Nimemzalisha ndugu yangu bila kujua, naomba msaada wa mawazo

Ntikwite

Member
May 13, 2017
93
52
Habari zenu wanaJF wenzangu, naomba msaada wa kimawazo mimi ni kijana mwaka 2015 nliingia kwenye mahusiano na binti ambaye kwa baadaye nilikuja kugundua kuwa ni ndugu yangu kiukoo yaani baba yake namuita baba yaani tulishare babu zetu wazaa baba.

Baada ya huo mwaka mimi nilienda mikoani kwenda kutafta maisha nikakaa huko hadi 2017 ndio nikarudi home baada ya hapo ndiyo nikawa nimempachika mimba na baada ya mwezi mmoja ndiyo nikagundua kuwa ni ndugu yangu, na nilichogundua tena kumbe yeye alikuwa anaujua undugu wetu lakini hakuniambia kabla.

Na baada ya kupata hiyo mimba aliniambia yeye atalea hiyo mimba na hatawaambia nyumbani kwao kuwa ile mimba ni yangu kwa sababu sisi ni ndugu japo kuna muda wanambana sana amtaje baba wa mtoto ila anaogopa.

Na namshukuru Mungu alimjaalia akajifungua japo kwa kisu mtoto wa kiume mpaka sasa ana mwaka na miezi mitatu.

Naombeni msaada wa mawazo ndugu zangu.
 
Wote Mlikuwa Mnafanya wakati mnajuana "inbreeding" angalia sentensi yako hii hapa " na baada ya kupata hyo mimba aliniambia yeye atalea hyo mimba na hatawaambia nyumbani kwao kuwa ile mimba n yangu kwa sababu sisi n ndugu".Ni ujinga Ulioufanya kwenda kuzaa na dadayako as if there are no other women, Cheap always is expensive, so enjoy aibu yako Nyambafu.
 
Huyo dada mlijuana vipi na yeye nataka kujua hadi mnaanza mahusiano ulikuwa naye kijijini kwenu au wapi. Maana haiingi akilini useme yeye alikujua kuwa ni ndugu ila wewe hukujua.

Hadi unaanza mahusiano na yeye hata huyo baba yake ambaye ni baba yako hukuwahi kuonana naye na humjui?

Hamna haja ya kuficha, wekeni mambo wazi.

Ndio imeshatokea, mtafanya nini?

Iteni kikao muwajumuishe watu wazima kwenye Familia yenu na muwaambie ukweli.

Nafahamu ni jambo zito sana jinsi ya kuanza kuelezea, ingawa haitokuwa rahisi mwanzoni, itafikia wakati watakuja kuelewa tu.

Haitokuwa jambo zuri mtoto wenu akue kama hana Baba vile ilhali Baba wa Mtoto yupo
 
Huyo dada mlijuana vipi na yeye nataka kujua hadi mnaanza mahusiano ulikuwa naye kijijini kwenu au wapi. Maana haiingi akilini useme yeye alikujua kuwa ni ndugu ila wewe hukujua.

Hadi unaanza mahusiano na yeye hata huyo baba yake ambaye ni baba yako hukuwahi kuonana naye na humjui?

Huy binti walihamiaga hapo kijijin kwetu mimi siku moja npo na babayangu tukakutana na babayake baba akanitambulisha kuwa n babayangu ila watotowake nikawa siwafaham mpka inakuja kutokea hyo inshu kwahyo mimi na babayake tunajuwana vizuri tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wote Mlikuwa Mnafanya wakati mnajuana "inbreeding" angalia sentensi yako hii hapa " na baada ya kupata hyo mimba aliniambia yeye atalea hyo mimba na hatawaambia nyumbani kwao kuwa ile mimba n yangu kwa sababu sisi n ndugu".Ni ujinga Ulioufanya kwenda kuzaa na dadayako as if there are no other women, Cheap always is expensive, so enjoy aibu yako Nyambafu.
Asante kaka ila mimi nlikuwa sijuw ila baadae nlikuja kugunduwa kuwa binti alikuwaga anajuwa unduguwetu japo Hakuniambia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh kama ulikua haujui usingeficha hio siri.. kuficha siri ni sawa na kukubaliana na uovu wenu.. hata hivyo undugu wenu ni wa mbali sana biologically hakuna effect sana.. genes kadhaa zilishachanganyikana kuanzia kwa babu yenu na baba zenu...
Kwahio wewe angalia kipi chema, kusema ukweli then kusubiri litakalotokea au kuendelea kuficha siri (hadi lini??)
 
Mkuu, ebu eleza vizuri!?? Maana huyo ni mtoto wa baba yako mdogo/mkubwa, sasa nini kilipelekea msitambuane!??

Mlikutana katika mazingira gani!??

Sent using Jamii Forums mobile app
Labda nikueleze kwa mifano , ufipani tunaishi kwa makabila yapo makabila Mbali mbali kama sinkala, siyame,simchindo,sinkonde nk sasa huyo binti tumeshare ukoo ambao ukifuatilia kiundani ndo unakuja kukuta kuwa babayake natakiwa nimwite baba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom