Nimenusurika kichapo mfungo huu wa ramadhani

Daktari wa minyoo

Senior Member
May 15, 2019
117
114
Kwanza kabisa naomba mnipe pole wanajamvi kabla hata ya kutoa maelezo yoyote yale.

Leo mida ya saa 6 mchana hv nlikua nakatiza mitaa flani hapa znz nikiwa natafuna zangu vikaranga tu vichache nilivyotoka navyo home, Eeeh bwana eeeh si nkashangaa ghafla tu nimezungukwa na njemba ka 5 hv.

Zikaanza kunihoji kwann nimekua mkaidi kiasi hicho cha kuwaharibia watu swaumu zao, yani nikawa najaribu kujielezea huku nimekwidwa kama kibaka.

Nikawaomba wazee waniachie kidogo nijieleze duh, mshikaji ameniachia shati tu nmechomoka kama mshale. Yaani siamini kama nimenusurika kula kichapo kutoka kwa masheikh asee.

Kwakweli sitarudia hata kumeza mate mbele ya watu ktk kipindi hiki cha mfungo hapa Zanzibar.
 
Ungeendelea kutafuna alafu wangeleta zakuleta unaanzisha Vita ambayo itaamuliwa na Polisi tu.

Yani unalazimsha watu wote wafunge Pumbaaavu nini maana ya funga

Manufaa ya funga ni nini si ya mtu binafsi watakudharau hao ungechapa mkono vibaya sana na hudhuria mafunzo ya Karate ili huo upumbavu uwe unautendea haki
 
Mi ninavyo jua HASIRA na VISASI ni kazi za shetani. Najua pia mtu akiwa kwenye mfungo hua anakua karibu sana na Mungu and hence hata tabia zinaweza kufanana na tabia za Mungu kwa mbaaaali na ndio maana watu wakifunga huaga wanatoa vitu vyao kuwapa masikini nk, sijui aina hi ya hawa "wacha mungu" sijui kwanini wana hasira namna hi, ukweli sijui.
 
Shukuru.Mungu ungeliwa kiboga baada ya kichapo heavy toka kwa maustadhi! (Wangekufuturu)
Yaani mtu mzima unabeba Karanga na kutafuna barabarani? Kwanini usile huko huko home kwako?
Nyie ndio mnaotafuna BIG G kuanzia asubuhi hadi jioni??
 
sijui uliniponyokaje pale tulipanga tukutandike leo,ila una mbio na hayo matege yako
 
Hawa watu hatari sana yani hadi karanga tu kutafuna shida, yani mtu hata kumumunya pipi hadharani tu wanaweza wakakukabiri. Very pathetic people,
Hiki kisiwa huwa kinakua kichungu sana kipindi kama hiki.
 
Shukuru.Mungu ungeliwa kiboga baada ya kichapo heavy toka kwa maustadhi! (Wangekufuturu)
Yaani mtu mzima unabeba Karanga na kutafuna barabarani? Kwanini usile huko huko home kwako?
Nyie ndio mnaotafuna BIG G kuanzia asubuhi hadi jioni??

Kwa hiyo kumbe hadi kutafuna karanga mtu ujifiche, hivi hiki kitu kimeandikwa kwny Quran ama ni kuna baadhi ya watu ni veherehere tu.
 
Back
Top Bottom