Genius Man
JF-Expert Member
- Apr 7, 2024
- 3,560
- 7,914
Nimesikitishwa kuona watu wamekamatwa baada ya kuzuia watu wasio na sifa kuandikishwa kupiga kura kwasababu hawana sifa, baadhi yao nimesikia katika vyombo vya habari ikiwemo JamiiForums kuwa walizuiwa kwasababu wananchi wa eneo hilo waliwatambua kuwa sio wakazi wa eneo hilo.
Hii inaweza kupelekea hawa watu wasio wakazi wa eneo hilo kujiandikisha zaidi ya mara moja na ukizingatia uandikishaji wetu hauna utaratibu wa kuhakiki mtu utambulisho wake.
Nilishauri kuwe na utaratibu huu wa kukagua utambulisho wa mtu hata kwenye kitambulisho chake kutaonesha mtaa anao tokea ili kuthibitisha kwamba ni mkazi wa eneo flani na kama yupo kwenye mkoa mwengine na anahitaji kuandikishwa lazima awe na barau hata ya mjumbe ili kumthibitisha utambulisho wake.
Sikuizi hata ukitaka kufungua account JamiiForums unatakiwa uthibitishe email yako lakini sisi kwenye mambo ya msingi na muhimu zaidi tumeshindwa kuweka utaratibu mzuri wa kuhakiki wapiga kura hali inayo pelekea hata zile sheria zetu za uchaguzi kuwa kama mapambo tu haziwezi kufanya kazi ipasavyo.
Kumbuka kuto kuhakiki wapiga kura kunaweza kupitisha watu wasio na sifa kujiandikisha kupiga kura hali inayoweza kupelekea kuvurugika kwa uchaguzi mzima.
watanzania waliokamatwa hawakutakiwa kukamatwa bali tulipaswa turekebishe sheria zetu za uchaguzi kuwe na uhakiki wa taarifa mambo kama haya yasingetokea hivyo watanzania waliokamatwa hawana hatia waachiliwe.