Nimemsikiliza JK Jana; Tafsiri Yangu...

Nimemsikiliza JK Jana; Tafsiri Yangu...

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,250
Ndugu zangu,

Jana saa kumi jioni nilishachukua nafasi yangu kwenye kijiwe hicho ( Pichani) cha wafanyabiashara ndogo ndogo Soko Kuu, Iringa.

Kwa kawaida, ndani ya banda hili la biashara kwa muda kama ule wa jana, watu huwa bize kuangalia mechi za Ligi Kuu zinazorushwa na Azam TV kutokea Dar. Na jana kulikuwa na Big Match; Azam dhidi ya Mbeya City.

Lakini, kwa umuhimu wa hotuba ya Rais, hata wapenzi wale wa soka waliamua kwa hiyari yao kusamehe soka na kubaki na hamu ya kufuatilia mambo muhimu kwa nchi, na kwa wakati huu.

Na hakika, aliyoanza nayo JK kwenye hotuba yake ndio haswa ilikuwa hamu ya Watanzania hawa niliojumuika nao kumsikiliza Rais wa Nchi.

Walikuwa na hamu sana ya kupata mtazamo na ufafanuzi wa Rais wao juu ya yaliyo karibu sana nao ( Proximity): Katiba na wimbi la Ujangili. Katiba inahusu mustakabali wao na watoto wao. Inahusu pia ulinzi wa rasilimali zao. Kwamba Katiba iliyo bora inaweza pia kuwazuia ' Majangili wa Kisiasa' kuingia au kubaki madarakani huku wakifanya ' ujangili' wa mali ya umma wakilindwa na mfumo dhaifu unaotokana na Katiba dhaifu.

Na Wananchi wale wanajua pia, kuwa wimbi la ujangili dhidi ya wanyamapori wetu unawahusisha pia vigogo wakiwemo wanasiasa. Wanataka kujua namna gani wahusika watadhibitiwa ili wasije kuwamaliza wanyamapori wetu kwa ' Ujangili' wao.

Suala la Afrika Mashariki na kutengwa kwa nchi yetu linawagusa na kuwakera Watanzania wengi. Wamefurahi kuwa Rais wa Nchi kalizungumzia Bungeni. Kwamba msimamo wetu kama nchi hatujitoi Afrika Mashariki.

Na ni ukweli, kuwa si ni Wana Jumuiya ya Afrika Mashariki na tutabaki kuwa hivyo. Hatuwezi kuwa jumuiya ya watu wa Afrika Magharibi, Kusini au Kaskazini.

Rais ameahidi kuendelea kuzungumza na Marais wenzake na tunaamini kuwa itafika mahali wenzake nao watatambua, kuwa hakuna Afrika Mashariki bila Tanzania.

Lakini, kwa Watanzania , Jumuiya ya Afrika Mashariki haiwaumizi sana kichwa kuliko haya ya Katiba , ujangili na mengineyo wanayokutana nayo nje ya milango yao kila kukicha. Mambo yenye kauthiri maisha yao ya kila siku.

Maana, tunajua, kuwa hakuna nchi ya Afrika Mashariki itakayotulazimisha tushirikiane kwenye tusilotaka kushirikiana. Tukiweka msimamo wetu kama taifa utabaki kuwa hivyo, hata waje na vifaru vya kivita, tutapigania msimamo wetu na tutashinda.

Na katika hili iko wazi, kuwa kwa sasa Watanzania hatutaki yaingizwe kwenye jumuiya masuala ya Uhamiaji, Ajira, Ardhi, Sarafu Moja na nchi yetu kuwa ndani ya Shirikisho la Kisiasa. Mengine yote tumesema sawa.

Na Tanzania haitakuwa nchi ya kwanza duniani kuchagua mambo ya kushirikiana kwenye jumuiya. Mfano hai ni kwenye Jumuiya ya Ulaya, nchi ya Norway ni mwanachama lakini haimo kwenye ushirikiano wa masuala ya Uhamiaji ( Schengen) Hivyo hivyo kwa Uingereza.

