Nimsaidiaje mtu huyu?

Nimefatilia comment za wengi humu naona wengi hawajui au hawajawahi kuishi kwa bajeti na nadhani ndio maana watanzania tunaendelea kulalamika kila siku hali ngumu. Tuwe wakweli kama ni watu tunaoishi hapa mjini, uchoyo ni nini? Hv mtu anajiwekea utaratibu wa kila siku anakuja kula kwako anatumia kila kitu chako hv huyo kawa nani mwanao, nduguyo, baba yako au mamayako? Hatukatai mtu kuja kwako kula kwa kipindi fulani haina shida kabisa, mtu mzima ana kipato kama wewe, kama alivyosema mtoa mada anapewa pesa ya matumizi ananunua vibato. Alafu mizigo yake aitue kwangu thubutuuuu, bora niitwe mchoyo. Kuna watu wao pesa zao za maendeleo tu hela ya kula ya kwako period
 
MamaBeata sio kwamba unaogopa zaidi atakuchukulia mumeo?

On a serious note, mwambie tu kiroho safey kwamba sasa ajitegemee kiujumla ikiwepo kujipikia

Hasa hasa kama mume wake ni mdogo wako...duh! atajiiba mwenyewe amsingizie binti wa watu.
MAMA Beata washasema wengi zangu hapa salamu tu!
 
Last edited by a moderator:
mamabeata, maisha magumu bana, kisa cha kuishi bila raha ndani ya nyumba yako? Hebu mpe makavu huyo mtoto kama vipi achangie hela ya msosi kwa mwezi hawezi akapike geto kwake au akale chips kwenye vibanda huko
 
ongea na huyo aliekuomba ukae nae huyo mtoto na pia ikibidi mpe live huyo binti kuwa ndoa yako ni changa aangalie ustaarabu wake maana watoto wa siku hizi balaa ukiwalea siku chache tu unakuwa mke mwenza.
 

marrykate we ndio ulimuweza. Ila afadhali ww alikua ndugu sasa mi huyu sina undugu nae wala nn. Yani hata kama akifanikiwa hawezi kukumbuka ukoo wetu.
 
Last edited by a moderator:


mmmh maman beata hata sijui nianzie wapi,
wengi tunakutana na hayo mambo, sio kwa watu baki tu lakini hata kwa ndugu,
ushauri wangu mimi muangalie na tabia yake kwanza kama ni nzuri, halafu mchukulie kama ndugu japo si ndugu
kama ana tabia nzuri sio mbaya akija mara moja moja, atakusaidia espcially kukupatia habari za wadad wa kazi ambao kwa kweli ni majanga
pia anaweza kukusaidia kazi mabali mabli za nyumbani...anapokula mpangi nza kazi kadhaa za kufanya, mfano akija kufua mpe na nguo zenu afue, aoshe vyombo, apike n.k ilimradi mshughulishe...akiona mwenyewe kazi zimemzonga atakata miguu kuja hapo..
siamini kama kweli chakula cha mtu mmoja ni bg issue sana, naaamini chakula cha watu 3 kinatosha wanne...n.k..

mimi kwangu chakula sio issue kama huyo mtu hana tabia mbaya...tatizo ni tabia, wengine utakuta anakukosanisha na wadada wa kazi au anakusema vibaya, au hasaidii kazi yoyote hapo nyumbani..hapo sawa unamuondoa..
nafikiri ungelichukulia in postive way kuliko negative..halafu huyo ni km mdogo wako unatakiwa umkalishe chini umfundishe hasa kama anachzea hela,
sio mbaya kumsaidia mwanafunzi, mdog wa rafiki yako esp kitu km chakula mi naona very minor issue..
kiukweli mi yaani uchoyo uchoyo wa ugali sinaga kabisaaa....tutakula hicho hicho kilichopo hata km ni dagaa...ila akiniboa kwa matabia yake hapo namuondoa ila chakula tu aleeeeee mpk ashibe
 

kamusi asante kwa ushauri kweli nimeutekeleza leo. Amekuja tulikua hatujamuhesabu kwenye menu ila tumemsihi asiondoke bila kula. Nimeutumia huo muda wa chakula kumshauri awe anapika na kumwambia awe anafulia kwao akasema maji hayatoki ila najua yanatoka maana line ya maji ni moja kwahiyo yakitoka kwangu na kwao yanatoka ila sikutaka kumuumbua. Nikamwambia ruksa kuja kuchota maji ila kufulia ni kwake hukohuko. Naamini kaelewa.
 
