Nimewamiss Sana Hawa Wanasiasa Wakiwa kwenye Uhalisia Wao.

Director D

Senior Member
Feb 24, 2016
192
250
Hapo zamani kidogo siasa ilikuwa tamu sana kwa kuwa kulikuwepo na viongozi mbalimbali waliokuwa na hoja za msingi na mashiko makubwa kwa maslahi ya taifa.
.
.
Kwa bahati mbaya sana baadhi ya viongozi hawa wamebadilisha kabisa mitazamo yao na sasa ni wapya kabisa
.
Hawa ndio niliowamiss
1. Dr Slaa
Kuna wakati niliamini kuna siku huyu mtu angekuwa rais wa hii nchi kutokana na hoja na mitazamo yake makini hapo zamani ila sijui hata yuko wapi siku hizi
.
2. H. Polepole
Nakumbuka wakati wachakato wa katiba mpya kila mtanzania alikuwa kipenzi cha kijana huyu kutokana na msimamo wake juu ya katiba ya wananchi ila sijui nini kimempata siku hizi. maana.....
.
3. Prof Kitila Mkumbo
Huyu msomi nae nimemmiss sana akiwa katika uhalisia wake wa kujenga hoja zenye utashi mkubwa ila siku hizi ni kama amezaliwa upya Maana......
.
4. James Mbatia
Amekuwa kimya kwa siku nyingi sana naye nimemmiss kuona akitema cheche zake,
.
5..........
n.k
.
Je wewe umemmiss nani..???
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
6,691
2,000
MKUU KWANI SIKU HIZI WAMEPOTEZA UHALISIA WAO???AU NI MABADILIKO YA KIMBINU TU
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom