PostGE2025 Nimeona ni vyema nikatolea ufafafanuzi wa kina kuhusiana na nyuzi zangu zilizopelekea kupokea jumbe nyingi za huzuni na lawama

PostGE2025 Nimeona ni vyema nikatolea ufafafanuzi wa kina kuhusiana na nyuzi zangu zilizopelekea kupokea jumbe nyingi za huzuni na lawama

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Pakome

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2024
Posts
1,541
Reaction score
916
Hivi karibuni niliandika nyuzi zilizojikita zaidi kwenye nidhamu na ukosoaji wa matendo mabaya, nyuzi zilizopelekea kupokea jumbe nyingi za huzuni na lawama ambazo zilinihuzunisha sana

Nimeona ni vyema nitolee maelezo ya kina kuhusiana na nyuzi zile kwasababu inawezekana baadhi ya wasomaji waliguswa kwa namna mbaya pasipokujua dhamira yake ilikuwa ipi

Nianze na nyuzi zinazohusiana na Serikali:

1:
Watanzania na Serikali tulinde sana nchi yetu kwasababu vita ya Wakoloni bado ipo, wanatumia mbinu mpya ya Mapandikizi kuharibu Uhuru wetu
Maelezo: Ni sahihi kulinda nchi dhidi ya maaduni. Kila nchi duniani inawezakuwa na baadhi ya rasilimali ambazo nchi nyingine hazina. Linapotokea swala kama hili basi litapelekea nchi zisizokuwa na rasilimali hizo kujawa na wivu mkubwa na kujaribu kuzipata. Kwanini inawezakuwa tatizo kubwa? Hii ni kwasababu nchi zenye rasilimali za kipekee zinaweza kuwa na Sheria kali za kulinda rasilimali hizo, sheria zinazozuia wageni kuzipata, na mwisho wageni hao wakatumia njia haramu kuzipata.

Binafsi siwezi kuamini kuwa wageni hawatamani rasilimani za Tanzania kwasababu historia inaonesha matendo hayo yalikwishakufanyika enzi za Ukoloni. History of Tanzania - Wikipedia

Nilipoandika uzi huu nilikuwa nimesoma historia ya Wakoloni barani Afrika na kuona matendo yao ambayo yamethibitishwa kihistoria na wala haikuwa propaganda ya kusifia Serikali kama baadhi ya wasomaji walivyonishutumu



2: PostGE2025 - Ufafanuzi wa Vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025
Maelezo: Uzi huu ulikuwa na lengo la kuonesha namna gani hasira inawezakupelekea kuchukua maamuzi mabaya ambayo mwisho wake ni majuto. Matatizo yaliyotukumba yalitokana na hasira kubwa tuliyokuwa nayo, na endapo kama nchi tutakiri basi nchi itapona. Hasira ni hasara, hata katika familia zetu tunashuhudia namna watoto wanaathirika pale wazazi wanapotumia hasira, tuna watoto waliovunjwa viungo vya miili yao mfano miguu, mikono, meno, kuathirika kisaikolojia na wengine kupoteza maisha kwasababu ya adhabu za Wazazi au Walezi wao. Lengo la uzi huu lilijikita zaidi kwenye hasira, chanzo na madhara yake bali lengo halikuwa kuitetea Serikali kama baadhi ya wasomaji walivyonituhumu



3: PostGE2025 - Tuhuma za Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Gwajima kwa Jeshi la Polisi zinaweza kupelekea kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu
Maelezo: Uzi huu ulilenga zaidi swala la kimaadili na Kisheria. Maadili yanagusa dunia nzima si tu kwa nchi moja au eneo moja. Kimaadili si sahihi kudhalilisha Jeshi la Polisi kutokana na majukumu yake. Matatizo ya Jeshi la Polisi yanatatuliwa Kisheria na si kwa kashfa mbaya. Matatizo yote yanayoihusu nchi yeyote duniani hasa usalama wa raia na mali zao yanatatuliwa na Idara ya usalama

Kwa maelezo ya Kanisa kwanza kabisa inaitwa kashfa kwasababu zifuatazo

Kanisa halikuwa na Ushahidi wa moja kwa moja bali lilituhumu. Je, ikiwa utatuhumu kuwa Jeshi la Polisi ndilo liliharibu mali za Kanisa na baada ya uchunguzi kufanyika ukabaini wahalifu wengine utajitetea vipi? Lakini utafuta vipi kashfa hiyo?

