mtanganyika mpya
JF-Expert Member
- Feb 6, 2015
- 424
- 302
Umri wangu ni miaka 44, sijaolewa na sina mtoto. Ninafanya kazi katika Taasisi ya Serikali, mwanzoni mwa mwaka huu nilipelekwa semina kwa wiki moja.
Tukiwa kule kiti changu kilikuwa karibu na kiti cha kijana mmoja, mrefu, nadhifu, mcheshi. Tulifikia hoteli moja, baada ya siku tatu tulibadilishana number za simu maana tuliweza kuelekezana migahawa mizuri kwa chakula.
Semina iliisha Ijumaa na tuliagwa kwa tafrija baada ya hapo kila mtu aliekea alikotoka.
Mimi na kijana tuliendelea kuwasiliana kwenye whatsApp, imefikia katika hali kuwa, nikiamka asubuhi lazima tusalimiane, tunabadishana picha za lunch, usiku ndio kabisa tunachat masaa mawili-matatu. Ilitokea nikamuuliza hivi unahisi mimi nina miaka mingapi?
Akajibu 28, nilicheka, nikaamua kukaa kimya. Moyo wangu umempenda sana, sasa lakini niliamua kumueleza ukweli. Alishtuka na kukaa kimya, nikajua basi ameshaondoka.
Kesho yake alinipigia simu akaniuliza kama nilishawahi kuolewa, je nina mtoto. Akajibu umri kwake sio tatizo. Yeye ana miaka 31, anakazi nzuri sana.
Weekend iliyopita alikuja kunitembelea, alifika Jumamosi asubuhi, kwa sababu bado tunafahamiana alichukua hoteli mjini, alikuja kwangu jioni, tulikaa tukaongea mpaka saa nane usiku, akaondoka kurudi hotelini kwake, kesho yake alirudi kwake.
Dada yangu mkubwa ambae mtoto wake wa kwanza ana miaka 29 ameniambia nimuache kijana kwani ni sawa na mwanangu! Kijana mwenyewe amekiri kuwa kwao wazazi wataleta zengwe, amenishauri tuzae kwanza kabla hajanipeleka kwao.
Ushauri jamani
Love, CareMe too.
You are brutally honest44yrs , no Husband no kid/kids...Nadhani its too late...honestly.. ukizaa now..ukifika 50 yrs mwanao ndo atakua 6yrs..yani hata shule hajaanza,.
Its too late. lets be realistic .
Lol bebaneni,love is love sex is sexDada mpaka sa8 usiku mnaongea tuu live bila chenga wala umeme kukatikakatika??
ushauri....wewe kama mnapendana bebaneni tu muoane tena kwa shangwe zote! wambie unamiaka28! kwani wakwe watadai cheti cha kuzaliwa???
Wewe atafika fifte sasa ivi bila mtoto mwache azae banaUckubali kuzaaa mama angu ohooo
44 bado anazaa...hata hivyo kama anazaa bora azae tu coz kwa mwanamke miaka yote hyo then mnamshauli asizae...it is not fair....otherwise kama ameamua au hana haja na familia..Usithubutu kuzaa, huu ushauri wa bure tu nakupa!
Kwani wangapi wamezaa na wameachwa?.
Km kweli yupo serious na ni mpango wa Mungu itakua tu dada yangu!!...
Huyo Dada ako nae ataingiliaje mapenzi ,hajui ni makubaliano ya watu 2!
.sorry,huyo Dada ako kaolewa?
Huyo kaka anasema kwao wataleta zengwe,kwahiyo ataenda kuwatangazia ndugu zake kuwa umemzidi?..
If so,hayupo tayari kukudefend huko kwao!?
Dada Yangu muombe Mungu,ukipata amani moyoni jua ndie ,na km ndie hakutakuwa na chochote kitakachozuia,means kila mmoja wenu atakua tayari kudefen penzi lenu!!
Nb:naona anataka kujua km unaweza kuzaa.
Mtazamo wangu tu!!!
Uko sahihi mkuuKuna wakati wanaume tuwe tunaangalia mbali na si mbele tunapofanya analysis ya mambo ambayo yana umuhimu sana maishani.
Tofauti ya miaka 12 kweli?!