Nimerudi salama-Niliwamiss sana

Status
Not open for further replies.

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,971
0
Wapwaz na Binamuz wote.

Ni matumaini yangu kuwa wote mko salama.Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza wale wote kwa namna moja ama nyingine mmeshiriki kufanikisha uchaguzi wa mwaka hu popote pale mlipo kwa ngazi yoyote ile iwe udiwani,ubunge na hata urais,pongezi sana!!!.

Napenda kuwaambia kuwa nimerudi salama toka Kilombero,nimepambana kadiri ya uwezo wangu na kufika hapa nilipofika.namshukuru MUNGU niko salama kabisa na nitaendelea kuvinjari kwenye jukwaa letu pendwa la urafiki na mapenzi.

Nimewamiss si kidogo!!!Natafuta muda nionane na baadhi yenu.

With love
Regia
 
Baija Bolobi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
1,096
2,000
Dear Regia
Karibu sana na pole sana kwa masahibu yote.
I will be the last one to dispute your committment to our nation.
Looking foward to meeting you personally

Baija
 
Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,275
1,195
Dear Regia

Karibu sana pole san na mapambano
hope bado unaendeleza mapambano ya kukata rufaa??
 
Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,698
1,250
Wapwaz na Binamuz wote.

Ni matumaini yangu kuwa wote mko salama.Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza wale wote kwa namna moja ama nyingine mmeshiriki kufanikisha uchaguzi wa mwaka hu popote pale mlipo kwa ngazi yoyote ile iwe udiwani,ubunge na hata urais,pongezi sana!!!.

Napenda kuwaambia kuwa nimerudi salama toka Kilombero,nimepambana kadiri ya uwezo wangu na kufika hapa nilipofika.namshukuru MUNGU niko salama kabisa na nitaendelea kuvinjari kwenye jukwaa letu pendwa la urafiki na mapenzi.

Nimewamiss si kidogo!!!Natafuta muda nionane na baadhi yenu.

With love
Regia

Regia Salaam sana;

Hongera sana na harakati zote na karibu tena jamvini.

Baadhi yetu tulijaribu kukupigia kukutia moyo na kukupongeza lakini najua ulikuwa na mambo mengi.

Kwa kuwa sasa umerudi, wengi tunapenda kujua kwa hakika ni nini kilitokea jimboni kwako. Mengi sana yamesemwa lakini nina uhakika ukweli wote unao. Please tuhabarishe na pia tunapenda kujua ni nini kitafuata au hatua gani unatarajia kuchukua.

Wasalaam

SM
 
Meale

Member
Nov 24, 2009
91
0
Karibu sana dada Regia, na hongera kwa mapambano uliyoyafanya. Naamini umeonyesha unaweza ila kura hazikutosha, kwa hiyo bila shaka utajipanga upya na vizuri zaidi kwa mapambano yajayo. Keep it up.
 
Mahesabu

JF-Expert Member
Jan 27, 2008
5,374
2,000
pole na hongera kwa kuthubutu....!
tunapingana kwa hoja na tunakuwa pamoja pia kwa hoja......my ushauri....pamoja na yote yaliyotokea its better uka-appeal, then uangalia ni wapi uliteleza....iwe kwa ujuzi wako au kwa wewe kutokujua......ita wataalamu wanaoweza kukuambia ukweli(SIO KUTOA UNAFIKI WAO KWAKO) then within no time K4C will be yours....! remember dada regy...am speaking from UZALENDO point of view and not otherwise...! TAKE FIVE...!
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
55,512
2,000
Hii concept nzima ya "kurudi" kutoka Kilombero mimi napata tabu nayo sana. Inaonekana Kilombero -pamoja na majimbo mengine ya vijijini- ni sehemu za kwenda wakati wa uchaguzi tu, uchaguzi ukiisha watu wanarudi kwenye shughuli zao za kawaida mijini.

Badala ya wagombea walioshindwa mwaka huu kubaki huko vijijini kuimarisha vyama vya upinzani, kuisadidia jamii pamoja na kupanga mikakati ya kushinda hivi viti katika uchaguzi ujao, tunaona increasingly "wanarudi" mijini.

Wapinzani wakiendelea kushindwa katika kila chaguzi zijazo watashangaa kweli kwa mwendo huu wa kwenda majimboni nyakati za chaguzi tu, na chaguzi zikiisha wanarudi mijini kwenye mitandao na urahisi wa maisha ?

Tunawatendea haki wananchi kweli kwa mwenendo huu ?
 