Mali zinapoibiwa zikiwa katika uangalizi wa Jeshi la Polisi haimaanisha ndilo lililoiba bali aliyeiba ni mwizi ambaye anatakiwa kubainika baada ya uchunguzi na sio kabla ya Uchunguzi. Kwahiyobasi Kanisa lilipaswa kufika katika Kituo Cha Polisi kupeleka malalamiko ili yafanyiwe uchunguzi na sio kupeleka malalamiko katika mitandao ya kijamii ambayo hayana ushahidi wa moja kwa moja

Kwahiyo kwa uzi huu sio kweli kwamba ulikuwa na lengo la kukumbatia Jeshi la Polisi kama baadhi ya wasomaji walivyokosoa. Bali ni swala la Kimaadili na Kisheria na hii ni duniani kote si katika nchi moja. Lakini vilevile Kanisa linapaswa kukiri kwamba lilikosea kwasababu njia ile haiko sahihi Kimaadili wala Kisheria ( Sheria inataka ushahidi na sio kashfa ) ( Sheria inataka malalamiko yapelekwe kwenye kitengo cha Idara ya Usalama na sio katika mitandao ya kijamii )



4: PostGE2025 - Si sahihi Bunge la Ulaya kusitisha misaada nchi ya Tanzania, mapendekezo hayo yanafaa kupingwa kwa nguvu zote
Maelezo: Uzi huu unaohusiana na Bunge la Ulaya nimekosoa kwasababu lengo la Bunge la Ulaya nikutaka kudhoofisha nchi ya Tanzania na hasa katika Sekta ya Uchumi kwa mgongo wa kuadhibu Serikali.

Ni nani asiyejua kuwa Ukoloni ulianzia kwao? Ukoloni ulianzia bara la Ulaya ndipo ukaja Afrika.

Ikiwa Waafrika ni Wakoloni basi aliyewafundisha ni wao

Waafrika wangejulia wapi Ukoloni pasipokuingizwa katika biashara ya Utumwa? Naambatanisha ushahidi ufuatao History of colonialism - Wikipedia

Kwa kupitia ushahidi huu nawezakusema kuwa ikiwa wao ndio walifundisha Waafrika Ukoloni basi wanapaswa kuwaeleza madhara yake kwani wao ni shahidi wa madhara yale

Baba wa Taifa Mwl Nyerere pamoja na Nelson Mandela ndio wanaoweza kuwaelezea kuhusu utu wa Wazungu idadi kubwa tunawaona kwa macho lakini Mwl Nyerere ameishi nao nadhani angeweza kuwaelezeeni kwa kina kama angekuwa hai

Lengo langu sio kuchonganisha Waafrika na Wazungu bali lengo langu nikutaka kuonesha kuwa Ukoloni walianza wao lakini siishii hapo nataka wafundishe Waafrika madhara ya Ukoloni kwasababu wao ndo walioanza inawezekana Waafrika hawafahamu madhara yake ndiyo sababu wanafanya lakini watakapofundishwa na kukanywa wanaweza kuacha



5: Changamoto zilizoikumba Tanzania zitatuliwe kwa kutumia Busara na Utamaduni wa Watanzania. Njia ya lawama itateketeza Taifa
Maelezo: Uzi huu ulikuwa na lengo la kuponya Taifa la Tanzania na sio kutetea Serikali kama baadhi ya wasomaji walivyokashifu. Ikiwa tupo kwenye matatizo yaliyosababishwa na hasira basi njia sahihi ni kuondoa hasira na kujiponya kwa majeraha tuliyopata. Kwanini unaonekana kama unatetea? Hi ni kwasababu haukubaliani na matendo ya kutatua matatizo kwa kulipa visasi, matatizo hayatatuliwi kwa bunduki wala kudhoofisha uchumi bali matatizo yanatatuliwa kwa utulivu. Ikiwa tutaendeleza hasira huku tukiwa tumeshaumia basi mwisho wake tutaongeza maumivu mara dufu hapa ndipo ninapoonekana kama sitetei lakini lengo langu nikuepusha madhara mengine

Tofautisha mifano hii
Asha amepewa lita moja ya maji, akamwaga nusu lita
Juma amepewa lita moja ya maji, akamwaga yote

Je, yupi kati ya Asha na Juma atakayekuwa na unafuu au hasara?
Je Taifa liharibike lote kwasababu liliharibika kidogo ama sehemu iliyobakia itunzwe?

Binafsi sikuona sababu yeyote ya kupokea malalamiko katika uzi huu labda tu ilikuwa challenge



6: PostGE2025 - Kijana anayejiita Habili au Khabili atashtakiwa kwa kosa la kuvunja Sheria za ndani na nje ya nchi
Maelezo: Hii inajumuisha wakosoaji wengine wote niliowazungumzia. Lengo la kuandika uzi huu ni kwasababu wakosoaji hawa wanajaribu kudhoofisha na kuchafua Taifa la Tanzania kwa kuwapa wageni siri za nchi ya Tanzania, siri ambazo baadaye zitatumika na wahalifu, magaidi, waasi kama fimbo ya kuchapa nchi ya Tanzania. Hata baba wa Taifa angekuwa hai asingekubaliana nao. Lakini jambo baya zaidi wamevunja Sheria, Katiba na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Utamaduni wa Tanzania, Heshima na Utu wa binadamu pamoja na Sheria za Umoja wa Mataifa kwa kigezo cha kudhoofisha Serikali.

