Wisest man
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 993
- 333
MamaBeata sio kwamba unaogopa zaidi atakuchukulia mumeo?
On a serious note, mwambie tu kiroho safey kwamba sasa ajitegemee kiujumla ikiwepo kujipikia
Kama unaogopa kumwambia live basi time will tell siku akiwa anakuja na rafiki zake ndipo utajua cha kufanya! nikikusoma katikati ya mistari nakuona kama ni mtu ambaye sio mkweli kwa watu, yani unacheka hata kama moyo haukurusu kufanya hivyo, ulipoanza kukaa nae ulikuwa unaficha tabia yako halisi ili dadake asikuone kuwa wewe ni mchoyo, kwa sababu unaogopa kumwambia ukweli wewe ni mchoyo ila hutaki kujulikana tu na sifa kubwa ya wachoyo ni kuwachangamkia watu harafu mbeleni wanawageuka!! Jaribu kubadilika kwanza mwambie kivitendo kabla ya kumwambia kwa maneno endapo hataelewa kivitendo . lakini pia jaribu kumwambia hata huyo dada yake ajue kuwa mdogo wake hatumii pesa ipasavyo, na utakuwa umemsaidia sana, binafsi huwa siogopi kumwambia mtu ukweli kwani naona kama namuacha mtu afe huku namuona,ukimweleza ukweli hatarudia na wala hatajisikia vibaya kwani anajua kwamba anafanya makusudi.
Mama beata , hapo ni kwako na unataratibu zako za kimaisha. Huna sababu ya kumuonea haya cha msingi mkalishe umweleze .. Maadam umeshapata chumba unapaswa kukabiliana na maoisha ukiwa huko suala la kufua , kuoga afanyie kwake. Pia muulize / mnunulie jiko na umwambie tayar yeye ni mtu mzima ajitegemee na atengeneze maisha.
inawezekana nikawa nina tabia ya kuchangamkia watu usoni ila sio kwa nia mbaya. Tegemeo langu ni kua angeheshim makubaliano yetu. Dada yake aliomba akae siku tatu lakini alikaa wiki tatu. Mimi uchoyo sina ila navyoona huyu ni mtu opportunist hana aibu. Ukisema mimi mchoyo basi hujui how it feels kukaa na stranger asietaka kuiacha nyumba yako. Tena mwenye tabia za uvivu na dharau kwa wenyeji wake. Angekufanya umchoke tu hata kama ungekua wewe Wisest man
BPM asante kwa ushauri mzuri. Ila huyu jiko analo, sufuria na vyombo anavyo ila hataki kupika anasema kwao alikua hafanyi kazi sekondari kasoma boarding. Ila ntafuata ushauri wako nimweleze aweze kujitambua. Navomficha nimegundua hali itaharibika zaidi.
Kuwachangamkia watu siku ya kwanza bila kufahamu undani wa tabia yake ni mbaya kwani inamfanya akutafsiri namna usivyokuwa, kama hapo anapokuchukulia hivyo wewe ndiye uliyemruhusu awe hivyo kwani endapo ungekuwa mkali sidhani kama angetamani kupasikia kwako! mimi nakushauri umwambie kiustaarabu atakuelewa, ila usimwekee kinyongo.
binafsi sijakupenda kivileeee, sijakataa ndoa ni changa ila una katabia kauchoyo kishkaji. usimind mambo ya misosi tunakula na kunyw*. lalamika huna amani atakuibia mume lakini sio msosi. share ya mtu mmoja haiwezi kukuharibia bajet kihivyoooo
Bongo bwana!! Hii ni ishu ya kutafutia ushauri nayo?? Sasa wewe unaweza kuamua kitu gani kama ishu ndogo kama hii inakushinda??!!!!
Ukizubaa utachukuliwa mpaka mume!!au tayari keshabebwa!huyo mtu mmoja kila siku Sista? Tena anataka kulala tu asimsaidie msichana wangu wa kazi? Yani humu ndani tumekua wenye nyumba wawili. Kinachonikera hataki mapishi nayoagiza mimi. Mfano chai huwa napenda iweke tea masala anamwambia dada usiweke bwana mi sipendi. Wali tumezoea kuweka iliki ye anasema ya nn usiweke. Mi mtu wa kunipangia maisha yangu kwenye nyumba yangu simtaki hata ukisema mi mchoyo.