Nimemwachia Kunguru, wenye mitego naseni... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimemwachia Kunguru, wenye mitego naseni...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Magulumangu, Jan 6, 2011.

 1. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nilimnasa kwa tundu bovu, nilitegesha misosi, mazagazaga kibao, nalo likanasika, likafugika ingawa kwa tabu na maumivu mingi kwangu, Kunguru kila mwanya likipata ujue hutoroka hadi usuke mtego kulikamata, Sasa Natangaza rasmi, NIMELIAHIA KUNGURU mwenye mtego alinase.....
   
 2. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  Deuces Lyrics

  All that bullshit's for the birds
  You aint nothin but a vulture
  Always hopin for the worst
  Waiting for me to **** up
  You'll regret the day when I find another girl, yeah
  Who knows just what I need, she knows just what I mean
  When I tell her keep it drama free
  Ohohohohohohohoh… x2(Chuckin up them(deuces)
  I told you that im leaving (deuces)
  I know you mad but so what?
  I wish you best of luck
  And now im finna throw them deuces up............
   
 3. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kunguru halitaka watunga Verse mkuu, linataka wazee wa EPA maana minyama kwao litapata....Limepaa Kunguru kwenda Unguja kwa mashehe
   
 4. u

  utiyansanga JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2011
  Joined: May 19, 2010
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lIAMBIE SAFARI NJEMA YA KUPATA MWINGINE KAMA WEWE!
   
 5. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #5
  Jan 6, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Magulumangu.....ninachoweza kusema ni kuwa wewe si mfugaji mzuri umekurupukia mifugo usoiweza........wangapi tumewaona wamechukua mikunguru tena ile ya zanzibar na wameibadilisha ikawa njiwa kama wale waofugwa enzi za wana Israel wakati njiwa wakiitwa Hua.
  pole
   
 6. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #6
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nimeiimbia ule wimbo wa wewe mapepe wa Kingwendu...
   
 7. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  hehehehehe mkuu duh yaweza kuwa mie na mifugo basi, ila huyu Kunguru mwache aende zake, dege lisilofugika hili jamani
   
 8. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,901
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Midege mingine haifugiki jamani..!!
   
 9. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #9
  Jan 6, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kabla hujamwacha alikua kasuku?
  Haya mambo mengine jamani... Kwani huwezi kusema umemwacha Kasuku?
   
 10. s

  shosti JF-Expert Member

  #10
  Jan 6, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Khaaaaaaa!!!
   
 11. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #11
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,901
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  ??????????
   
 12. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #12
  Jan 6, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kwa mashehe.....ila masheikh wapenda Njiwa.
   
 13. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #13
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu nimeliacha liende zake mie sitaki kufuga hii mindege...
   
 14. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kasuku mhhh naye lakini kiama chake kwa majirani, kila linalotokea mtaani yeye, lifanyikalo mjini analijua...ila huyu Kunguru kakaaaa usiombwe kumfuga utakoma...
   
 15. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #15
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ndo yalikotokea haya Makunguru mzee huko Zanzibar....aaaacha liende huko huko mzee...
   
 16. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  unamuongelea kunguru au mtu? nieleweshe mie
   
 17. mapango

  mapango Member

  #17
  Jan 6, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  kunguru ana wenyewe, humuwezi asilani
  atakutia kiwewe, kuzidi umasikini
  ulimtega mwenyewe, sielewi ni kwanini
  una matatizo wewe, kutojuwa vya thamani?

  limtegea mizoga, hilo pia ni tatizo
  nyamu tamu ametega, jamaa kaja anazo
  wajua kunguru mwoga, ila bingwa wa mizozo
  amevunja lako bega, mwishowe mepata wazo

  sio tu wa zanziba, kunguru tabia yao
  hata wale wa Bukoba, na huruma hawanayo
  na hupiga hadi roba, kupata chako niyao
  kunguru hawana baba, kubali hawana kwao
   
 18. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #18
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Kunguru asiefugika mkuu, kiswahili vipi weye ulikuwa unakula kona nini?
   
 19. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #19
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  kiswahili saa zingine kigumu, asante kunielewesha


  hivi unajuaje haraka kaa mtu amejibu baada yako humu, nachoka kusaka posts
   
 20. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #20
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Navyojua ni muwoga,na sumu hutotumia,
  Mitego kutokutega, akili hutotumia,
  sikuhitaji mshenga,wala sikudhamilia,
  sina matatizo mimi, navijua vya thamani,

  acha liende zake, likutane na waovu,
  nililipa vitu mwake, likaona mi mchovu,
  halina hata yake, heshima japo chovu,
  hata wazo sina, ni kiuno sio bega,,

  acha niende kwa bibi, nikalione chabivu,
  nitaliita habibi, likijibu kwa maivu,
  nitalipa hanibi, lipokee bila wivu,
  Acha walile huko,mtungo litajiju,

  uvuvuzela naacha, narudi kitaani,
  wengi kunakokucha, kunguru wako vitani,
  marefu yake makukucha,hata huko utosini,
  Mtego wako ukinasa, kama kunguru achia
   
Loading...