Kwenye Jumuiya hiyo hiyo ya Ulaya, Norway, Sweden na Uingereza hawamo kwenye kushirikiana kwenye sarafu moja ya Euro. Na kuna mifano mingine. Yote haya yanatokana na matakwa ya wananchi wa nchi hizo kupitia kura za maoni. Kwamba wananchi wa nchi hizo wamekuwa tayari kuwa kwenye Jumuiya ya Ulaya lakini kuna maeneo ambayo wamekataa kuyaingiza kwenye jumuiya.

Na sisi Watanzania tutakuwa watu wa ajabu sana, katika mazingira yetu ya sasa, tukakubali kuyaingiza kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki maeneo ya Uhamiaji, Ajira, Ardhi, Sarafu , na hata kuwa ndani ya Shirikisho la kisiasa.

Hivyo basi, kuhusu Afrika Mashariki, Watanzania tuko nyuma ya Rais wetu kimsimamo, na hatutasogea hata hatua moja.

Lakini, kuna ya kwetu ya kila kukicha na yenye kutuhusu na kutuathiri leo, na yatawahusu na kuwaathiri watoto na wajukuu zetu kesho na kesho kutwa.

Ni haya ya Katiba, Ujangili, kutunga sheria za kubana vyombo vya habari ilihali uporaji na kujimilikisha maelfu ya ardhi bila hata kuyatumia kunaofanywa hata na wanasiasa wetu kukiendelea.

Haya yana athari ya mbaya kwa mwananchi kila kukicha na tuendelee kupambana nayo kwa kasi zaidi...
Maggid Mjengwa.
Iringa.
 
Mimi kwa upande wangu nipo kinyume na ufikiri wa Mh. Rais.

Katika hotuba ya rais kuhusu swala zima ja E. Afrika amekuwa akilalamika kwa kiasi kikubwa, na hotuba yake nzima hakuna hata sentensi moja inayoonyesha fursa ambazo Tanzania tumezitafuta katika shirikisho na wenzetu wakazikataa. Zaidi alibaki akilalamika kuwa wenzetu wanaenda resi, wanataka kutumia ardhi yetu, wanataka tutumie vitambulisho vya uraiya kama paspoti ya kusafiria wakati sisi bado hatujakamilisha swala la vitambulisho.

Na hapa ndipo wenye akili tunagundua kuwa tatizo sio Kenya, Uganda wala Ruanda. Tatizo ni uwezo wa kufikiri wa wawakilishi wetu katika jumuiya ya E. Africa.

Ombi:
Mh. Rahisi naomba fanya hima pangua timu nzima ya uwakilishi katika jumuiya ya E. Africa na uiunde timu mpya yenye watu wenye uwezo thabiti wa kulisaidia taifa la Tanzania
 
Mimi kwa upande wangu nipo kinyume na ufikiri wa Mh. Rais.

Katika hotuba ya rais kuhusu swala zima la E. Afrika amekuwa akilalamika kwa kiasi kikubwa, na hotuba yake nzima hakuna hata sentensi moja inayoonyesha fursa ambazo Tanzania tumezitafuta katika shirikisho na wenzetu wakazikataa. Zaidi alibaki akilalamika kuwa wenzetu wanaenda resi, wanataka kutumia ardhi yetu, wanataka tutumie vitambulisho vya uraiya kama paspoti ya kusafiria wakati sisi bado hatujakamilisha swala la vitambulisho.

Wewe kama si umetumwa na akina Museveni, Kagame na Kenyata, basi umetumwa na Sumaye. Watu waliopo kwenye hiyo jumuiya ni makini sana na wasingekuwa makini, tungekuwa kama Kenya tu maana wao wanaburuzwa tu
 
Watanzania tuache unafiki.

Wakati tukilia na ujangili, serikali ilisikia kilio chetu na ikaendesha operesheni tokomeza. yaani hata haijafikia tamati, watu kama akina Kangi Lugola wanakula mlungula ili watumie sauti zao za kibabe kupaza sauti bungeni ili serikali isitishe. Hakika wamefanikiwa kwa hatua moja ila hatua nyingine hawajafanikiwa.

Rais amesema kuwa wanafanya tathmini ya kina na wakijiridhisha itaendelea kwa kasi zaidi, ari zaidi na nguvu zaidi. Majangili wakae chonjo na hata kama wana mapembe kiasi gani lazima wakamatwe tu
 
Mimi kwa upande wangu nipo kinyume na ufikiri wa Mh. Rais.

Katika hotuba ya rais kuhusu swala zima la E. Afrika amekuwa akilalamika kwa kiasi kikubwa, na hotuba yake nzima hakuna hata sentensi moja inayoonyesha fursa ambazo Tanzania tumezitafuta katika shirikisho na wenzetu wakazikataa. Zaidi alibaki akilalamika kuwa wenzetu wanaenda resi, wanataka kutumia ardhi yetu, wanataka tutumie vitambulisho vya uraiya kama paspoti ya kusafiria wakati sisi bado hatujakamilisha swala la vitambulisho.

Na hapa ndipo wenye akili tunagundua kuwa tatizo sio Kenya, Uganda wala Ruanda. Tatizo ni uwezo wa kufikiri wa wawakilishi wetu katika jumuiya ya E. Africa.

Ombi:
Mh. Rahisi naomba fanya hima pangua timu nzima ya uwakilishi katika jumuiya ya E. Africa na uiunde timu mpya yenye watu wenye uwezo thabiti wa kulisaidia taifa la Tanzania
Nahisi wewe sio mtanzania halisi labda ni mtanzania mpitaji! alichosema Rais Kikwete ni sahihi! hao mabwana watatu wanataka ardhi yetu! Mseveni ana uchu wa kuwa Rais wa Kwanza wa Shirikisho la A/Mashariki.
 
nimeisoma na kuisikiliza hiyo hotuba, wala alikuwa halalamiki, aliweka wazi mambo wenzetu wanayotufanyia na kutoa msimamo wa nchi kwenye jumuiya.. me naona unaongeza chumvi tu.

uzalendo sio swala la chama, kama hukipendi chama fulani usitumie mwanya huo kuponda na kupaka matope hata kama viongoz wanaongea point.

Wewe ulitaka kikwete aongee nini??
 
Mkuu Chambruma, Mimi ni mtanzania na naipenda nchi yangu kuliko kitu kingine, hivyo siwezi tumwa na mtu yeyote ili kuisaliti au kuinajisi nchi yangu. Ndio maana nasisitiza tuwe watu wa kupanga na kutekeleza kuliko kuwa watu wa kuongea na kulalamika
Wewe kama si umetumwa na akina Museveni, Kagame na Kenyata, basi umetumwa na Sumaye. Watu waliopo kwenye hiyo jumuiya ni makini sana na wasingekuwa makini, tungekuwa kama Kenya tu maana wao wanaburuzwa tu
 
Nahisi wewe sio mtanzania halisi labda ni mtanzania mpitaji! alichosema Rais Kikwete ni sahihi! hao mabwana watatu wanataka ardhi yetu! Mseveni ana uchu wa kuwa Rais wa Kwanza wa Shirikisho la A/Mashariki.

Ndugu yangu haina ya kugombana. Nikuombe utumie akili yako kidogo kutafakari manaeno machache kati ya menghi ya hotoba ya JK.
Nanukuu:
"Mheshimiwa Spika;
Kwa mujibu wa matamko ya pamoja (Communique) yaliyotolewa baada ya mikutano hiyo, kuna mambo yapatayo manane ya msingi yaliyoamuliwa kufanywa na nchi hizo kwa lengo la kuendeleza utengamano wa nchi hizo wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mambo hayo ni haya yafuatayo:
(1)Kujenga reli ya kisasa kutoka Mombasa hadi Kampala, Kigali na Bujumbura.
(2)Ujenzi wa Bomba la Mafuta la kutoka Kenya hadi Uganda na Sudani ya Kusini.
(3)Kujenga Kiwanda cha kusafisha mafuta nchini Uganda.
(4)Kuanzisha Himaya Moja ya Ushuru wa Forodha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kutekeleza vipengele vyote;
(5)Kuharakisha Shirikisho la Afrika Mashariki na kwamba itaundwa Kamati ya kuandaa rasimu ya Katiba ya Shirikisho.
(6)Kuharakisha uanzishwaji wa Visa ya pamoja ya Utalii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (Single East African Community Tourist Visa);
(7)Kuandaa utaratibu wa kutumia vitambulisho vya taifa kama hati ya kusafiria katika nchi zao; na
(8)Kuongeza uzalishaji na usambazaji wa umeme."

Mwisho wa kunukuu.
Kati ya fursa zote hizo wenzetu wapo tayari ila sisi hatupo tayari, zaidi ukiangalia fursa no.7 utaona udhaifu mkubwa wa serekali yetu, kwani mpaka sasa ukiuliza mchakato wa kutoa vitambulisho vya kiraiya limefikia wapi? jibu ni kitendawili kigumu.
YOU HAVE A LOT TO LEAN
 
Mr.Mjengwa,Mimi ninavyo ona hii suala la East africa sindhani kama litawezekanakwanza kabisa kwenye mioyo ya watanzania hilo suala la east africa halipo.Ukifuatilia kwa kina utaona muungano huo ni wa kisiasa lakini wananchibado hawajana umuhimu wake.Huwezi kulazimisha east africa wakatikenya,uganda na Rwanda hawakutaki,kila mtu ana lengo lake,Sababu ya Kenyata kuichukia Tanzania ni sababu Tanzania ina kubalika na mataifamakubwa kuliko Kenya mfano ziara ya Obama,Rais wa china,Thailand,India etcKenya waliuzika kuona Tanzania inapewa kipaumbele kwenye mambo ya diplomasia.Sababu ya Uganda kuichukia Tanzania ni sababu Museveni anataka kuwa rais wa kwanzawa east africa sasa anaona kama Tanzania inasua sua kwenye suala la shirikisho,Sababu ya Rwanda kuichukia Tanzania ni suala la Tanzania kupeleka jeshi congo kupambana na M23 na kwa namna moja Rwanda itakosa mapato yatokanayo na rasilimaliza congo.SASA UNAFIKIRI KWELI TANZANIA INA NAFASI EAST AFRICA?
 
nimeisoma na kuisikiliza hiyo hotuba, wala alikuwa halalamiki, aliweka wazi mambo wenzetu wanayotufanyia na kutoa msimamo wa nchi kwenye jumuiya.. me naona unaongeza chumvi tu.

uzalendo sio swala la chama, kama hukipendi chama fulani usitumie mwanya huo kuponda na kupaka matope hata kama viongoz wanaongea point.

Wewe ulitaka kikwete aongee nini??

Mkuu sina haja ya kuongeza chumvu wakati hotuba yenyewe imezidi chumvi, Embu tunukuu kidogo

"Mheshimiwa Spika;
Jambo la nne ni ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Mombasa – Kampala – Kigali – Bujumbura. Hili nalo hatuna tatizo nalo. Si mradi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ni jambo lililo chini ya mamlaka ya nchi wanachama husika. Hata hivyo, ni vyema kutambua ujenzi wa miundombinu ya reli, barabara na usafiri wa anga na majini kuunganisha nchi za Afrika Mashariki ni miongoni mwa mambo ya kipaumbele cha juu yanayoshughulikiwa na Jumuiya yetu. Jumuiya hutengeneza mikakati ya pamoja na ndiyo maana tuna East African Railway Masterplan, tuna East African Road Network, na tuna Lake Victoria Development Programme kwa ziwa Victoria.

