Nimeruka mtego wa 2 na Rais Magufuli

Nimeruka mtego wa 2 na Rais Magufuli

sangujoseph

Senior Member
Joined
Nov 30, 2015
Posts
164
Reaction score
184
By Sangu Joseph
.
Leo March 22 , 2020 nimemsikiliza kwa makini sana Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, na nimeendelea kumsoma zaidi nakujua ni kiongozi ambaye anaujua uhalisia wa wananchi anaowaongoza, kama ambavyo Mimi niliwaza majuma kadhaa yaliyopita. ( Nilipita kituo cha Daladala, Sokoni, Mama Lishe, NK niliwauliza unaweza kumudu maisha bila kufanya kazi na utumie akiba yako tu, baadhi ya walinieleza uwezo wao ni wa siku 2 wengine waliniambia broh hata hiyo akiba hatuna, tunajua tutatuma nini nyumbani tukishafika kwenye mishe)

Licha ya kelele nyingi za muda mrefu juu ya kutangazwa kwa Lock Down, katik jiji la Dar es salaam, lakini yeye amekuja na maamuzi ambayo kwangu nimeyaita kama kuruka mtego wa pili ambao wapinzani wake wangetamani auingie na iwe ngumi yao ya kumpigia hapo baadaye (Soma mtego wa 1 aliouvuka Magufuli Hata mimi ningefanya kama Rais Magufuli - JamiiForums )

Ni kweli tunajua kwa sasa DSM ndiyo inaongoza kuwa na wagonjwa wengi wa Corona kuliko mikoa mingine (Hii ni kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu Mil. 6 jumlisha na wale wanaoingia na kutoka) tuendelee kutumia nafasi zetu kuwahamasisha kuchukua tahadhari ya kujilinda.

Kwanini nasema Rais Magufuli amevuka mtego huu wa Kulock Down DSM, kwa asilimia kubwa sana ya Watanzania hawana uwezo kumudu maisha ya bila kufanya kazi kuanzia siku 5 wengi wao wakisogea sana siku 3 na wengine huwa wanajua watakula nini baada ya kwenda kutafuta asubuhi.

Sasa mtego ungekua hapa endapo Rais angeruhusu lock Down maana yake shughuli za kiuchumi na uzalishaji zisingefanyika ndani ya Dar es salaam na hata nje ya DSM (Imagine wewe ndiyo Rais unawafungia watu Mil 6 asilimia 80 hawana uwezo wa kusurvive kuanzia siku 3, ungeongozaje)

Hivyo uamuzi Kulock Down DSM, ungepelekea idadi kubwa sana ya Watanzania ambao hawana uwezo wa kumudu maisha kwa muda mrefu tungesikia taarifa nyingi mno juu ya athari za njaa, Vifo na pengine hata kuongezeka kwa matukio ya kiuhalifu kwa sababu watu wanasaka chakula na kujikimu.

Hivyo badala ya kuwaponya watu na Corona tungewaua watu kwa njaa, na matukio ya uhalifu hilo, kwa uamuzi huu wa Rais Magufuli kwangu ameruka mtego mwingine nampongeza sana.
.

Insta : FB ; Twit : Sangu Joseph
.
#KijanaMzalendo #IloveTZ

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni mtihani mkubwa sana kwa Raisi wetu, lakini COVID-19 nayo ni mtihani mwingine mkubwa mno.
Sijui itakuwaje mwezi wa tano (May) wa mwaka huu 2020.

Mungu amjalie hekima zaidi atuvushe salama bila wengi wetu kupoteza maisha kwa ugonjwa huu au kwa njaa.
 
Hii ishu kuna Padre aliwahi kuongea wiki moja kabla ya Pasaka kuwa TZ lock down ni ngumu sana kwasababu watu wengi hawana uhakika wa maisha,kipato kinasumbua sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lockdown si nzuri hata kidogo hii Ni kutokana na uchumi wa nchi,kikubwa Ni kupunguza misongamano mfano vituo vya mabasi Ni vyema wale wapiga debe waloweshwe virungu vya kutosha asibaki kenge stendi ambae hasafiri wawepo wasafiri na ofisi za mawakala tuuuh wakata tiketi tena kwa kipimo cha kampuni wakala moja na tiketi nyingine zikatwe mtandaoni

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
*NIMERUKA MTEGO WA PILI NA RAIS MAGUFULI*

*Na Sangu Joseph*

Leo Aprili 22 , 2020 nimemsikiliza kwa makini sana Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, na nimeendelea kukujua kwamba ni kiongozi anaeujua uhalisia wa wananchi anaowaongoza.

Majuma kadhaa yaliyopita, nilipita sehemu mbalimbali na kuwauliza wafanyabiashara wadogo wakiwamo mama lishe iwapo wanaweza kumudu maisha bila kufanya kazi kwa kutumia akiba zao tu.

Wachache walinieleza uwezo wao ni wa siku mbili tu huku wengi wao wakisema wanategemea wafanye kazi kila siku ndipo wapate chakula.

Licha ya kelele nyingi za muda mrefu zinazoshinikiza kwamba wakazi wa jiji la Dar es Salaam wafungiwe majumbani kama hatua ya kuepusha maambukizi ya virusi vya corona, Magufuli amekuja na maamuzi ambayo kwangu nimeyaita kama kuruka mtego wa pili ambao wapinzani wake wangetamani auingie na iwe ngumi yao ya kumpigia hapo baadaye (Soma mtego wa 1 aliouvuka Magufuli Hata mimi ningefanya kama Rais Magufuli - JamiiForums )

Ni kweli tunajua kwa sasa DSM ndiyo inaongoza kuwa na wagonjwa wengi wa corona kuliko mikoa mingine kwasababu ya kuwa na mji wa kibiashara wenye idadi kubwa ya wakazi na watu wanaoingia na kutoka.

Nasema Rais Magufuli amevuka mtego huu wa kuifungia Dar kwasababu asilimia kubwa ya Watanzania hawana uwezo kumudu maisha ya bila kufanya kazi zaidi ya siku 5. kuanzia siku 5 na wengine hujua watakula nini baada ya kwenda kutafuta asubuhi.

Endapo Rais angeruhusu _'lockdown'_, maana yake shughuli za kiuchumi na uzalishaji zisingefanyika ndani ya Dar es salaam na hata nje ya DSM kungekua kugumu.

Fikiria wewe ndiyo Rais halafu unawafungia watu milioni sita asilimia ambapo asilimia 80 hawana uwezo wa kuishi zaidi ya siku 5, ungeongozaje?

Hivyo uamuzi wa kulifungia jiji hilo la kibiashara ungepelekea vifo vitokanavyo na njaa, ongezeko la uhalifu, na hata maandamano mithili ya yale yanayoshudiwa huko Marekani.

Hivyo badala ya kuwaponya watu na Corona, tungewaua watu kwa njaa, na matukio ya uhalifu. Kwa uamuzi huu wa Rais Magufuli, kwangu ameruka mtego mwingine nampongeza sana.

*Insta : FB ; Twit : Sangu Joseph*

*#KijanaMzalendo* *#IloveTZ*

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lockdown si nzuri hata kidogo hii Ni kutokana na uchumi wa nchi,kikubwa Ni kupunguza misongamano mfano vituo vya mabasi Ni vyema wale wapiga debe waloweshwe virungu vya kutosha asibaki kenge stendi ambae hasafiri wawepo wasafiri na ofisi za mawakala tuuuh wakata tiketi tena kwa kipimo cha kampuni wakala moja na tiketi nyingine zikatwe mtandaoni

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
Hao wapiga debe waende wapi nawakati wao wanategemea hapohapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mhubiri 10:11

Nyoka akiuma asijatumbuizwa, Basi hakuna faida ya mtumbuizi.
 
Back
Top Bottom