Nimenusurika kifo kwenye ajali ya bodaboda

Nimenusurika kifo kwenye ajali ya bodaboda

Kijana leo

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
2,860
Reaction score
812
Ndugu zangu humu ndani, namshukuru Mungu, siku ya juzi usiku nimenusurika kifo, baada ya kupata ajali ya bodaboda niliyokodisha kugongwa na gari.

Nilikimbizwa hospitali kuu ya mkoa na kupatiwa huduma ya kwanza, na kesho yake kupiga X-ray na kuonesha kuwa mguu na mkono wangu haujavunjika, japo michubuko nimeipata ya kutosha maeneo ya mkononi na mguuni, ila usoni kidogo sana.

Nipo mapumziko kwa ajili ya mguu kupungua uvimbe, ila maisha yanaenda. Hakika Mungu ni mwema bado ana makusudi na mimi.

Bodaboda nouma waungwana.
 
Kijana leo pole sana uachege ubahili ukodi hata bajaji bodaboda sio
 
Last edited by a moderator:
pole kijana.. boda boda wanasifa sana nowdays wanaendesha kwa mashindano
 
Pole sana, hakikisha unakuwa na waendeshaji unaowafahamu kitabia, wengine ganja sana, usipande yeyote tu watakuuwa.
 
pole sana mpendwa...kuna jamaa mmoja alipata ajali ya boda boda alibusu lami ngozi ya mikono na uso na miguu iliishia pale kwenye lami duh boda boda wapunguze viroba watatumaliza
 
Ndugu zangu humu ndani, namshukuru Mungu, siku ya juzi usiku nimenusurika kifo, baada ya kupata ajali ya bodaboda niliyokodisha kugongwa na gari. nilikimbizwa hospitali kuu ya mkoa na kupatiwa huduma ya kwanza, na kesho yake kupiga X-ray na kuonesha kuwa mguu na mkono wangu haujavunjika, japo michubuko nimeipata ya kutosha maeneo ya mkononi na mguuni, ila usoni kidogo sana. nipo mapumziko kwa ajili ya mguu kupungua uvimbe, ila maisha yanaenda. hakika Mungu ni mwema bado ana makusudi na mimi. ila bodaboda nouma waungwana.

Na huyu jamaa alokuwa anapitisha picha yako kuchangisha msiba ushamzuia asiendelee?kwa maana alisema hiyo bodaboda imekuua.
 
Na huyu jamaa alokuwa anapitisha picha yako kuchangisha msiba ushamzuia asiendelee?kwa maana alisema hiyo bodaboda imekuua.

du mkuu, huyo atakuwa mwingine, sio mimi, mi nipo vizuri na majeraha yangu tu hapa.
 
Back
Top Bottom