Nimeuza kiwanja na kununua simu ya ndoto yangu

Mkuu kwanza hongera kwa kutimiza ndoto yako,unapoamua kutimiza ndoto usigeuke nyuma kamwe cha msingi angalia namna ya kutumia hiyo simu kukuingizia kipato.
 
Ni nzuri mkuu, ina specifications za maana kabisa mkuu. Mimi hata kwa 2.5m nakuachia, kikubwa tugawane hasara, nitajua ni biashara ipi nitafanya ili kurudisha heshima kwenye ukoo japokuwa mpaka sasa hakuna anayejua hii issue
Nielewe nilichokuomba.

screenshot specification za simu,

ipige picha mbele, nyuma na pande nyingine kisha weka hapa tuione simu vizuri

maneno mengi hayasaidii
 
Naombeni mnipe moyo ili nisiugue presha mwenzenu, nafsi inatapatapa maskini
emoji24.png
emoji24.png
, bora hata ningefungua biashara.
dogo mjinga sana wewe
 
Habari wakuu,

Hapa nilipo nimejaa kitete siyo poa. Yaani hata sielewi, ingawa maamuzi niliyoyachukua nilishauriana na moyo wangu nikaridhika, lakini still nafsi inanisuta.

Nimeuza kiwanja changu cha urithi nilichopewa kwenye mgao wa familia, tena kiwanja kilicho barabarani kabisa. Nilitakiwa kukiuza kwa Tsh. Mil 18 (atleast), lakini nimejikuta nakiuza kwa milioni tano ili ninunue simu ya ndoto yangu kabla haijatoka kwenye chati.

Tayari nishafanya yangu. Nimenunua kitu cha Samsung Galaxy Z Fold 4 kwa Mil. 4 na laki 9. Hapa mfukoni nimebaki na laki tu. Kiwanja kimeenda. Naombeni mnipe moyo ili nisiugue presha mwenzenu, nafsi inatapatapa maskini, bora hata ningefungua biashara.

Nilivutiwa na hii simu kwa sababu imekaa kama kitabu, nikiifungua inaungana vioo viwili inakuwa kama ka TV kadogo, kamera safi na hadhi ya kimataifa.

Moyo umejaa kitete, nifanyeje? View attachment 2428948
laki iliyobaki nunua kifurushi yote hapo itakua umeshamaliza Mchezo mkuu
 
Naomba msaada wako wa kimawazo mkuu. Maji yameshamwagika, hayazoleki tena Muacheni kunilaumu tupange tujue tunafanyeje wakuu
Msaada ilipaswa uombe kabla hujauza uwanja. Isitoshe kuuza kitu chochote cha urithi wakati huna kitu ni laana,wewe unaweza kujiuza hata mwenyewe.

Sasa basi hapo ni kuwarudishia hela yao. Fanya vyovyote vile hata kujifanya hukuwashirikisha baadhi ya ndugu. Hao ndugu wafanye waje juu. Hao uliwauzia kama ni milioni 5 wape milioni 5.5 ya usumbufu. Uza hiyo simu haraka,japo utauza si sawa na ulivyonunua. Utajua kwa kuongezea hela za kutosha kuwarudishia.
Badaa ya hapo najua inaweza kuwa maeneo fulani in dar. Ukifanikiwa kurudisha eneo,fungua carwash hapo hata kwa kujibanana. Tafuta sehemu za carwash wana wawili wanajua kuosha,anza nao kuosha mwenyewe kuosha magari. Hakikisha unajifunza vizuri hiyo kazi.
Nakuhakikishia ukifanikiwa hayo,utakuja kubadiri simu kama hizo hata 5 upendavyo. Pia kupitia hiyo carwash itajenga yenyewe vyumba vingine hapo vya kupangisha vya biashara. Patakupa hela hapo.
(Japo kwa akili yako hiyo sina uhakika ushauri wowote kama utakusaidia). Maisha ni uvumilivu kwanza na kujituma sana. Utafikia malengo. Usiwe na haraka na unachohitaji.
 
Simu pekee yenye hadhi ya kununuliwa kwa zaidi ya milion moja ni iphone pekee, hayo mengine utajutia tu
 
emoji24.png
emoji24.png
Mkuu, kwa mfano nikiirudisha wakaikubali, hakuna namna ninaweza fanya ili kubatili mauzo ya kiwanj

Mkuu, kwa mfano nikiirudisha wakaikubali, hakuna namna ninaweza fanya ili kubatili mauzo ya kiwanja?
Dukani hawataikubali maana nao walikuwa wanangoja mzembe ajilete wampige, na Mwenye kiwanja nae hatochukua maana anajua kakupiga, dukani watataka wakurudishie milion 2
Na aliechukua kiwanja atataka milion9 kwenda mbele, kifupi we umepigika
 
GENTAMYCIME huwaita mapopoma watu kama hawa 😂😂

Samsung zilivyo mbovu ikizingua kidogo tu hela yake imeenda na akimkumbuka marehem aliemwachia kiwanja cha urithi basi roho itamuuma zaidi 😂😂😂😂
Mkuu, sema walau neno moja la kunifariji. Yaani nahisi kufa kufa mkuu
Fanya urudishe dukani Mkuu waeleze kuwa umepata shida kama jamaa ni muelewa na simu bado ipo kwenye ubora wake anaweza kukupa hela.
 
Kwa hiyo umekuja humu kuipigia promo Samsung Galaxy kidizaini eeh?

Tafadhali lipia tangazo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom