Jinsi ya kutumia bando kidogo la internet kwa siku/wiki/mwezi kwenye simu na kwenye PC ya window 10

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
29,087
2,000
Naenda moja kwa moja kwenye mada.Nilikuwa ni mhanga wa bondo la internet kuisha haraka sana hadi nikawa nalaumu kuwa mitandao ya simu ni wezi wa kutupwa.Matumizi yangu kwa siku ni ya kawaida sana kwani huwa natumia simu yangu kuchat hapa JF,instagram,twitter,telegrama mara moja moja na kwenye whatsapp mara moja moja pamoja na wifi kwenye PC yangu lakini kwa wiki gb 10 zilikuwa hazinitoshi,yaani kwa siku nilikuwa natumia zaidi ya 1gb mpaka 2gb

Hiki kitendo kilikuwa kinanikera sana hadi nikawa nakata tamaa ya kutumia internet kwani ilikuwa inanigharimu sana.Sikuwa najua ni kwa nini bando linaisha haraka sana.Sasa kwa kuwa natumia PC yenye window 10 huwa inajiupdate mara kwa mara ila ilikuwa inaniwia vigumu kujua inakula bando kiasi gani lakini nilikuwa nahisi itakuwa inakula bando kubwa sana.

Siku moja nikaingia humu JF kutafuta msaada jinsi ya kuzima automatic update katika window 10 nikakutana na uzi wa mtu mwenye shida kama hiyo hiyo ambapo watu wengi walimshauri aweke pc yake katika metered connection ila mimi nilijaribu kuweka katika metered connection nikashindwa.Nikaendelea kuhangaika ila likanijia wazo kuwa huenda play store inaweza kuwa na majibu.

Nikaingia play store nikakutana na application inayoitwa my data manager halafu nikaiweka kwenye simu yangu.I was shocked!Hii application huwa inaonyesha vizuri sana na kwa usahihi ni kitu gani kinakula internet kwa siku na kwa kiwango gani,kwa wiki hata kwa mwizi.Yaani haiachi kitu,inaonyesha kila application pamoja na bando inayokula.Kumbe kilichokuwa kinakula bando langu ni PC yangu yenye window 10 ambayo huwa inaupdate karibia kila siku na ikiupdate inakula hata gb 1 au zaidi kwa siku.

Kitu kingine ambacho nilikuwa natumia tu bila kujua kinakula internet kwa kiwango gani ni instagram.Instagram huwa inakula bando ile mbaya.Ilinibidi niingie google fasta nijifunze jinsi ya kuset pc kuwa metered connection ambapo baada ya hapo nilijikuta naanza kutumia internet kwa MB 200 hadi 300 kwa siku kwani pia nilijiwekea utaratibu maalum wa kutumia zile application zinazokula zaidi bando.Yaani matumizi ya bando la internet kwa siku yalishuka sana ghafla.Nashauri sana tumia hii application ya my data manager kwani utajua ni kitu gani kinakula bando lako zaidi na ukicontroll vipi.

Jinsi ya kuset PC ya window 10 kuwa metered connection kwa wale wanaotumia internet ya wifi kutoka kwenye simu zao kwenda kwenye PC ingia hapa(Hii haiwahusu wanaotumia njia nyingine za kupeleka internet kwenye PC zao kama vile bluetooth,e.t.c):https://support.microsoft.com/en-us...ndows-10-7b33928f-a144-b265-97b6-f2e95a87c408

Kabla ya kufuata hatua zinazoelekezwa katika hiyo website hakikisha kuwa wifi yako ipo on na PC yako inapokea internet kutoka kwenye simu yako.Kwenye hizo hatua ukishafikia kwenye kipengele cha manage known network hakikisha kuwa unachagua simu unayotumia halafu chagua properties halafu unaweka on sehemu iliyoandikwa metered connections.

Hii maana yake ni kwamba kila ukiwasha wifi ya simu yako window 10 itakuwa inadownload tu yale mafile madogo madogo ambayo yanawezesha window 10 yako kujiendesha na itaacha kudownload mafile makubwa yanayohitaji bando kubwa.Lakini hapa kilichokuwa set kama metered connection ni simu yako tu ila siku ukiwa na net work nyingine ambayo ni tofauti na simu yako then mafile makubwa yataendelea kujidownload kama kawaida.Siku ukitaka window 10 yako iendelee kujiupdate kama kawaida unafuata process zote hapo juu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwanza kuwa wifi ya simu yako ipo on na PC yako inapokea internet kutoka kwenye hiyo simu yako kisha unaenda kwenye setting za kwenye PC yako kama kawaida kisha unaweka metered connection off.Hizi process ukifanya simu yako ikiwa imezimwa na PC yako ikiwa haipokea internet kutoka kwenye hiyo simu yako hazitafanikiwa na hiki ndiyo kilinikwamisha mimi mwanzoni kama nilivyoandika hapo juu kuwa nilishindwa kuset PC yangu kama metered connection.

Nilichojifunza pia ni kwamba kinachomaliza bando la internet siyo kukesha kwenye mitandao bali umekesha na mtandao gani.Ukikesha kwenye JF au twitter hakuna bando litaisha ila ukikesha kwenye instagram,youtube au ukiwa na PC yenye window 10 ambayo inaupdate automatic tegemea maumivu.Internet kwa sasa hivi imekuwa kama basic needs kwa hiyo ni muhimu kujifunza jinsi ya kubana matumizi yake kwa kuwa tunaitumia kila siku.78907654.jpg
 

Mzee23

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
1,088
2,000
Ufanye na settings kwenye hiyo pc 'inayojiapdet' kila siku

Instagram inalaumiwa sana kwenye kula bando! Sema Sijawahi kuitumia
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
29,087
2,000
Ufanye na settings kwenye hiyo pc 'inayojiapdet' kila siku

Instagram inalaumiwa sana kwenye kula bando! Sema Sijawahi kuitumia
Hakuna haja ya kufanya setting kila siku.PC huwa ina uwezo wa kushika kumbukumbu ya net work iliyowekwa kama metered connection kwa kuchukua na kuhifadhi IP address ya network husika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom