Nimesimama! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimesimama!

Discussion in 'Entertainment' started by Mchaka Mchaka, Mar 28, 2011.

 1. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Artist:II Proud a.k.a Mr.II
  Song:Nimesimama
  Album: Ndani Ya Bongo(1997)  Akili inanituma kusema nasimama asubuhi na mapema,
  nafungua macho naona ktu ambacho kwangu ni kama kiwingu we polisi njoo na pingu,
  maisha haya ni mabaya ndio maana vijana wanapenda kwenda ulaya ,
  na wasichana wanaamua kuwa Malaya,
  ni nani amlaumu nani, yeyote popote, usifanye chochote waachie watu wote ni wakati uwazi
  mbona mi nikisema unabaki mdomo wazi, we kiongozi,
  umeshafanya nn na utafanya nn mwakani,
  kabla hujanipeleka gerezani, niskilize kwa makini nasema nn,
  mi naasa muziki sio anasa ni siasa na sasa nasimama nasema mambo mema Kwa nchi yangu njema.

  Chorus
  Nimesimama..akili inanituma kusema ..na we simama
  sikiliza ninachosema..nimesimama x 2

  Kwenu maisha ni matamu,
  kwetu ni magumu ndio maana tunalaumu.
  Vita inayoendelea kati ya polisi na wamachinga,
  wengi tunapinga ni vipi mi nirudi kijijini wakati mbunge wangu yuko mjini,
  anatunua na shangingi mi nna akili nyingi toka msingi mpaka sekondarii, ila naona hatarii kwenda chuo kikuu naogopa FFU watanivunja miguu ntapogoma kusoma mi nasema ili msije kusema mi sikusema,
  siku za nyuma mama alisema dunia tambara bovu inanibidi niwe shupavu, wako wanaoniona mi mpumbavu na wako mi mwerevu maisha ndivyo yalivyo kila ktu ovyo ovyo kampeni za uchaguzi zaambatana na matusi sijapata kusikia ni demokrasia au ghasia………
  ……………..
  Repeat chorus.
  --------------------------------------------------------------
  Hizi ndio zilikuwa message kwenye nyimbo nyingi za enzi hizo.
  mambo haya ya kubana Pua, wanaume kutoga masikio, kuweka kalikiti(km diamond) hayakuwepo enzi hizo. Duh natamani muziki huu wa kizazi kipya ungebaki kama zamani.
   
 2. inamankusweke

  inamankusweke JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2016
  Joined: Apr 24, 2014
  Messages: 3,449
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  umenikumbusha mbali sana,albam hii na king kong nilizinunua,mshua akawa ana-mind siipumzishi radio yake panasonic bouble deck
   
 3. inamankusweke

  inamankusweke JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2016
  Joined: Apr 24, 2014
  Messages: 3,449
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  Nikumbushe pini zingne za albam ile 'ndani ya bongo' manake nilizimeza zote ati leo nimesahau
   
Loading...