Kwa ajili hiyo, nilitegemea kuwa reli ya kutoka Mombasa hadi Kigali na Juba ingekuwa na tawi linalounganisha reli hiyo na reli ya Tanzania kama ilivyo reli ya Moshi – Voi – Taveta aliyotuachia mkoloni. Tulitegemea hivyo kwa minajili ya kuunganisha soko la Afrika Mashariki ambapo naamini Tanzania ni mdau muhimu. Lakini inaelekea kwa maoni ya wenzetu hivyo sivyo.

Mheshimiwa Spika;
Lazima nikiri kuwa inashangaza na tunayo kila sababu ya kuuliza kwa nini wenzetu wameamua kufanya hivi. Kumetokea nini toka tukutane pale Arusha Aprili 28, 2013 na Juni 24, 2013 walipokutana kuamua kufanya mambo ya kujenga na kuimarisha utengamano wa Afrika Mashariki kwa kubaguana, Haijawahi kuwa hivi kabla"

Ukitaka malalamiko zaidi utapata pia
 
JK ameongoza taifa kwa vipindi viwili na muda sio mrefu atakuwa mbali na siasa,atabaki mshauri kama ataona inafaa...natatizika kidogo anapokumbuka shuka wakati wa machweo! Angekuwa strong hivi toke kwanza yumkini chama na taifa vingekuwa na sura tofauti sasa
 
Mleta Mada: JUMUIYA ya kiuchumi maana yake nini? USHIRIKIANO maana yake nini? Ili nchi ziitwe Jumuiya, ni mambo gani yanatakiwa kutekelezwa?

Werevu wanaelewa nani mkweli, wasio werevu wataendelea na 'maneno mingi'.
 
Mr.Mjengwa,Mimi ninavyo ona hii suala la East africa sindhani kama litawezekanakwanza kabisa kwenye mioyo ya watanzania hilo suala la east africa halipo.Ukifuatilia kwa kina utaona muungano huo ni wa kisiasa lakini wananchibado hawajana umuhimu wake.Huwezi kulazimisha east africa wakatikenya,uganda na Rwanda hawakutaki,kila mtu ana lengo lake,Sababu ya Kenyata kuichukia Tanzania ni sababu Tanzania ina kubalika na mataifamakubwa kuliko Kenya mfano ziara ya Obama,Rais wa china,Thailand,India etcKenya waliuzika kuona Tanzania inapewa kipaumbele kwenye mambo ya diplomasia.Sababu ya Uganda kuichukia Tanzania ni sababu Museveni anataka kuwa rais wa kwanzawa east africa sasa anaona kama Tanzania inasua sua kwenye suala la shirikisho,Sababu ya Rwanda kuichukia Tanzania ni suala la Tanzania kupeleka jeshi congo kupambana na M23 na kwa namna moja Rwanda itakosa mapato yatokanayo na rasilimaliza congo.SASA UNAFIKIRI KWELI TANZANIA INA NAFASI EAST AFRICA?

Kuheshimu mawazo ya watu wengine ndio mila na desturi yangu.
Ila naomba unisamehe sana, kwani ni hatari sana mtu kuwa na "NAROW MIND" alafu akapata nafasi ya kutoa wazo nndani ya jamii.
 
