Nimfanyeje???

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,618
Ni zaidi ya miaka miwili nimekuwa kwenye mahusiano na mwanamke ambaye daima huwa ananambia kuwa hana mume. Jana nikakutana ma rafiki yake ambaye yeye ananifahamu mi simfahamu. Nikasikia ananiita Shem - nikamuuliza shem kwa nani; akanambia shem kwa xxxxxxx. Nikamwambia simfahamu mimi. Huyo mama akanambia hivi "Pamoja na kwamba umesema humfahamu, mi nakufahamu na tayari mume wake naye anakufahamu"

Nimfanyeje? Nimwambie au nimchunie tu!
 
we fanya uchunguzi wako ujuwe ukweli, na ungemtumi vizuri uyo shem unayesema utapata ukweli ndo ujuwe atua za kuchukua

Ni sahihi, niliwahi kuambiwa siku za nyuma, nilipomuuliza akanikatalia. Siku moja nikaamua kukaa naye hadi usiku wa saa 5; then nikamsindikiza na kumpeleka anakoishi, hakutaka nifike nyumbani anakoishi. Huyo mudada alonambia jana wamepanga nyumba moja na huyo dem wangu.... nimfanyeje?
 
Jisalimishe Polisi na andikisha maelezo yako kabisa.
Maana naona dalili ya harufu ya damu ipo karibu
 
Jisalimishe Polisi na andikisha maelezo yako kabisa.
Maana naona dalili ya harufu ya damu ipo karibu

Damu ya nani tena! Nina mpango wa kumtafuta mume wake nikaongea naye.
 
Umeshawahi kufika kwake hata siku moja, au ndo hivo unaishia njiani kila siku?
 
Yalizaliwa Tanga yakakulia Tabora
 



Mmhhhh!!!!
 

Run away from trouble, mwache mara moja
 
Its very unfortunate kuwa wengi tunategemea jibu la mdomoni tu, Lazima sana tujifunze 'body language' maana hubeba zaidi ya 75% ya maana ya kitu mtu anachozungumza. ila ukitegemea kusikia peke yake utapotoshwa vingi sana.

Nakushauri ujitoe mapema sana, mke wa mtu ni sumu. Pia google namna ya kusoma na kuelewa 'body language' itakusaidia sana kuepuka majibu ya kuambiwa ambayo yanakuaga na upotoshwaji mwingi wakati mwingine.

 
Umeshawahi kufika kwake hata siku moja, au ndo hivo unaishia njiani kila siku?

Sikuwahi kufika kwake hata siku moja. Kila nikimwambia niende ananiyeyusha na kukutana kwenye hotel jirani na anakoishi.
 

Ahsante sana; mkuu
 
We ongea naye tu fresh, unaweza kumgonga na yeye. Anajipeleka kibla huyo
 
Naona dalili za kunatiana hapa.Mhh ngoja nipite nitasoma kwenye magazeti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…