Lady N

JF-Expert Member
Nov 1, 2009
1,916
1,250
I admire you.
I miss u too.
welcome back:hug::kiss::welcome:
 
kwa hiyo asifanye kazi akakae kilombero? chama kitamtengea fungu kweli? am just asking
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
55,512
2,000
kwa hiyo asifanye kazi akakae kilombero? chama kitamtengea fungu kweli? am just asking

Kilombero watu hawafanyi kazi? Yaani wewe ushaona kukaa Kilombero na kufanya kazi haviwezi kwenda pamoja.

Au definition yako ya kufanya kazi ni lazima kazi iwe mjini kwenye ofisi moja kubwa yenye kiyoyozi?

Bila ya kukaa na hawa wananchi wagombea hawawezi kuyajua matatizo yao vizuri na kuwasaidia ipasavyo, pamoja na kujinetwork vizuri kwa uchaguzi ujao. Mwisho wa uchaguzi mmoja ndio mwanzo wa uchaguzi unaofuata, CHADEMA waanze kampeni za kuchukua jimbo hili sasa, na moja ya kitu wanachotakiwa kufanya ni kuamua nani watamsimamisha, na mtu huyu itabidi aishi Kilombero na kufanya kazi na wananchi wa Kilombero, sio kuwaletea mbunge mtalii anayekuja nyakati za uchaguzi na uchaguzi ukiisha wiki moja tu anarudi mjini.
 
Pakawa

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
6,475
2,000
Mkuu Kiranga sasa ni hivi uchaguzi umeisha maisha lazima yaendelee. Sasa Regia aendelee kukaa Kilombero kama ni maswala ya kutafuta mawakili na mengineyo si inabidi arudi mjini wajameni!! Nadhani ni wakati muafaka wa kumpongeza kwa alivyojitoa kupigania haki ya wengi walio maskini. Dada Regia karibu tena hongera sana kwa kazi uliyoifanya maisha yaendelee.
 
Regia hajasema kaja kutafuta mawakili, kasema karudi kutoka Kilombero. Unafahamu maana ya "kurudi" ? Mtu anarudi kwenye base yake, mtu anarudi nyumbani kwake. Inaonekana Regia anaona Kilombero si base wala makazi yake, ndiyo maana "anarudi kutoka Kilombero". Ama sivyo angetuambia "nimekuja mjini" kama kweli angekuwa amefanya Kilombero base yake.

Hili ni tatizo kubwa tunalo, wabunge wetu na wadau wengine wanaotaka kuwakilisha wananchi wanataka kulundikana mijini, watakuwa vipi karibu na wananchi wanaotaka kuwaomba kura? Hawa kweli wanataka kuwakilisha matakwa ya wananchi au wanataka ukubwa tu ?
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
55,512
2,000
Kiranga mwenyewe yupo mjini na anajaribu tu kuleta concept zake hapa

Tofauti kati ya Kiranga na Regia Mtema ni kwamba, Kiranga hajawahi kugombea nafasi ya kutaka kuwawakilisha wananchi wa Kilombero, kwa hiyo hana haja wala wajibu wa kuwa karibu na watu wa Kilombero.

Lakini Regia Mtema ndiyo kwanza anatoka kugombea ubunge na ameonyesha kuwa mdau mkubwa wa watu wa Kilombero.

Wanaotaka dhamana kubwa kutoka kwa wananchi inabidi watuonyeshe kwamba wanafanya kazi kubwa na wananchi hawa, vile vile wasiotaka dhamana hata ndogo kutoka kwa wananchi hawa, watu kama kina Kiranga ambao hawana ndoto ya kugombea public office, hawana wajibu wa kuwa karibu na wananchi hawa. Wakifanya hivyo kwa matakwa yao ni sawa, lakini pia wana haki na uhalali wote wa kuingia katika spaceship na kwenda Andromeda Galaxy for all that we care.

You can't eat your cake and have it still. Huwezi kujinadi kama mdau mkubwa wa watu wa Kilombero, halafu uchaguzi ukiisha wiki moja tu unajitoa Kilombero na "kurudi" mjini kwenye uafadhali wa maisha. Kama unaishi kwenye uafadhali huu wa maisha utapata wapi uchungu wa kudai uafadhali huu wa maisha wa mjini ufike vijijini?

Ndiyo maana vijijini hakuendelei, wabunge wote na wapinzani wao wako mijini, wanaenda vijijini nyakati za chaguzi tu.
 
Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
52,055
2,000
Tofauti kati ya Kiranga na Regia Mtema ni kwamba, Kiranga hajawahi kugombea nafasi ya kutaka kuwawakilisha wananchi wa Kilombero, kwa hiyo hana haja wala wajibu wa kuwa karibu na watu wa Kilombero.

