Nimemuota mama yangu aliyefariki kitambo amerudi kama vile katoka safari kapendeza hatarii

flulanga

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2016
Messages
3,839
Points
2,000

flulanga

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2016
3,839 2,000
Wakuu usiku waleo kiukweli nimeota ndoto nzuriiii sanaaaa tena sana naweza sema nindoto nzuri kwangu kwahuu mwaka toka uanze. Unajua ile unaota ndoto nzuri alafu unashtuka kumbe ulikuwa unaota, unaanza kujilaumu kwanini umeshtuka.

Ipo hivi mama yangu kafariki zaman sana, ila nimemuota amerudi tena kapendeza, mwenye furaha tele. Akawa kawaona watoto wangu akafurahi sana ila sio kama alikuja moja kwamoja ila alikuwa anajiandaa kwasafari yaani aondoke tena. Nikawa namtafuta mpenz wangu/mzazi mwenzangu aje amuone mama yangu alivyo mzuriiiii...

Nikawa nahesabu pesa ili nikaweke bank ila sikumbuki hizo pesa nizanani, sikumbuki kama alinipa yeye au lah! Pesa zilikuwa sio Chini yamilioni mbili, alafu mda huo bank hata sio mbali yaani bank ipo nyuma yanyumba tu wakati kiuhalisia hakuna bank maeneo yanyumbani. Nikawa namwambia kuwa umeona maendeleo bank tumesogezewa karibu ukiondoka tena ukirudi utakuta nasoko limejengwa hapo kwajirani akachekaaa.

Mda huo nababu yangu nae alikuwepo nababu mkubwa nae alikuwepo nahawa wote walishafariki. Namda huo babu alikuwa anazaja makaratasi nakuweka sahiii nadole gumba hayo nimakaratasi kama vile ya mashamba nakiwanja nawalikuwa wanaweka sahihi ili wanapoondoka wasiache utata maana walikuwa nikama wapo kwaajili yakuondoka.

Namda huohuo walikuwepo mjomba wangu namama yangu mkubwa hawa wote wazima ila ninamasiku hatujaonana.

Kiukweli hii ndoto ilikuwa ninzuriii sana hasa hasa kukutana namama yangu aiseee nilikuwa nimemmisi sana alafu kwajinsi alivyokuwa kanawiri nafuraha niliyokuwa nayo ndio iliongeza chachu.

Mwenye kujua maana yahii ndoto aiseee samahani aniambie jamani duh kuna ndoto jamani nzuriiii
 

mangatara

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2012
Messages
13,737
Points
2,000

mangatara

JF-Expert Member
Joined Jul 6, 2012
13,737 2,000
Kuna jambo moja lazima ulielewe; Kumuota mtu aloyekwisha fariki na mkazungumza naye mkajibizana maneno flani flani ni ishara kuwa, Utapatwa na ugonjwa mbaya sana siku za karibuni. Ikirudia tena ni kukuonesha kuwa huo ugonjwa hautachelewa kukujia.
Ukiota wamefanya sherehe yako ni ajali inakupata.
Hii ndoto yako sio nzuri sana kwani inaonesha soon utaparwa na ugonjwa mbaya sana. Ile furaha yako itageuka kuwa huzuni nyingi. Pole sana
 

3 Angels message

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2017
Messages
2,222
Points
2,000

3 Angels message

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2017
2,222 2,000
Hakuna lolote la maana, itakuwa ulikuwa unamuwaza sana ubongo ukafanya yake usiku

Mama alishalala umauti hawezi kuzuka tena kurudi tena. Ingawa uwe makini maana shetani anaweza kumleta pia ili ajidai anakupa maelekezo ikitokea kemea maana atakuwa siyo mama bali pepo aliyechukua mfano wa mama yako
 

Mtamba wa Panya

Senior Member
Joined
Aug 6, 2017
Messages
168
Points
500

Mtamba wa Panya

Senior Member
Joined Aug 6, 2017
168 500
Kwanza nikupe ovyo; USIPENDE KUANIKA NDOTO ZAKO PUBLICLY KAMA MITANDAONI

UFANYE NINI: Kuna watu wanaelimu ya ndoto kawaulize

Huku mitandaoni kuna "mizwazwa" mingi inayojifanya inajua kila kitu. Kama hao walio comment Hapo juu, ni wazi hawana elimu yoyote ya Ndoto:

Kwa kifupi tu: Jiandae na mafanikio katika mambo yako yote/baadhi yaliyokuwa yamekwama. Hii inategemea na furaha/uchangamfu uliomuona nao mama yako kwenye ndoto hiyo.

Hakuna ndoto nzuri katika maisha ya mwanadamu kama kuota wazazi wake.. hasa hasa mama yake mzazi akiwa na furaha.

Ukiota kuna uadui unakufuata mfano nyoka mweusi halafu hapohapo ukamuota mama yako mzazi , maana yake huo uadui hautofanya kazi. Haimaanishi mama yako ni mchawi! Lahasha!

Kama mambo yalikuwa magumu ukamuota mama yako mzazi, ni dalili ya kufunguka mambo yako na kuanzia hapo yatakuwa mepesi..

All this is created by your subconscious mind... your mother will always have a special place in your soul...