Last edited by a moderator:

Ha ha ha pole dada yangu. mijitu mingine kweli ni mzigo. mtoe tu asikukoseshe raha nyumbani kwako
 
Last edited by a moderator:
Jamani kwa nn wanawake wanaongoza kwa roho mbaya!?? Just ugali only unaleta JF!!? Mara ooo atanichukulia mume wangu hujiamini? Hayo umeamua kuongezea tu bt da major issue ni ugali (mavi), yaani ww ukikabidhiwa mtoto ambae huna undugu ndani ya mwezi waweza mlisha sumu ili asikuharibie budget Lol! Wa unga robo na nyanya chungu utawajua tu, NB: safisha ndani ya kikombe kabla ya kusafisha nje ya kikombe. Nalog off
 

yani we kweli no matter inaelekea ww ndo una tabia kama hizi za kiuwendawazimu. Usolijua litakusumbua mi sio wa unga robo. Usilete dharau kujifanya matawi ya juu utakuwa mzamiaji namba moja. Hivi ningekuwa na roho mbaya ningeishije naye siku zote hizo na ningemkaribishaje kwangu? Tumia akili. Angekuwa na busara angeaga kuwa asante kwa kunitunza siku hizo ili akaendelee na maisha yake sio kugeuza nyumba yangu ghetto la masela eboo.
 
pole sana mamabeata,ila watu wenye hizo tabia ni bora wapigwe tu,ndio tumechoka wapigwe tu mimi sioni sababu ya kuwavumilia wapigwe tu.
 

Ngoja nikupashe upashike mtoto wa kike, kwa taarifa yako wa unga robo na nyanya chungu ni wakarimu mno kwenye chakula kuliko hao wa mboga Saba. Uswazini wana maisha ya taabu na dhiki lakini wana upendo wa hali ya juu kuliko uzunguni...
Kama bi Dada mchoyo kwa mujibu wa maelezo yako si sababu ya umaskini alokuwa nao..
 

ukisoma ukaelewa utagundua tatizo si uchoyo wala umaskin. Kama watu mngekua wakarimu hivo mnavosema hata watoto wa mitaani wasingekuepo wote wangeshachuliwa majumbani kwenu muwalishe hayo mnayoyaita mavi (ugali).
 
Mama beta wadau wameshauri na wakaelekeza naamin kuna vitu umepata kupitia michango ya wadau. Je umeshachukua hatua yoyote kwa mhusika?
 
Mama beta wadau wameshauri na wakaelekeza naamin kuna vitu umepata kupitia michango ya wadau. Je umeshachukua hatua yoyote kwa mhusika?

BPM nimechukua hatua nilimweleza kiustaarabu nahisi kanielewa. Thanx for ur concern BPM
 
Last edited by a moderator:
Mamabeata. Futa kauli ya kusema wewe sio mchoyo vinginevyo mwache aendelee kuja hapo mpaka amchukue hata mumeo. Hata ndugu yako wa kuzaliwa lazima awe na mipaka nyumbani kwako, hapa duniani hakuna uhuru usiokuwa na mipaka. Mkalishe chini umwambie masharti ya kufika nyumbani kwako na mengine yote yanayostahili.
 

dada....hapo kinakushinda nini? fukuzia mbali.....mwambie dadake humtaki mdogo wake kwako....hasaidii chochote.... na isitoshe una bajeti yako.... angalizo beata.... mumeo c amekaa kimya? anaangalia msimamo wako....we muweke tu... atambandua ndo utajuta....
 
mimi mtu akiwa ni mama mwenye nyumba thn akashindwa kusimama kama mama wa mji ananikera!
UNALALAMIKA badala ya kutenda?
humtaki hapo nyumbani kwako,TELL HER !over!
mambo ya kujiumiza umiza moyo na makitu hata hayapaswi kukuumiza moyo ya nini!?
huu NI UNAFIK'!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…