Mr Bluetooth
Senior Member
- Aug 23, 2022
- 126
- 233
Habarini Wakuu..
niende moja kwa moja kwenye hiki kisa kinachoumiza akili yangu..
Mwaka 2011 nikiwa kidato cha kwanza pale shuleni kwetu kulikuwa na mwanafunz wa kike wa kidato cha pili mzuri kiasi wa sura na katako kakuvutia wanaume, wengi walimuita yeye ni mzuri wa shule kati ya wasichana wote pale shuleni. Wale walimu vijana na wengi wao ambao walikuja kufanya field pale walimsumbua mno maana alikuwa anashawishi sana kuwa nae , mzuri, msafi, mtaratibu, hanaga makundi ya hovyo, na shida ndogondogo pale shuleni hakuwaga nazo kiasi kwamba ingempelekea aweze kuliwa kimasihara kama ilivyokawa kwa wanafunzi wengine wa kike.
Licha ya hayo yote lakini uwezo wa kimasomo kwake haukuwa mkubwa. Hivyo ikapelekea yeye kufeli kidato cha pili na akareseat darasa, kwahyo tukasoma nae sisi tulipoingia kidato cha pili.
Tulivyokuwa tupo darasa moja vile na tutaonana kila wakati, nikajikuta shauku yangu ya mapenzi inakuwa kubwa zaidi kwake nilikuwa nimeanza kumtamani. Ikafikia kipindi namuangalia sana pale class mpka akawa ameshtuka kuwa namkata sana jicho akaamisha meza yake akaiweka nyuma zaidi ya nilipokuwa nakaa.
Pale shuleni kulikuwa na mwalimu ambae pia ni shangazi yake (dada wa baba ake mzazi) M/Munga amlaze mahali pema peponi, siku moja nimetulia class akafika dogo wa kidato cha 3 (namuita dogo coz alinizidi darasa ila nilimzidi umri) akanipa salamu kuwa naitwa idara ya Kiswahili. Nikachomoka zangu kuelekea huko, njiani nikawa najiuliza maswali kuna nn huko ofisi ya kiswahili maana mle mna wanoko tupu manguli wa adhabu shuleni. Nilivyoingia pale ofisini nikakuta kuna watu wawili tu, yule demu na madam ambae ni shangazi yake, nikawa nawaza pia au yule demu ameenda kushitaki kuwa namkata jicho sana na kumkonyezakonyeza.
Akanikaribisha niketi kitini na baada ya salamu, akaniambia "wewe ndie kipanga wa form two B ambapo huyu mwanangu pia anasoma, leo ajaingia darasani anasema.. " kabla ajaendelea simu yake ikawa imeita na akaipokea akawa anaongea zile dk 3 ambazo alikuwa anaongea na ile simu zilikuwa ngumu mno kwangu, moyo ulinidunda na kajasho kananitoka, namtazama yule demu namtusi kimoyomoyo kwann amekuja kumwambia shangazi yake wakati hata sijamtongoza! Yaani kumuangalia sana ndo iwe tatizo!.
Alipomaliza kuzungumza na aliempigia akaendelea "anasema ameshindwa kusoma na anataka kuacha shule anaona masomo magumu na anapoteza muda hivyo anajua atafeli tena akarudi tu nyumbani kwahyo bora aache shule aondoke, sasa nimeongea nae sana na amekubali kubaki ila ametaka mtu wa karibu wa kusoma nae. Hawa wanafunzi wenzake anaoishi nao hostel amesema hawataki, nimekuwaza wew ndo uwe unamsaidi kumuelekeza hayo masomo yenu, anapokwama umsaidie, kuanzia leo na ni jambo la kila siku mpaka atakapofanya mtihani wa kidato cha pili ili aweze kufahulu".
Baada ya mazungumzo ya dakika kadhaa tuliruhusiwa kuondoka na yule demu akarudi zake hostel kwakuwa akuingia darasan siku ile. Shule ile ni ya Kata na ina hostel za kike tu pale shuleni. Sie wa kiume na baadhi ya wanafunzi wa kike wanaotoka kata ileile tunatembea kutokea home kuja shuleni.
Siku zikasonga tunaelekezana ili na lile, nikaanza sasa kuzoeana na yule demu japo yeye alikuwa ni mtu wa aibu asiekuwa na story nyinginyingi, nikawa navutiwa nae zaidi, mpaka uzalendo ukanishinda nikaamua kumwambia jambo lililopo akilini, ilikuwa ijumaa tupo kwenye pindi la jioni nikamwambia "kuna kitu nataka tuzungumze," akajibu "ujawahi kuniomba tuzungumze unapotaka kusema kitu huwa unasema sasa leo vip!
Bhasi hiko kitu sio cha masomo sasa kama ni ishu zingine naomba leo tusome unielekeze hivi visubtopic then kesho utasema unachotaka kusema kwakuwa hatutokuwepo darasani." Ikabidi niwe mpole niendelee kumelekeza kama dakika 3 mbele nikiwa naelekeza kitu akanyanyuka na kuondoka nikamuuliza vipi mbona unaondoka hatujamaliza, akasema "sielewi kitu unachonielekeza kipindi umeshakiharibu wewe mwenyewe tutaonana kesho tuzungumze hilo jambo lako." Akasepa zake hosteli...