Nimeshushiwa amri kumi za kisiasa hapa Tanzania

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,598
3,644
1. Ipende nchi yako ya Tanzania kuliko chama chochote cha SIASA.

2. Iheshimu mamlaka ya nchi kwani kila mamlaka hutoka kwa MUNGU

3. Usimtamani mwanachama wa chama kingine, wala mali zake wala chochote alichonacho.

4. Usiwe kigeugeu au muongo kama viongozi wa CHADEMA

5. Usiwe mnafiki kama viongozi wa CCM kwa kuipinga katiba ya nchi yako

6. Usiwe FISADI wa mali ya umma wala mali ya nchi jirani.

7. Usichonganishe Watanzania kwa udini au ukabila.

8. Usitafute uongozi kwa njia za kishirikina

9. Usitoe wala kuchukua Rushwa

10. Simamia haki, usawa na maslahi ya Watanzania wote
 
16.Usimiliki gari ya thamani kubwa tsh.400,000,000/= Wakati wananchi wako wanakosa dawa mahosipitalini
 
21. Usinunue kivuko chakavu.
22. Usiuze nyumba za umma.
23. Usijenge barabara mbovu.
24. Usidanganye utatumia gari halafu ukatumia ndege.
25. Usijifanye unayajua maadili halafu ukauza pembe za ndovu na kuwapitisha mafisadi wa escrow kugombea ubunge.
26. Usiwakashfu wapiga kura na walipa kodi, eti malofa na wapumbavu ili hali ndio wanaokufanya ule na kupumzika.
27. Usipakie Twiga kwenye ndege.
28. Usilipe mishahara hewa.
29. Usizurure sana duniani.
30. Usiwadanganye watu utawaletea maisha bora ili hali wewe dhaifu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom