Nimepishana na NIDA

Nimepishana na NIDA

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,374
Reaction score
38,248
Za asubuhi wanaJAMII!

Nina changamoto Mkuu wenu, nimepishana na zoezi zima la uandikishaji kwa ajili ya Nationl IDs, mimi na kaya yangu nzima.
Wakati zoezi la uandikishaji linaanza DSM, mimi na kaya yangu hatukuwepo DSM, nilikuwa kikazi mkoani, nikabeba na kaya yangu yote nikaondoka nayo mkoani! Zoezi likaisha DSM.

Kule mkoani nilikokuwa, nikavunja ndoa na mwajiri wangu, nikapata mwajiri mpya DSM, nimerudi na kaya yangu yote, nimekuta watu wa DSM ndio kwanza wanapewa IDs zao!

Msaada, naanzaje taratibu za uandikishaji, kwa mimi na wanakaya wangu wote!

Nawatakia asubuhi njema
 
...fika ofisi ya serikali ya mtaa wako ukiwa na vielelezo vya utambulisho wako na wanafamilia na ndugu unaoishinao, "serikali watakueleza sehemu ya kuanzia"
 
miss chagga unamaanisha watarudia tena DSM, na baadae kila mkoa?

Lazima warudie tena kwa sababu mwaka huu kuna watu wamefika kumi na nane tena ..kuna wafonjwa wamepona kuna waliokuwa nje ya nchi wamerudi so lazima iwe hivyo iwe sustainable
 
Last edited by a moderator:
yaani hata mimi nina situation kama yako...ngoja nijimuvuzishe kwa serikali ya mtaa ili nipiwe muongozo
 
usihofu havina dili hivi vitambulisho , passport ndio mpango mzimaaa
 
Kuna vituo baadhi vimekwekwa kwa ajili ya watu kama nyinyi ukifika kwa mwenyekiti wako wa mtaa atakujulisha kilipo na utapata huduma
 
na mimi ni mmoja wapo, ila nimeelekezwa pale kimara wanaendelea na ili zoezi muda wote, pia lazima warudie kupita, ila du wanatujazia ID mpaka basi, bado vya NEC.
 
Nenda ofisi zao za mjini karibu na makao makuu ya magereza wanaandikisha pale daily watu ambao hawakujiandikisha mwanzo na wale ambao hawakupiga picha huduma hizo zipo pale.
 
Back
Top Bottom