Nimezaa na mwanamke mzuri lakini...

Nimezaa na mwanamke mzuri lakini...

jaribu tena uatapata anayefanana a mama,
ila ujue mwanaume hasifiwi sura
 
Kwanza kabisa nina sura baya kwa kweli hilo nalijua. Na baada ya kujua hilo, nikasema sitaki watoto wangu wawe na sura baya kama mimi.
Kwahiyo moja ya mkakati wangu ukawa kutafuta mwanamke mwenye sura nzuuri kabisa ili angalau ni dilute kidogo hili sura wasije nilaumu baadae.

Nikatafuta kwa nguvu zote mwanamke mzuri, yani nilitumia uongo grade ya juu hadi nikampa mimba huku nikijua hatuna future yoyote ila nikamdanganya ntamuoa nakadhalika ili tu ata ni dilute hii gene, maana kwetu wote reception ni majanga.

Mimmba ikalelewa hadi akagombana na ndugu zake wasionipenda, akakataa kuitoa kwasababu track niliyompa kwakweli alijua kampata mwanaume bora kuliko wote duniani, na pia alikuwa mgeni kwenye mapenzi hivyo akajua mimi ndiyo kila kitu.

Basi yoote yakaenda juzi usiku akazaliwa njemba. Mimi sikuwepo hospitali ila nilikuwa na safari ya kikazi nje, simu niliyopigiwa na besti yangu ni kwamba njemba inafanana na mimi kopirait pia wakaniwhatsapp. Pumzi zikaniishia kwenye simu. Nikajiuliza sasa hiki ni kitu gani tena? Yani pamoja na kuinvest muda waoote jamaa kafata tena ile reception yetu ya kule nyumbani? Imenidepress vibaya mno maana nimerudi leo nimemuona, du nimechoka. Ila namshukuru Muumba. Naombeni ushauri

Ushauri wangu muoe huyo Dada mzuri then umtafute handsome boy azae na mkeo halafu iwe siri yenu
 
Hii sikuitegemea ktk maisha yangu, naona kama umejidharau Sana..ooh!!
 
Unataka uzae hemed phd wakati wewe ni remmy ongala?

Btw, shukuru umezaa kidume, take it to school first, silaha ya kwanza ya kudumu katika maisha!

Then komaa na kusaka mkwanja, mengineyo baadae..

Remmy ongala anawatoto Handsome

Umeshamwona kali ongala kocha msaidizi azam fc.
 
Watu wana dhambi....yaani umeukosoa uumbaji wa Mungu kwa kiwango cha juu sana!! Huyo mtoto akishakuwa mzuri hivyo then what?!.... Kuna wanataman hata huyó mbaya lakin hawampati
 
Kamfanyie plastic surgery huyo mtoto, rekebisha pua, mdomo, masikio n.k ni ushaur tu
 
hahahahahaaaa, ungezaaa na mzungu , trust me ingejidilute vizuri and dont get me wrong, i like black women sana lakini kwa nyie wenye sura nzito wazungu wanawafaa
 
Oa huyo dada, kakukubali na sura yako mbaya halafu hukuwa na plan ya kumuoa? Binadamu hamuaminiki
 
Acheni kumsahihisha Mungu;
na ndiyo maana ukapewa tena hilo li poligon;
 
Inabidi wanasaikolojia wakusaidie best una roho ya kujichukia na kujikataa
huwezi kupinga mpango wa Mungu wa uumbaji wake kwani
kila mtu aliumbwa kwa mfano wake hivyo hakuna mtu mbaya duniani
 
Kwa hiyo huyo ndiye wa ukoo wa nyani?unawafahamu wote katika ukoo wao kumbe.
 
Huyo ndiye wa ukoo wa Nyani?Unawafamu wote katika ukoo wao kumbe..
 
Back
Top Bottom