 
Be very careful Mkuu, Sheria inamaana yeke. Tafadhali sana waone Ustawi wa jamii watakupa ushauri mzuri na kuweka rekodi ya kiserekali kuwa huyo binti na Kachanga chake wanaishi na wewe. Siombi mabaya lakini Kuna (1) Vifo (2) Migogoro na baba mtoto na familia ya huyo binti --Ukidharau hili siku moja itakula kwako mkuu.

Ni vizuri sana kumsaidi binadamu mwenzako. Likini fuata sheria husika ili uwe na amani na kulinda familia yako.
Hapo umenena -ahsante sana.
 
Story yako inakuwa kama vile imerukaruka matukio na imenipa maswali.

Kama ni kweli huyo msichana ulimpokea wiki 2 zilizopita kama ulivyojieleza ni dhahiri kwamba alikua na tumbo kubwa hivyo ilikua ni rahisi kumtambua kwamba huyo msichana ana mimba.

Je wewe au mkeo hamkumuona huyo mwnamke kwamba ana mimba?

BTW kama hamkuona kwamba ana mimba au kama mlimuona na mkamridhia kwa jinsi alivyo ni sawa tu. Ila ni vyema mkashauriana na mkeo katika hilo ili kuweza kulibariki jambo ili hata baadae kusitokee maneno yasiyo na tija.

Ila kama hamjatoa taarifa katika Serekali ya mtaa ni vyema mkafanya hivyo na pia kufanya taratibu za kumjua binti vizuri kuhusu familia yake na huko alipotoka ili baadae likitokea la kutokea mjue pakuanzia.

soma chini utapata majibu kiongozi, mimba za kwanza huwa ni za ajabu kwa baadhi ya mabinti
 
Back
Top Bottom