Nimemuota mama yangu aliyefariki kitambo amerudi kama vile katoka safari kapendeza hatarii

Kuna jambo moja lazima ulielewe; Kumuota mtu aloyekwisha fariki na mkazungumza naye mkajibizana maneno flani flani ni ishara kuwa, Utapatwa na ugonjwa mbaya sana siku za karibuni. Ikirudia tena ni kukuonesha kuwa huo ugonjwa hautachelewa kukujia.
Ukiota wamefanya sherehe yako ni ajali inakupata.
Hii ndoto yako sio nzuri sana kwani inaonesha soon utaparwa na ugonjwa mbaya sana. Ile furaha yako itageuka kuwa huzuni nyingi. Pole sana
Waafrika bwana dah
 
Kwanza nikupe ovyo; USIPENDE KUANIKA NDOTO ZAKO PUBLICLY KAMA MITANDAONI

UFANYE NINI: Kuna watu wanaelimu ya ndoto kawaulize

Huku mitandaoni kuna "mizwazwa" mingi inayojifanya inajua kila kitu. Kama hao walio comment Hapo juu, ni wazi hawana elimu yoyote ya Ndoto:

Kwa kifupi tu: Jiandae na mafanikio katika mambo yako yote/baadhi yaliyokuwa yamekwama. Hii inategemea na furaha/uchangamfu uliomuona nao mama yako kwenye ndoto hiyo.

Hakuna ndoto nzuri katika maisha ya mwanadamu kama kuota wazazi wake.. hasa hasa mama yake mzazi akiwa na furaha.

Ukiota kuna uadui unakufuata mfano nyoka mweusi halafu hapohapo ukamuota mama yako mzazi , maana yake huo uadui hautofanya kazi. Haimaanishi mama yako ni mchawi! Lahasha!

Kama mambo yalikuwa magumu ukamuota mama yako mzazi, ni dalili ya kufunguka mambo yako na kuanzia hapo yatakuwa mepesi..

All this is created by your subconscious mind... your mother will always have a special place in your soul...

Kumuota mama yako aliyefariki haimaanishi alichukuliwa na wachawi, hiki nikichekesho kikubwa
Amen...

Nilimuota mama aliyekwishafariki tumekaa tunaongea tunacheka. Baada ya wiki mbili jambo ambalo lilikuwa limekwama kabisa kwa muda mrefu likafunguliwa. Check ya dola 48, 680 ikanifikia.

Katika imani yangu naamini kuwa wafu hawajui lolote na hawana madhara yo yote kwa walio hai bali wanasubiri siku ya mwisho waje wahukumiwe kulingana na matendo yao.

Mama pumzika salama huko uliko. Kaburi lako nimelitengeneza vizuri kwa hadhi unayostahili. Tutaonana siku moja
 
Back
Top Bottom