Nimfanyeje???

Damu ya nani tena! Nina mpango wa kumtafuta mume wake nikaongea naye.

Sijakuelewa mkuu. Unataka ukajitambulishe rasmi kuwa wewe ni Bw. Mwizi? Unataka kuijaribu sumu kwa kuilamba eeh!!
 
Pole sana, dalili kubwa ya msichana kuwa na kidumu kingine ni hiyo ya kutokuruhusu ufike kwake.
Pole sana once again........achana naye.
 
Sikuwahi kufika kwake hata siku moja. Kila nikimwambia niende ananiyeyusha na kukutana kwenye hotel jirani na anakoishi.
Da unatembea na mwanamke miaka miwili hujui anapolala, kosa kubwa sana hilo kaka labda ingekuwa ni one night stand ningekuelewa ila miaka miwili? jamaa mmoja alikatwa shingo kwa sababu kama hii ya mke wa mtu! kama unajipenda kaa mbali na ngoma za watu.
 

Si kwamba sikutaka kujua anapoishi, nilitaka ila mwenyewe anasema ipo siku ya kwenda kujitambulisha rasmi. Nyumbani kwa baba yake niliwahi kwenda kulikuwa na sherehe fulani nikapewa kadi. La kushangaza mumewe hakwenda, na bado wadogo zake wananiheshimu kama shemeji yao.
 
kudadadeki duuuu kweli mapenzi yanalaani dunia
 
Pole sana, dalili kubwa ya msichana kuwa na kidumu kingine ni hiyo ya kutokuruhusu ufike kwake.
Pole sana once again........achana naye.

Asante mkuu;
Nilianza kushtuka siku moja ilikuwa sikukuu ya Idd; akanikaribisha chakula cha pamoja, nilishangaa nilipompigia sim alinambia nimsubiri sehemu flani aje anichukue. Nilishangaa anashuka kwenye gari na mahot-port yenye misosi eti nulie pale hotelini na mambo mengine yaendelee kama kawa!
 
We jiandae KUNASA TU baaaaaaaass! Sasa mtu kakudanganya uso mkavu mara zote hizo what makes you think this time atakwambia ukweli!!!?

Lisemwalo lipo kama halipo laja!!!!!!!!!!!
 
Jiandae kunasana one day mkuu!!mke wa mtu sumu
 
Damu ya nani tena! Nina mpango wa kumtafuta mume wake nikaongea naye.
Heeeeeeeeeeeeeeeeeh! SIJAWAHI SIKIA MTU ANAJIPELEKA MWENYEWE KUNYONGWA, HAYA KAKA KILA LA KHERI.
KATIKA AKILI YAKO UKIENDA KUMWELEZA KUWA MKEWE ALIKUDANGANYA ATAKUELEWA, WAKATI ANAJUA ULIKUWA UNAKULA URODA WAKE? MM NADHANI ATAHISI UNAENDA KUMRINGISHIA KUWA WEWE KIDUME KUSHINDA YEYE. SASA UTAKIONA CHA MTEMA KUNI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…