Nimenunua bundle la wiki, usiku naambiwa bando la siku limeisha

BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,735
5,005
Siwasemi kwa ubaya angalieni vituko vinavyonijia kwenye simu yangu hii ni wiki ya tatu sasa. Naamini Airtel mko hapa. Jana mida ya saa kumi nimenunua bundle la wiki na hongera juu mkanipa expire date 27 November. Saa tatu usiku mnanitumia bundle lako la siku GB 1 limeisha.

Naomba kuuliza hili bundle nani amenunua la siku moja na iweje ninunue la wiki nipate message mbili tofauti ama line yangu ina ka uspecial fulani na wengine?

Kwa nini nimeamua kuwajulisha hili, muwe makini sana msikimbilie kusoma message mkakimbilia kujazaa tena vifurushi. Nilipowapigia wakasema mbona una 975 MB. Nikauliza na hii message ya bundle la siku tena GB 1 imetoka wapi na nani kwa nini mnanirushia wakati sijajiunga na kifurushi cha aina hii?

Onyo: Muwe makini sana na hawa watu wa mitandao wakati mwingine wanahisi mmelewa. Ukisoma tu message utakimbilia ku topup hela.

Screenshot_20191121-060845.png


Screenshot_20191121-060826.png


Screenshot_20191121-060905.png


Screenshot_20191121-060851.png
 
Back
Top Bottom