Nimenusurika kifo kwenye ajali ya bodaboda

Nimenusurika kifo kwenye ajali ya bodaboda

Pole sana mkuu kama sio una haraka ya muhimu tena sio muhimu kidogo,au unaenda sehemu ambazo hakuna bara bara kuu zenye magari mengi boda boda achana nazo kabisa,sababu ukiacha boda boda wengi ambao ni viroba at work hata madereva wa magari nao wapo majanga kuovertake wanaangalia magari tu boda boda ni JANGA.
 
Ndugu zangu humu ndani, namshukuru Mungu, siku ya juzi usiku nimenusurika kifo, baada ya kupata ajali ya bodaboda niliyokodisha kugongwa na gari. nilikimbizwa hospitali kuu ya mkoa na kupatiwa huduma ya kwanza, na kesho yake kupiga X-ray na kuonesha kuwa mguu na mkono wangu haujavunjika, japo michubuko nimeipata ya kutosha maeneo ya mkononi na mguuni, ila usoni kidogo sana. nipo mapumziko kwa ajili ya mguu kupungua uvimbe, ila maisha yanaenda. hakika Mungu ni mwema bado ana makusudi na mimi. ila bodaboda nouma waungwana.

pole sana!! Mungu ni mwema!!!!
 
pole sana kama mtu una haraka ya kwenda ni heri ujidamke lakini hawa madereva wa boda boda roho mkononi
 
Ni bora ungekufa tu.

Usiwe na roho ya hivyo kama binadamu.
Kumbuka tumeumbwa na upendo,hizi roho za kikatili ni sisi wenyewe ndio tunazitafuta.!
Jaribu kufikiria ungejisikiaje kama maneno hayo angeambiwa mama ako,baba ako,mtoto ako,au hata wewe mwenyewe.!

Tupendane binaadam.
 
Ndugu zangu humu ndani, namshukuru Mungu, siku ya juzi usiku nimenusurika kifo, baada ya kupata ajali ya bodaboda niliyokodisha kugongwa na gari. nilikimbizwa hospitali kuu ya mkoa na kupatiwa huduma ya kwanza, na kesho yake kupiga X-ray na kuonesha kuwa mguu na mkono wangu haujavunjika, japo michubuko nimeipata ya kutosha maeneo ya mkononi na mguuni, ila usoni kidogo sana. nipo mapumziko kwa ajili ya mguu kupungua uvimbe, ila maisha yanaenda. hakika Mungu ni mwema bado ana makusudi na mimi. ila bodaboda nouma waungwana.

...mzinga ulikuwaje...? Pole..!
 
Back
Top Bottom