Nimesoma hadi chuo kikuu, ila bado ni MTUMWA

Nimesoma hadi chuo kikuu, ila bado ni MTUMWA

Idn

New Member
Joined
Sep 28, 2021
Posts
3
Reaction score
1
Nimesoma hadi chuo kikuu, ila bado ni MTUMWA, elimu kabatini kichwani hamna kilichobakia, niliambiwa kuna uhuru lakini bado ni MTUMWA.

Nawe kama ulisoma usichopenda ni MTUMWA, ulifuata mkumbo ni MTUMWA, uliyenunua mitiani kupendezesha vyeti ni MTUMWA, upo tu hufanyi chochote unasubiri ajira ni MTUMWA, unafanya kazi usiyoipenda ni MTUMWA, Unafanya kazi ili kupata tu pesa ni MTUMWA.

MTUMWA hatatoka utumwani mpaka atakapo kubali na kuamua kuwa huru.

Wengi wapo huru kimwili, ila kiakili ni watumwa, aliye huru kiakili atauokoa mwili, na aliye mtumwa kiakili atauangamiza na mwili.

Elimu imetufanya wa Tanzania wengi kuwa watumwa wa kifikra, wengi kusoma tusichokipenda, na kushindwa kukiishi.

Uwe wa mwisho, ushauri wangu.

1. MTUMWA, USIMLAUMU MTU.

2. USIMCHAGULIE MTU MASOMO YA KUSOMA

3. ELIMISHA WATU WASOME WANACHOPENDA SIO KINACHOPENDEKEZWA.

Kipaumbele cha kusoma si kupata pesa au kazi, ila kuisaidia jamii katika utatuzi wa changamoto mbalimbali.

Ubunifu, uwajibikaji, uzalendo, moyo wa kujitolea, nidhamu, uchapakazi, uadilifu, mapenzi ya kweli katika kazi na UHURU WA KIFIKRA upo na utakuwepo ikiwa mtu amesoma au atasoma kile anachokipenda.

UHURU, mtu kuipa jamii kipaumbele na kuwa tayari kuisaidia wakati wowote katika utatuzi wa changamoto fulani, upo ikiwa mtu amesoma au anafanya anachopenda.

Wewe si MTUMWA! Ee unaweza kuwa HURU. KUWA HURU, FANYA UNACHOPENDA.
 
Back
Top Bottom