Nimevunja kibubu muda huu nimekuta 2,000 na mke wangu anasema hela hajui ilipo!

kinyamkela mahaba

JF-Expert Member
May 4, 2022
1,181
1,574
Jamani za wikiendi, nilikuwa na utaratibu wa kuweka 1,000 kila siku kwenye kibubu chetu na mke, ni miezi mitatu sasa.

Ilitakiwa leo nikute 90k na kidogo, ila nimeikuta 2000 tu. Nimehamaki na kumuuliza mwenzangu ananiuliza zile nyama na ile mikate ya mayai aliyokuwa ananipikia hela alikuwa anatoa wapi?

Baada ya kumbana mno kwa maswali ndiyo akafunguka kuwa alikuwa anachukua yeye na ananunua mahitaji hayo tajwa, ambayo kimsingi hayakuwa na ulazima wowote. Usiku huu naona utakuwa mrefu mno kwangu, mwenzangu ndiyo anakaribia kupitiwa na usingizi muda huu.

Yaani kutoka 90k mpaka 2k kwa mikate ya mayai na nyama mara 3 au 4 kwa wiki? Hayupo serious kabisa huyu mke wangu.

Anathamini mno vyakula vizuri kuliko maendeleo. Ni kweli tulifululiza mno kula nyama na mikate ya mayai na sikujua kuwa anachukua akiba yetu.

Dah!
 
Fanya maendeleo kivyako achana na mwanamke, hao wana mambo mengi na tamaa za kitoto.

Usingepungukiwa kitu kuhifadhi hizo pesa kwenye M-Power ama Tigo kibubu, sas utakula ulkopeleka mboga.

Mnajifanya kupenda mapenzi ya demokrasia na hayo ndyo malipo yenu, mwanamke si wakufanya nae mipango ya maisha ingewezekana kazi yako iwe kumpa mahitaji ya muhim tu na sio kufanya nae saving.

Tukiwaambia KATAA NDOA mnaona tunawatukana? Kwanza unaoa vip wakat hujaweka hali vzr ya maishayaan mkeo asile vzr kisa kusave pesa kwa kibubu?

Pambana umpe tena aweke
 
Kuna nyumba sister wa mama mkubwa kapanga kino. Alinunua kibubu akawa anaficha ila akifungua hakuti Hela akaanza ugomvi na mumewe. Ila baadae akawa anaficha kweli kweli na akawa hakuti na mumewe yuko kazini sio mtu wa kushinda akaja gundua mmoja wa wenye nyumba alikuwa Kila siku anamwaga madawa kumbe Hela zikawa zinapotea kimazingira. .

Ila pia hivi vibubu uwe unaangalia vingi vina kuwa na uchawi wa kupoteza pesa. .

Tatu unachanganya Hela ya chuma ulete kwenye vibubu. Kitu ambacho kinafanya Hela zipotee.

Mwisho kabisa acha kuweka Hela kwenye vibubu. Na wenzako wanaweka 200 kwa sababu hazipigi kutu ukiweka Hela za noti Huwa zinaharibika. .
 
Jamani za wikiendi, nilikuwa na utaratibu wa kuweka 1,000 kila siku kwenye kibubu chetu na mke, ni miezi mitatu sasa.

Ilitakiwa leo nikute 90k na kidogo, ila nimeikuta 2000 tu. Nimehamaki na kumuuliza mwenzangu ananiuliza zile nyama na ile mikate ya mayai aliyokuwa ananipikia hela alikuwa anatoa wapi?

Baada ya kumbana mno kwa maswali ndiyo akafunguka kuwa alikuwa anachukua yeye na ananunua mahitaji hayo tajwa, ambayo kimsingi hayakuwa na ulazima wowote. Usiku huu naona utakuwa mrefu mno kwangu, mwenzangu ndiyo anakaribia kupitiwa na usingizi muda huu.

Yaani kutoka 90k mpaka 2k kwa mikate ya mayai na nyama mara 3 au 4 kwa wiki? Hayupo serious kabisa huyu mke wangu.

Anathamini mno vyakula vizuri kuliko maendeleo. Ni kweli tulifululiza mno kula nyama na mikate ya mayai na sikujua kuwa anachukua akiba yetu.

Dah!
Bro tafuta wimbo wa Dizasta vina unaitwa wimbo usio bora. Pole sana kwa kupata mwanamke mpumbavu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom