usisahau kuwa lazima ukubaliane na hali halisi ya Tanzania na viongozi wake ,usijifanye kuwa hujui kuwa sio wabunge wote twanaoishi kwenye majimbo yao, sasa iweje ushangae dada Regina kurudi kutoka kilombero?mbona hushangai viongozi wengine tena wa ngazi za juu ambao hata dodoma kwenyewe hawataki kwenda(kuhamisha serikali)? sasa akikaa huko kilombero una uhakika kuwa antapata kazi ya kumuingizia kipato?aua wewe unafikiri mpiganaji yeye hataji mshiko wa kujikimu?
This is no defense at all, basically ni kama mtu kashikwa anafanya kitu kibaya, halafu anajitetea kwa kusema "mbona na wengine wanafanya". If anything it is admission of wrongdoing.
Washtakiwa wa genocide ya Rwanda wakitoa utetezi wa kusema mimi niliua lakini nchi nzima iliua, hii defense itakuwa haina mantiki. Majaji watasema wewe ndiye tunakutaka tuwaonyeshe mfano wengine wote. Regia Mtema ni mgombea aliyepita wa upinzani, na mimi nawasema hawa wapinzani kwa sababu wao ndio walikuja under the banner of good governance na kuleta mabadiliko.CCM tunawajua, kuna wengine wetu wanafikiri CCM is beyond repair, ndiyo maana unaweza hata usinisikie kuongelea sana kuhusu CCM, lakini tukiwa tunaona uozo ule ule wa CCM kutoka kwa hawa wapinzani wanaosema wanataka kuleta mabadiliko tunapata mshtuko.
Unapouliza "sasa akikaa huko Kilombero una hakika kuwa atapata kazi ya kumuingizia kipato" unaonyesha kutoelewa kuwa tunachopigania katika mabadiliko ya uongozi ya taifa letu ni kikubwa kuliko kipato cha mtu mmoja. Na kama Regia Mtema naye ana mtazamo kama wako, then hii ina confirm suspicions za cynics kwamba hawa wanasiasa wanajiingiza katika siasa kwa maslahi binafsi tu.
Hivi Nyerere angeamua kujali kipato zaidi ya kujenga TANU wakati anafanya uamuzi wa kutaka kujiuzulu ualimu ili aweze kupata muda zaidi wa kufanya kazi za vyama na asiviolate code of conduct ya ajira yake ya ualimu, leo angekuwa na historia hii aliyoacha?
Hivi Barack Obama alivyo graduate from an Ivy League school, angeamua kukubali zile lucrative offers za kazi Wall St. ambazo zingemlipa mara nyingi tu kuliko mapato yake kama community organizer leo angekuwa na historia aliyonayo ?
Hivi Nelson Mandela angesema aangalie personal gains kutoka law career na asirisk kufungwa na kupoteza kipato historia leo ingekuwaje ? Angeweza ku achieve yote aliyoweza ?
Political achievements zinataka personal sacrifice, to whom much is given, much is required. Ukitaka wananchi wakuamini na kukupa dhamana ya uongozi, inabidi uwaonyeshe kwamba unafanya sacrifice zinazotakiwa kwa wao kukuamini hivyo. Nyerere, Mandela na Obama wote walishafanya sacrifices kubwa kabla hata ya kuwaomba wananchi kura, ndiyo maana walishinda bila matatizo.
Regia Mtema anafanya sacrifice gani? Au anataka dhamana ya uongozi tu, lakini hata sacrifice ya kuachia ofisi za viyoyozi za mijini hataki ?