Nimependwa,Nimependa na mtu simjui

Nimependwa,Nimependa na mtu simjui

Joined
May 29, 2013
Posts
25
Reaction score
8
Habar zenu wana jamiiForum nilikuwa naomba mnipe ushaur kuhusu hili-:Kuna siku wakat napiga simu nikakosea namba moja tu akapokea msichana kama mnavyojua vijana kupokea nikamwambia kuwa nakupenda akakataa kabisa baada ya kupita siku 2 akanipigia simu ndipo aliponimbia amekakubali nikamuuliza unaishi wapi akaniambia anaishi arusha me nikamwambia nipo dar nikamuuliza una mpenzi?akajibu alishakuwa nae ila ana miaka 3 mpaka sasa hajawahi kumwona na akipiga simu yake haipatikani nikaendelea tena kumuuliza unaishi na nani akajibu naishi na wazazi wangu,kaka na mdogo wangu wa kiume ila mara kwa mara wazazi wangu huwa wanasafiri wanaenda nchi za nje zikapita wiki mbili cha kunishangaza zaidi alianza kunitumia pesa mara kwa mara.Siku akaniuliza unakuja lini nikamjibu sina nauli nikipata nauli nitakuja tukaendelea na mazungumzo ya kawaida siku zikaendelea kupita siku moja asubuh akapiga simu akaniambia nakutumia nauli nataka uje kweli akanitumia nauli ananitaka niende ila sasa hapo ndo pananikwaza mimi jamani nipeni ushauri.
 
Watchout!! Yashankuta mwenzie cku ya kuona nae ikawa tofav nalvyotegemea.
 
yeah jamaa kaongea kweli we waweza zania bonge la toto halafu ukakuta tofaut na umfiliavyo utakuwa huna raha tena
 
Ushaolewa wewe jini mahaba hiloooooooo..........................
 
jini mahaba hilo, litakujengea hadi nyumba ila hautakuja kuoa maisha yako yote, litakuwa linaua wapenzi wako na watoto wako. lina wivu kama nini. yamekukuta mtoto wa mwenzetu sijui utafanya nini.
 
wala sio jini mahaba ni jimama lililoopoa kiserengeti!
 
Anataka mpaka me niende ndo aje yeye

Skia! Hiyo safari unayoitaka lolote (baya or zuri) laweza tokea huko!
.....
Umakini ndio ngao yako!
Usisahau aliwazalo Mji.nga ndilo litalomtokea!!!!
....
TAFAKARI! CHUKUA HATUA!
 
Acha kwenda, kwa nini usiamue kupenda mtu unaemfaham au kumjua walao kwa picha yake?...

Gharama yake yaweza kuwa kubwa, mbaya na hatari..
 
ha ha haaa, dah huo mtihani, dunia imeharibika hii, ukila vyawatu lazima ulipie!!
 
mwambie umekosea kupokea nauli hutaenda tena mmalize uhusiano kwa kukoseana kwani mlianza kwa kukosea number malizeni na kukosea pia chaooooooooooooooooooooooooo
 
we nenda...ukishuka tu kweny bus...piga simu afu angalia nani atapokea...ukiona magumashi sepa fasta...unalala zako lodge unachapa mwendo kesho yake...au nauli ya kurudia pia huna?
 
Back
Top Bottom