Nimemtongoza kaniambia ana mchumba lakini...

EL ELYON

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
1,563
1,886
Habari za asubuhi wakuu, kuna dada nipo naye kwenye group moja la whatsapp la mambo ya dini nimekuwa nikichart nae sana mpaka usiku wa manane nilimuomba awe rafiki yangu akakubali bt lengo langu nilitaka nimsogeze karibu kisha nimtokee kweli tumezoeana sana full kumsifia sifia status zake zote sasa niliamua kumpa ukweli wa lengo la kumuomba urafiki.

Mi nataka awe mpenzi wangu na mbeleni nimchumbie ilikuwa ni usiku wa juzi akanijibu ngoja afikirie nimpe muda nikamwambia poa sasa jana usiku akanitumia sms kwamba yeye ana mchumba wameahidiana ahadi nyingi sana na anaogopa kuwa msaliti wa ahadi hizo mmh nikamwambia sawa haina shda na asante sana bs akaanza kulalamika kwamba anajisikia vibaya mi kuumia kwaajili yake.

Nikamwambia hapana nipo pamoja na wewe naheshimu mawazo yako utaendelea kuwa rafiki yangu kiukweli mi nampenda yaani nimempenda sana hata nikimwambia nirushie picha zako anarusha kama 20, hawez kulala mpaka tuagane je wajuba na mabaharia huyu tampata kweli au nimpotezee kabisa. nipeni mbinu mpya.
 
hope1985, Umri wako utakua ni mdogo sana. kua na bidii ktk kutafuta maisha na hayo mambo yatakuja yenyewe..nasema umri wako ni mdogo kwa sababu nimetazama jinsi ulivyo andika na ushauli unao utaka kwa watu mpaka nimeshangaa,kua busy na pesa kwa bidii utengeneze maisha badala ya huu upuuzi.
 
Umri wako utakua ni mdogo sana. kua na bidii ktk kutafuta maisha na hayo mambo yatakuja yenyewe..nasema umri wako ni mdogo kwa sababu nimetazama jinsi ulivyo andika na ushauli unao utaka kwa watu mpaka nimeshangaa,kua busy na pesa kwa bidii utengeneze maisha badala ya huu upuuzi.

Kwenye profile yake kaandika ana 34,kazaliwa 1985 so huu mwaka anafikisha 35

Ni mkubwa sana huyu
 
Hata huo umri bado ni mdogo tu wa kupambana na maisha kindaki ndaki kweli kweli badala ya kupoteza muda...Basi ana ujinga
Kwenye profile yake kaandika ana 34,kazaliwa 1985 so huu mwaka anafikisha 35

Ni mkubwa sana huyu
 
Kwenye profile yake kaandika ana 34,kazaliwa 1985 so huu mwaka anafikisha 35

Ni mkubwa sana huyu
Si mkubwa uyuu maana kama angekuwa mkubwa angekuwa anamla uyo msichana maana tayari kakubali Ila kamwambia uhalisia kwamba asiweke moyo kwake wale Raha tu
 
Hata yeye anakupenda. Sasa alitaka muda wa nini wakati ana mchumba. Komaa nae mkuu, mpore kwa muhusika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom