Nimemsikiliza Mzee Butiku dakika 45 za ITV na Radio One ameongea mengi, ila haya ndiyo yameonyesha kwanini Yeye ni Hazina ya Fikra Kubwa Tanzania

Mtawala katili kama huyu hawezi sikiliza kitu chochote
 
Hiyo point ya 7 sikubaliani nayo. Hivi kweli uchaguzi iliyofanywa na Tume ya Mahela kwa maelekezo toka juu.... Huyu mzee bado anataka kutuaminisha kuwa ni sisi ndiyo tuliowaweka madarakani....!! Seriously....!!
 
Hata Lisu ni muog tu ndiyo maana alijificha kwenye ubalozi na kisha kukimbiza ubawa wake Ubelgiji.
At least yeye ana sababu ya kuogopa baada ya kunusulika na kifo. Pia anachoogopa yeye ni kifo ila haogopi kusema...... Ila wengi wetu kusema tu tunaogopa!!
 
Umezuiwa kuanzisha Uzi unaomhusu Slaa? Yeye kapenda maelezo ya Butiku na ana sababu ambazo Wenye busara ndani ya JF wanajua Kwa nini!! Wewe kama unaona aliyoongea Slaa yana uzito anzisha Uzi wako watu wachangie.
'Genius' kama Wewe Mkuu na Rafiki yangu mkubwa hapa JamiiForums unapata wapi muda wa kuppteza Kumjibu huyo 'Certified Fool' aitwae KING KIGODA?

Ukiona GENTAMYCINE namnyamazia Mtu ambaye ama amenikwaza au amenichokoza hapa JamiiForums jua ya kwamba nakuwa 'nimeshamdharau' kwa Kiwango cha Kumfananisha na Kinyesi cha Uharo na Kinachonuka kwa Kutukuka.

Hata hivyo Heko tu kwa Kumpa makavu.
 
Ujamaa/Socialism upo wa aina nyingi sana hapa duniani.
1. Kuna ule Ujamaa wa Kimarksi (Marxism) ambao ulikuwepo Urusi, Uchina na Afrika.
2. Kuna ule Ujamaa wa Kidemokasia (Social-Democracy) ambao kule kwenye nchi za Scandinavia.
3. Kuna ule Ujamaa wa kiparadiso (Utopian Socialism) ambao uko kwenye vitabu vya dini kama Biblia.

Wewe unauongelea Ujamaa upi huo ambao unalinda haki za binadamu: Kama unazungumzia Ujamaa wa Kimarksi, umechanganya mambo. Maana Karl-Marx na wafuasi wake kama Lenin, Stalin, Mao, Nyerere na Nkurumah hawaamini katika haki za binadamu (Individual and Basic Rights), wanasema zinaigawa jamii, wenyewe huamini katika haki za kiuchumi (Economic Rights) kama zile za kutoa elimu na afya bure.

Kiufupi msingi mzima wa hii falsafa ni uchumi wa vitu (Materialism) tu, ambapo wanaamini kabisa ukidhibiti Uchumi wa nchi kinguvu na kugawanya rasilimali za ummah, basi matatizo yote ya binadamu yataisha. Lakini, kuna ukweli wowote hapa ??? Binafsi nimeusoma UJAMAA kwa miaka zaidi ya kumi na nimeona matatizo yake makubwa.....

Ujamaa wa Scandinavia ni ule wa ambao umejengwa kwenye msingi wa Demokrasia ya kimagharibi (Western Democracy), Usawa kihaki na kifursa kwa wanajamii wote (Egalitarianism) na Muingilio wa moja kwa moja wa serikali katika kuwainua wananchi (The Welfare State). Huku mbali na Uchumi wa vitu, wanazingatia mambo mengi ya msingi ambayo yako kimaadili.....

Ujamaa wa kiparadiso sasa ndiyo ule wa Mbingu-Mpya na Nchi-Mpya ambao Adamu na Hawa waliishi kule Bustani ya Eden. Hakuna dhambi, hakuna umasikini, wanadamu wote sawa, hakuna serikali, hakuna magonjwa n.k Yani mambo bwelele. Hata Karl Marx anavyoandika kuhusu Ujamaa wake aliiga huu Ujamaa wa kwenye Biblia.

Haya sasa: Mkuu wewe unauzungumzia Ujamaa upi hapa, ili twende sawa ???
 
Butiku hawezi kutuambia kuhusu haki hasa baada ya kuwadhurumu watoto wa Mwalimu wakati baba yao akiwa hai na kuwafanya wawe hivyo walivyo sasa.
 
Umezuiwa kuanzisha Uzi unaomhusu Slaa? Yeye kapenda maelezo ya Butiku na ana sababu ambazo Wenye busara ndani ya JF wanajua Kwa nini!! Wewe kama unaona aliyoongea Slaa yana uzito anzisha Uzi wako watu wachangie.
Asinge mtaja basi kwa chochote humu!.
 
Popoma mnafiki slaa voice.
 
Umendika nilichotaka kiqndika. Wakati wanaosema wanaminywa kusema. Butiku anawalaumu hao hao kuwa ni waoga.
Anaishi Tanzania tofauti na tunayoishi. Tatizo ni hilo gorofa analonyonya kidogo kidogo hapo Sokoine Drive
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…