Nimeshawasili ndani ya tunduru

Nimeshawasili ndani ya tunduru

SAM_0055.JPG

Haya magari yapo Tabora kwa wingi sana, yanaitwa enzi a Mwalimu!!
 
mwalimu hajui hata vitu vya kusifia.......mahali popote ni pazuri pakiwa na miundombinu ya uhakika kama maji,umeme,hospital,barabara na network .....kuniambia ni kuzuri sababu wali nyama ni 1000 ?

Kuna watu mnajiona mnajua sana vitu...taste and preference lazima
Ziwe tofauti na usidelute profession yetu kwa feelings zako
 
We huweZI ushazoea pesa nyingi huko mnapewa rushwa mnanunua maprado, sis walimu ngumu sana na tunavumilia mengi

Mkuu huku mbwembwe tu hamna kitu unakuta mtu title kuubwa kama vile mchumi huku mshahara tgs D....

Mi kilimo ndo kinanitoa
 
Ndugu wana JF (Jukwaa la Elimu)
Nawashukuru sana wale wote ambao walinipa taarifa juu ya wilaya hii ya Tunduru. Nawashukuru sana nimeshawasili hapa nashuhudia fahari mbakimbali zilizopo hapa kama vile:
  1. umeme wa uhakika kwa hapa mjini
  2. mitandao ya simu inashika(hadi JF ipo)
  3. chakula ni bei rahisi sana ( wali nyama tsh 1000)
  4. kuku wa kienyeji wanapatika kwa wingi ( supu pia ipo)
  5. Maduka ya kununua madini yapo kwa wingi sana
  6. biashara ya korosho imeshamili

NB
Sasa nasubiri siku ya jumanne ifike nijue nitapangiwa wapi
Walimu wenzangu ambao mmepangiwa vituo mbalimbali ni vyema mkaenda kuripoti kwanza mshuhudie hali halisi wenyewe, kuna habari za upotoshaji sana, zinazotolewa na watu ambao hawajafika maeneo husika,mf Kuna mtu aliniambia hapa Tunduru kuna simba wanatembea mchana, mpaka jioni hii nimewatafuta sijawaona

mtandao gani unashika vizuri hapo tunduru?
 
Umepitia tunduru masasi if so vipi barabara ina hali gani kuanzia mangaka
 
Kuna watu mnajiona mnajua sana vitu...taste and preference lazima
Ziwe tofauti na usidelute profession yetu kwa feelings zako


Halafu anaponda huku amesahau kwamba hitaji la kwanza la binadamu ni chakula na sio miundombinu. Jamaa kusifia wali nyama buku sawa kabisa,
 
Back
Top Bottom