Najaf
JF-Expert Member
- Jun 20, 2015
- 1,545
- 2,542
Kwa hakika nilimpenda kwa kila tone la damu yangu kwa tunu ya roho yangu, sina kazi wala mishe ya uhakikia bali nikuunga unga tu. Ninajisikia uchungu kila ninapokumbuka aliposema" hunijui chupi wala pedi, huwezi kuwa mwanaume tena."nilimjibu" kwa kuamka nikiwa na afya njema na hali ninaweza kufanya majukumu ya kibaiolojia kama mwanaume inatosha, pesa na vingine vitakuja nyakati zitakapofika.
Ndipo ilipofika kipindi nikaona mapenzi bila pesa kweli huwezi yapata na kwa kuamini huku sitaki kuamini mahusiano kwa kipindi hiki kigumu ambacho sins pesa. Moyo ni jicho linaloona wasichana ambao watautesa roho yangu kwa kipindi hiki nisicholambika mikono, maana ni mitupu mnoo.
Nimeshajiapiza kumpenda ambaye hatakuwa na mlengo wa maslahi ya pesa. Poleni wanaume wenzangu mnao nyanyasika kwa kutokuwa na pesa katika mahusiano yenu. Mungu awatie subira wanaowapenda wenza wao katika vipindi vyote vya mababadiliko kimaisha.
"Mungu nibariki nipate atakayenifaa kwa dhiki zaidi"