Nimepata kidonda kwenye kichwa cha uume

Panzi Mbishi

JF-Expert Member
Mar 8, 2021
2,053
2,669
Wadau habari, Ni matumaini yangu hamjambo. Nimejileta kwenu ili nipate utatuzi wa changamoto ya kiafya inayonikabili. Ni karibu wiki sasa nasumbuliwa na aina fulani ya kidonda juu ya uume.

Kwanza nilianza kuhisi maumivu kidogo suruali inapogusana na kichwa cha uume nikadhani nimepata michubuko ya kawaida sikujichunguza.

Baada ya siku kama tatu ndio nikahisi hali si kawaida nilipotazama nikaona kimeenea karibu robo ya eneo la juu ya kichwa cha uume.

Naomba kufahamishwa tatizo linatokana na nini na ikiwa kuna tiba zake nitashukuru wakuu.

Natanguliza shukrani!
 
Hapo nyuma nimeshinda sana hospitali kwa shida mbali mbali mpaka nimechoka, Mara niambiwe Pneumonia, Mara Amoeba wakati namaliza dozi ya mwisho ndio kidonda kinatokea sasa nimechoka kunywa dawa bila kujua natibu nini
Basi kaa nyumbani kusubiri miujiza
 
majibu ya vipimo yalikuwaje?
Hospitali ya kwanza nilipima damu tu wakasema haina shida wakahisi ni pneumonia wakanipa dawa maana nilikuwa nasumbuliwa na homa, Hospitali ya pili walipima damu tu pia wakanipa dawa bila kusema tatizo, Hospitali ya tatu wakapima damu, mkojo na haja kubwa, Damu na mkojo vikaonekana salama sasa sijui waliona nini kwenye haja kubwa wakasema huenda ni amoeba nikapewa dawa, Namaliza dozi tu ndio naona kidonda
 
Back
Top Bottom