Lakini Regia Mtema ndiyo kwanza anatoka kugombea ubunge na ameonyesha kuwa mdau mkubwa wa watu wa Kilombero.

Wanaotaka dhamana kubwa kutoka kwa wananchi inabidi watuonyeshe kwamba wanafanya kazi kubwa na wananchi hawa, vile vile wasiotaka dhamana hata ndogo kutoka kwa wananchi hawa, watu kama kina Kiranga ambao hawana ndoto ya kugombea public office, hawana wajibu wa kuwa karibu na wananchi hawa. Wakifanya hivyo kwa matakwa yao ni sawa, lakini pia wana haki na uhalali wote wa kuingia katika spaceship na kwenda Andromeda Galaxy for all that we care.

usisahau kuwa lazima ukubaliane na hali halisi ya Tanzania na viongozi wake ,usijifanye kuwa hujui kuwa sio wabunge wote twanaoishi kwenye majimbo yao, sasa iweje ushangae dada Regina kurudi kutoka kilombero?mbona hushangai viongozi wengine tena wa ngazi za juu ambao hata dodoma kwenyewe hawataki kwenda(kuhamisha serikali)? sasa akikaa huko kilombero una uhakika kuwa antapata kazi ya kumuingizia kipato?aua wewe unafikiri mpiganaji yeye hataji mshiko wa kujikimu?
 
This is no defense at all, basically ni kama mtu kashikwa anafanya kitu kibaya, halafu anajitetea kwa kusema "mbona na wengine wanafanya". If anything it is admission of wrongdoing.

Washtakiwa wa genocide ya Rwanda wakitoa utetezi wa kusema mimi niliua lakini nchi nzima iliua, hii defense itakuwa haina mantiki. Majaji watasema wewe ndiye tunakutaka tuwaonyeshe mfano wengine wote. Regia Mtema ni mgombea aliyepita wa upinzani, na mimi nawasema hawa wapinzani kwa sababu wao ndio walikuja under the banner of good governance na kuleta mabadiliko.CCM tunawajua, kuna wengine wetu wanafikiri CCM is beyond repair, ndiyo maana unaweza hata usinisikie kuongelea sana kuhusu CCM, lakini tukiwa tunaona uozo ule ule wa CCM kutoka kwa hawa wapinzani wanaosema wanataka kuleta mabadiliko tunapata mshtuko.

Unapouliza "sasa akikaa huko Kilombero una hakika kuwa atapata kazi ya kumuingizia kipato" unaonyesha kutoelewa kuwa tunachopigania katika mabadiliko ya uongozi ya taifa letu ni kikubwa kuliko kipato cha mtu mmoja. Na kama Regia Mtema naye ana mtazamo kama wako, then hii ina confirm suspicions za cynics kwamba hawa wanasiasa wanajiingiza katika siasa kwa maslahi binafsi tu.

Hivi Nyerere angeamua kujali kipato zaidi ya kujenga TANU wakati anafanya uamuzi wa kutaka kujiuzulu ualimu ili aweze kupata muda zaidi wa kufanya kazi za vyama na asiviolate code of conduct ya ajira yake ya ualimu, leo angekuwa na historia hii aliyoacha?

Hivi Barack Obama alivyo graduate from an Ivy League school, angeamua kukubali zile lucrative offers za kazi Wall St. ambazo zingemlipa mara nyingi tu kuliko mapato yake kama community organizer leo angekuwa na historia aliyonayo ?

Hivi Nelson Mandela angesema aangalie personal gains kutoka law career na asirisk kufungwa na kupoteza kipato historia leo ingekuwaje ? Angeweza ku achieve yote aliyoweza ?

Political achievements zinataka personal sacrifice, to whom much is given, much is required. Ukitaka wananchi wakuamini na kukupa dhamana ya uongozi, inabidi uwaonyeshe kwamba unafanya sacrifice zinazotakiwa kwa wao kukuamini hivyo. Nyerere, Mandela na Obama wote walishafanya sacrifices kubwa kabla hata ya kuwaomba wananchi kura, ndiyo maana walishinda bila matatizo.

Regia Mtema anafanya sacrifice gani? Au anataka dhamana ya uongozi tu, lakini hata sacrifice ya kuachia ofisi za viyoyozi za mijini hataki ?
 
Pakawa

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
6,475
2,000
Mkuu Kiranga taratibu mkuu nilikuwa natoa mfano si kwamba nilikuwa na hakiki hoja samahani kama nimekukwaza. Inawezekana kuna mambo mengi tu yamemfanya arudi mjini lakini kwa ufupi maisha lazima yaendelee.
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom