Kila kitu kimesimama! Barabarani hakupitiki, watu hawafanyi kazi kisa kifo cha Steve Kanumba. Ninaangalia TV watu wengi wapo leaders kumzika SK! Hilo taifa ni la wajinga Kama viongozi wake! Watu wote Hawa walio leaders hawazalishi kitu! Taifa maskini na wananchi wake maskini vichwani. Lowassa nadhani hakuhangaika na Huu msiba wa kisanii
RIP Kanumba
Rt Rev Masa
Una maana gani? ni uzembe uliopitiliza watu kujazana Leaders badala ya kujikita kwenye uzalishajimali, si wote ambao wako pale kwamba ni kweli wanaomboleza. siamini hilo na hata siku moja siwezi kufuata Mkumbo wa kwenda kwenye msiba wa mtu ambaye sikuwahi kufahamiana naye na wala siyo Kiongozi wa Kitaifa....ama kweli duniani kuna watu na viatu.....
Au jana jumatatu.Kamati ya Mazishi hovyo sana! SK angepumzishwa Jmosi siku ambayo si ya kazi!
Utakuwa umelogwa wewe AMA unapepo! I'm talking from economic point of view! Ujinga Huu watz hao walio leaders hajafanya kazi yeyote ya kuzalisha
hawa viongozi wetu wa serikal,
kwenye msiba wa dr remmy ongala mbona hawakujitoa sana kama huu?
Kuhangaika na misiba ni jadi yetu Waafrika na Kanumba (RIP) bila shaka alikuwa na umaarufu mkubwa kwa Watanzania wenzetu wengi. Lakini ukweli mwingine uliopo hapa ni wa wajanja wengi kupata fursa "adhimu" ya kujipa ujiko katika msiba huu. Hawawezi kuiacha ipite hivihivi. Na kama kawaida yao kila mkulu lazima akauze sura na kujinasibu hapo (penye umaarufu) kama vile itafidia utendaji duni kwenye majukumu yake ya msingi; kama vile alikuwa na mchango wowote wa maana katika umaarufu aliofikia bwana mdogo huyo. Sie wengine tungefurahi kuona hamasa ya aina hiyohiyo katika masuala yote muhimu ya kitaifa - hata katika kuikuza sanaa nchini.
Kila kitu kimesimama! Barabarani hakupitiki, watu hawafanyi kazi kisa kifo cha Steve Kanumba. Ninaangalia TV watu wengi wapo leaders kumzika SK! Hilo taifa ni la wajinga Kama viongozi wake! Watu wote Hawa walio leaders hawazalishi kitu! Taifa maskini na wananchi wake maskini vichwani. Lowassa nadhani hakuhangaika na Huu msiba wa kisanii
RIP Kanumba
Rt Rev Masa
kila jambo na wakati wake mkuu, yawezekana leo akafa msanii mwingine watu wakaw mara 100 zaidi ya hawa waliohudhuria msiba wa Kanumba, hata wakati wa msiba wa Dr Remmy tulisema watu walikuwa wamefurika..
all in all watanzania ni wavivu sana badala ya kuzalisha wameenda misibani, na kuna washikaji wamesafiri kutoka Iringa mpaka Dar kuja kuhudhuria mazishi yaani wameacha vipindi chuoni kisa msiba
Inabidi uelewe kwamba kwa wasanii wa television na sinema, kuwaangalia kila siku unajenga uhusiano nao japo hawakufahamu, na uhusiano huu unakuwa mkubwa sana kama vile ni rafiki zako wa karibu. Ndio kinachowapa hawa wasanii "celebrity status". Hivyo wanapokufa watu wengi huhisi kupoteza mtu wa karibu sana. Mifano halisi ni watu walivyohisi juu ya kifo cha Michael Jackson, Bob Marley, Whitney Huston, Bruce Lee nk. Hivyo usishangae kuona shughuli zimesimama kwa ajili ya mazishi ya Kunumba.
Kila kitu kimesimama! Barabarani hakupitiki, watu hawafanyi kazi kisa kifo cha Steve Kanumba. Ninaangalia TV watu wengi wapo leaders kumzika SK! Hilo taifa ni la wajinga Kama viongozi wake! Watu wote Hawa walio leaders hawazalishi kitu! Taifa maskini na wananchi wake maskini vichwani. Lowassa nadhani hakuhangaika na Huu msiba wa kisanii
RIP Kanumba
Rt Rev Masa
Ripoti kutoka makaburi ya Kinondoni mazishi yameshakamilika muda huu ila watu hawataki kuondoka!!......wengine wanahojiwa na mwandishi wanasema eti ilibidi mwili wa Kanumba ukae siku 3 pale Leaders ili waage vizuri, namuhurumia sana mtu anayetamani kuwa Rais wa Nchi kama hii, sidhani kama wana takwimu sahihi ya nchi yao ilivyojaa mambumbumbu na wasiojuwa hata kwa nini wapo Duniani.Kwa kweli inasikitisha, Watanzania tunatakiwa tutafakari, ndo kusema watu hawana kazi za kufanya. Tujifunze kutoka kwa mataifa yalioendelea. Jesus aliwahi kusema ''Waache wafu wakawazike wafu wenzao''