NIMEREJEA TENA JF..

mkumbwa junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2014
Posts
853
Reaction score
1,702
kwa mara nyingi nimerejea JF baada ya kupata changamoto mwaka 2015 iliyofanya nishindwe kuendelea kuwa active JF..
Nashukuru Mola leo baada ya miaka mitatu nimerejea nikiwa na Nguvu za kutosha...

Wakongwe naombeni mnijuze kama bado kuna uhuru wa kutoa mawazo kama zamani zile au mambo yamebadilika??
ASANTENI[emoji120] [emoji120]
 
Hakuna io kitu tulishazika zamani
 
Gentamycine ameshapotezwa humu
Kuchangia nyuzi za habari za TISS ni hatari
 
Karibu mkuu ila uwe makini kuliko ulivyokuwa zamani saizi ni balaa zaidi na nahisi hata kina Max wamelainika kuhusu kutoa taarifa za watu humu
 
Gari ni hili hili jf sema traffic wamekuwa wengi njiani kama ulizoea zamani kutembea utakavyo saizi kuna tochi mkuu wanajificha popote pale kwa hiyo ukiwa barabarani kuwa makini usipigwe tochi mkuu.
 
Hebu jaribu mkuu kushusha nondoz nzito

Ova
Ndo maana nimeomba mwongozo nisije shusha vitu nikajikuta mikononi mwa Watu wasiojulikana...

Miaka ile ya 2013-2015 nilipopata dharura tulikuwa tunajiachia kwa kadiri ya uwezo na akili zako...
Nataka nijue hizi zama vipi
 
Ndo maana nimeomba mwongozo nisije shusha vitu nikajikuta mikononi mwa Watu wasiojulikana...

Miaka ile ya 2013-2015 nilipopata dharura tulikuwa tunajiachia kwa kadiri ya uwezo na akili zako...
Nataka nijue hizi zama vipi
Hivi ulikuwa unajua kuwa jf yenyewe walikuwa korokoroni

Ova
 
Changia kwa kumumunya maneno bila kupanua mdomo.
Ukifunguka baba, utakutana na mnyausho (ban) wa bila maelezo wala muda wa kukaa segerea.
Wakikuheshimu sana utakutana na ufuto wenye kulamba mainbody pekee na kukubakishia kichwa tu (heading)
Jichekeshechekeshe kwa kujipendekeza na usishike kwa papara, shika kwa kupapasa na usibonyeze sana usije kuharibu na kunyang'anywa ulichonacho mkononi mwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…