Ikiwa mtawakalia kimya basi leo watatoa siri za Serikali kesho watatumika na magaidi na nchi ya Tanzania itaingia kwenye matatizo makubwa sana ya Kiusalama

Huyu gaidi Habil baadaye ataingiza nchi ya Tanzania kwenye matatizo makubwa sana kwasababu ataharibu mifumo yote ya nchi hasa software za Serikali na za watu binafsi kwasababu atanunuliwa na magaidi kwa lengo la kutekeleza shambulio la kutumia tekinolojia. Uhalifu ni sawa na chakula leo utakula na kesho utakula tena katika maisha yangu sijawahi kuona mtu aliyekula chakula mara moja tu na kuwaeleza watu kwamba ameshiba kwahiyo hatowahi kula tena katika maisha yake yote

Iwe marufuku kwa Magaidi hawa kutamka neno Mungu au maandiko ya vitabu vya dini wanapofanya uhalifu wao kwasababu Mungu hakumbatii Wahalifu, Magaidi na Waasi
 
Baada ya kusoma baadhi ya hoja zako ninachokiona ni unataka wanachokitaka upande wa watetezi wa watawala bila kulaumiwa na wenye hasira kwa watawala sababu ya matukio yaliyotokea huko nyuma. Hiyo ni kazi ngumu mno na mwisho wake unaweza kukataliwa na wote, watetezi wa watawala na wenye hasira.
 
Ifike hatua tusijitetee sanaaa tuwache vijana wafanye wanachotaka... Sindano ikipenya na wakagundua waoumia sio wanasiasa wala wanaharakati bali wetoto, mama, baba, bdugu na jamaa zao akili itawarudi ila itakua too late.

Kwenye hili sio Ridhiwani, Heche, Abduli, Maria, mange, Lissu sio Majaliwa wala Mwigulu watakao umia. Ni sisi tutanunua dagaa wa 500 kwa 50,000 mkate wa Buku kwa 100,000 muda huo. Mitandao itageuka kuonesha jinsi mazombi sisi tunavyoishi.

Tulivyo haribu nchi kwa mikono yetu wenyewe kwa ushawishi wa watu ambao hatuwaoni bali kuwasikia.

Ngoja tukaze vichwa, siku yaja na haiko mbali mabadiliko ni muhimu yanaweza kuwa + au -.
 
Ifike hatua tusijitetee sanaaa tuwache vijana wafanye wanachotaka... Sindano ikipenya na wakagundua waoumia sio wanasiasa wala wanaharakati bali wetoto, mama, baba, bdugu na jamaa zao akili itawarudi ila itakua too late.

Kwenye hili sio Ridhiwani, Heche, Abduli, Maria, mange, Lissu sio Majaliwa wala Mwigulu watakao umia. Ni sisi tutanunua dagaa wa 500 kwa 50,000 mkate wa Buku kwa 100,000 muda huo. Mitandao itageuka kuonesha jinsi mazombi sisi tunavyoishi.

Tulivyo haribu nchi kwa mikono yetu wenyewe kwa ushawishi wa watu ambao hatuwaoni bali kuwasikia.

Ngoja tukaze vichwa, siku yaja na haiko mbali mabadiliko ni muhimu yanaweza kuwa + au -.
Hapa ndipo tatizo lilipo kwa sisi Wanachi kuna ufadhili wa Masomo, maswala ya Afya na mengine mengi sasa sijui kwa upande wa Wasomi hali itakuwaje kwasababu kwa historia ya Mwl Nyerere alifadhiliwa masomo pia, kungekuwa na uhusiano mbaya sidhani kama angepata elimu ile
 
Baada ya kusoma baadhi ya hoja zako ninachokiona ni unataka wanachokitaka upande wa watetezi wa watawala bila kulaumiwa na wenye hasira kwa watawala sababu ya matukio yaliyotokea huko nyuma. Hiyo ni kazi ngumu mno na mwisho wake unaweza kukataliwa na wote, watetezi wa watawala na wenye hasira.
Hasira ndiyo itatumaliza kwasababu kila upande ukishakaza kwakweli sijui itakuwaje sana sana yatatokea maafa
 
Hapa ndipo tatizo lilipo kwa sisi Wanachi kuna ufadhili wa Masomo, maswala ya Afya na mengine mengi sasa sijui kwa upande wa Wasomi hali itakuwaje kwasababu kwa historia ya Mwl Nyerere alifadhiliwa masomo pia, kungekuwa na uhusiano mbaya sidhani kama angepata elimu ile
Wajinga hawalioni hilo acha panyeshe wametaka
 
Hapa ndipo tatizo lilipo kwa sisi Wanachi kuna ufadhili wa Masomo, maswala ya Afya na mengine mengi sasa sijui kwa upande wa Wasomi hali itakuwaje kwasababu kwa historia ya Mwl Nyerere alifadhiliwa masomo pia, kungekuwa na uhusiano mbaya sidhani kama angepata elimu ile
🤮
 
downloadfile-9.png
 
Watu wanauwezo wa kuchambua mada zenye hoja na propaganda. Jambo la msingi kuelewa, vijana wanajua wanachotaka. Mambo yamebadilika sana.
 
Back
Top Bottom