The Donchop
JF-Expert Member
- Jan 10, 2014
- 294
- 381
Mimi ni mwanamke mwenye miaka 27. Nilianza kujiingiza kwenye maswala ya kimapenzi kwa mara ya kwanza nikiwa na miaka 23. Nilitokea kuwa na kijana mmoja ambaye hatukudumu kwani sikuwa na hisia zozote juu yake na wala alipoondoka sikuumia.
Nilikaa miaka miwili ndipo nikaja kukutana na kijana huyu ambaye leo ameniumiza.
Kipondi nakutana nae mwaka 2014, hakuwa na maisha ya kujivunia. Hakuwa na kazi wala pesa. Hata mimi nilikuwa hivyo lakini nilikuwa na kihaueni. Mara kadhaa nilimsupport kupata nauli ya kwenda chuo na hata kumuandalia chakula nyumbani kwetu kisha ukipitia na kwenda nacho kwao.
Maisha yetu hayakuwa maisha mazuri ila tulikuwa na furaha. Ilitokea hata kuna kipindi tunashinda nje ya nyumba yetu kuanzia jioni hadi alfajiri.
Mwenzangu akapata kazi baada ya mwaka mmoja. Kuanzia hapo kukawa na mabadiliko. Akawa akinipigia simu asubuhi na jioni. Kuonana ni mara moja. Nikaelewa kuwa ni sababu za kikazi.
Baada ya kupita miezi sita, mwenzangu akahamia kwake. Hapo nikawa kwenye mtihani. Hata nikipiga simu kupokea ni shida. Nikituma msg inaweza isijibiwe hata zipite siku mbili. Nikaishi nae ivo ivo.
Jumamosi ya tarehe kumi alinipigia simu asubuhi akaniambia kuwa hanitaki tena sababu amekutana na mtu wake waliyependana nae zamani.
Sikuamini wana jamii, nikampigia simu usiku, akapokea yule mwanamke na kuongea vibaya sana na mimi.
Najisikia vibaya sana wana jamii. Naombeni ushauri utakaonifanya nisonge mbele.