Kumuota mama yako aliyefariki haimaanishi alichukuliwa na wachawi, hiki nikichekesho kikubwa
 

flulanga

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2016
Messages
3,839
Points
2,000

flulanga

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2016
3,839 2,000
Hakuna lolote la maana, itakuwa ulikuwa unamuwaza sana ubongo ukafanya yake usiku

Mama alishalala umauti hawezi kuzuka tena kurudi tena. Ingawa uwe makini maana shetani anaweza kumleta pia ili ajidai anakupa maelekezo ikitokea kemea maana atakuwa siyo mama bali pepo aliyechukua mfano wa mama yako
Sawa nashukuru
 

flulanga

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2016
Messages
3,839
Points
2,000

flulanga

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2016
3,839 2,000
Kuna jambo moja lazima ulielewe; Kumuota mtu aloyekwisha fariki na mkazungumza naye mkajibizana maneno flani flani ni ishara kuwa, Utapatwa na ugonjwa mbaya sana siku za karibuni. Ikirudia tena ni kukuonesha kuwa huo ugonjwa hautachelewa kukujia.
Ukiota wamefanya sherehe yako ni ajali inakupata.
Hii ndoto yako sio nzuri sana kwani inaonesha soon utaparwa na ugonjwa mbaya sana. Ile furaha yako itageuka kuwa huzuni nyingi. Pole sana
Duh Mungu apishirie mbali, Mungu nisaidie
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2018
Messages
2,705
Points
2,000

Alexander The Great

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2018
2,705 2,000
Mama yako anaonekana wakati wa uhai alikua akiishi maisha yanayompendeza mungu (Furaha aliokuonesha kwenye ndoto ni maisha ya furaha alionayo huko sasa hivi). Fuata nyayo za mama yako. Mungu amlaze salama.

Ungemuona ana huzuni na sura imechoka, basi ingeashiria ana maisha yasio na amani huko alipo.

USHAURI: Fanya maombi au dua za kumuenzi, pia mtolee sadaka hata kama ni ndogo (mfuko wa pipi kwa watoto wadogo n.k) kwa uwezo uliokua nao.
 

Song il gok

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2015
Messages
778
Points
1,000

Song il gok

JF-Expert Member
Joined Feb 23, 2015
778 1,000
Hiyo sio ndoto nzuri mkuu.Hiyo kaja kukuchukua.Kama umeokoka vunja roho ya sauti hiyo,si ajabu na wewe uko njiani.
Nimewaza kitu kama hichi pia,bibi yangu kabla hajafariki alikua anasema anawaona baadhi ya ndugu zetu waliofariki so hakuchukua round akfa,jamaa inabidi asali sana aisee,no one knows tomorrow
 

areafiftyone

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2017
Messages
6,508
Points
2,000

areafiftyone

JF-Expert Member
Joined Jan 4, 2017
6,508 2,000
Nimewaza kitu kama hichi pia,bibi yangu kabla hajafariki alikua anasema anawaona baadhi ya ndugu zetu waliofariki so hakuchukua round akfa,jamaa inabidi asali sana aisee,no one knows tomorrow
Hiyo ni roho ya mauti inakutafuta,wala sio bibi yako.Unatakiwa kuivunja katika Jina la Yesu,vinginevyo na wewe unakwenda mkuu.
 

mangatara

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2012
Messages
13,737
Points
2,000

mangatara

JF-Expert Member
Joined Jul 6, 2012
13,737 2,000
Duh Mungu apishirie mbali, Mungu nisaidie
Usiogope kwa lolote, Mungu akiisha kukuonesha jambo maana yake wewe sasa umelishinda. Mlilie Mungu zaidi ili akuvushe salama. Angekuwa hakupendi asingeli kuonesha.
Kama wewe ni mtu wa imani kumbuka hadithi moja iliyosema kuwa; Mungu alimwonesha mtumishi wake Ibrahim mambo aliyokuwa ameyadhamiria kuwatenda watu wa Sodoma na Gomora. Ibrahim akajitahidi kuwaombea rehema wale watu waovu na Mungu aliahidi kuwa kama kungelitokea watu wakaghairi uovu wao, wakaacha na kutubu, Mungu aliahidi kuwasamehe.
Tatizo ni kuwa, Hakukutokea yeyote aliye tubu bali wakamvamia Lutu na wageni wake toka mbinguni wakisema; Tunawataka hao wageni wako ili tuwatende uovu. Hata Lutu alipojaribu kuwatoa mabinti zake badala ya wale wageni; Japo Lutu hakuwa anawajua ni wa nani waliomjia. Tazama; yale majitu maovu yaliyojaa uovu ya Sodoma na Gomora wakamjia juu kuwa; Usituchagulie tunayemtaka leo kumsodomia. Hayo mabinti yako tunayaona hapa mlangoni petu kila siku, wala hayana mvuto. Tupe hao wageni.
Kumbe wanawataka malaika.
Wewe je, kuna jambo baya unalolitendaga? Sikuambii kuwa wewe nawe ni kama hao watu wa kisodoma ila maovu ni mengi sana duniani; Mfano: Wizi, mtembea na wake za watu/waume za watu, ukahaba, ulevi, hata kutokumuamini Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wako.
Mambo kama hayo huiamsha ghadhabu ya Mungu haraka sana. Usijifariji kuwa; Mbona kila mtu siki hizi anayafanya hayo. Hata wale wa kule Sodoma na Gomora walijifariji kuwa; Kila mtu mtaani kwetu hufurahia matendo yetu. Wakajiona "Machalii" kweli kweli. Kumbe Mungu alipowatumia malaika hawakumuona kama mjumbe wa Mungu.
Tafakari tu njia zako upatane na Mungu awezaye kukuepusha na mabaya yote yaliyokusudiwa juu yako.
 

Forum statistics

Threads 1,381,732
Members 526,184
Posts 33,810,262
Top