"Mh. Rahisi naomba fanya hima pangua timu nzima ya uwakilishi katika jumuiya ya E. Africa na uiunde timu mpya yenye watu wenye uwezo thabiti wa kulisaidia taifa la Tanzania"

Hana ubavu wa kufanya unayomwambia kwasababu yeye ndiye aliyepitisha hawa maboya na kuwaacha wenye akili kubwa kwa misingi ya kujuana na rushwa!! Nani asiyejua kuwa hawa wajumbe wa baraza la kutunga sheria la jumuiya ya afrika Mashariki wa chama cha magamba wote walipita kwa rushwa? Nani aisyejua kuwa kati ya hao wajumbe wengine ni mafisadi na wanajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya? Juu ya yote hayo Vasco Dagama aliwakumbatia na halafu leo unataka awatoe!!! You are a dreamer.
 
Mleta Mada: JUMUIYA ya kiuchumi maana yake nini? USHIRIKIANO maana yake nini? Ili nchi ziitwe Jumuiya, ni mambo gani yanatakiwa kutekelezwa?

Werevu wanaelewa nani mkweli, wasio werevu wataendelea na 'maneno mingi'.

God Analysis
 
"Mh. Rahisi naomba fanya hima pangua timu nzima ya uwakilishi katika jumuiya ya E. Africa na uiunde timu mpya yenye watu wenye uwezo thabiti wa kulisaidia taifa la Tanzania"

Hana ubavu wa kufanya unayomwambia kwasababu yeye ndiye aliyepitisha hawa maboya na kuwaacha wenye akili kubwa kwa misingi ya kujuana na rushwa!! Nani asiyejua kuwa hawa wajumbe wa baraza la kutunga sheria la jumuiya ya afrika Mashariki wa chama cha magamba wote walipita kwa rushwa? Nani aisyejua kuwa kati ya hao wajumbe wengine ni mafisadi na wanajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya? Juu ya yote hayo Vasco Dagama aliwakumbatia na halafu leo unataka awatoe!!! You are a dreamer.

Punguza jazba mkuu, na hapo kwenye red haujanitendea haki kabisa.
Ni kweli hawa waakilishi walipatikana kwa njia tofautitofauti na huenda kwa njia kama uliyoitaja. Nafahamu pia waziri wetu wa E. Africa yupo busy na mambo ya uraisi 2015. Hivyo basi huoni kama hapa kunaaja ya kuibomoa hii timu na kuiunda upya? na hapa hilo jukumu lipo mikononi mwa Mkuu wa Kaya.
 
nimeisoma na kuisikiliza hiyo hotuba, wala alikuwa halalamiki, aliweka wazi mambo wenzetu wanayotufanyia na kutoa msimamo wa nchi kwenye jumuiya.. me naona unaongeza chumvi tu.

uzalendo sio swala la chama, kama hukipendi chama fulani usitumie mwanya huo kuponda na kupaka matope hata kama viongoz wanaongea point.

Wewe ulitaka kikwete aongee nini??

wala si issue ya chama huyu si mtanzania kabisa.... kwenye hili watanzania tumeungana tukaweka vyama pembeni.... kuhusu jumuia ya afrika mashariki huo ndio msimamo wetu sote!!!
 
Mkuu ya Kaya;
Kuheshimu mawazo ya watu wengine ndio mila na desturi yangu.
Ila naomba unisamehe sana, kwani ni hatari sana mtu kuwa na "NAROW MIND" alafu akapata nafasi ya kutoa wazo nndani ya jamii.

Ok kama unaheshimu mawazo ya watu wengine barikiwa
 
Kikwete kasema hatutoki EA, that is fine. Lakini kwa kulizungumzia swala hili kwa mtindo wa wao wamekosea sisi tupo sahihi kutakuwa na EA kweli? Dipromasia ya kimataifa inataka busara nyingi, na hatutaweza kuwafanya Uganda, Kenya na Rwanda wawe pamoja nasi ikiwa viongozi wetu wanatoa kauli kama "sisi ndo watoa taraka". Wao wameshaungana wanasonga mbele, sisi tumebaki kuwa watu wa hotuba tu!
 
Mkuu nashukuru kwa mawazo yako mazuri. Na siku zote jambo la msingi ni kujitasmini wewe kwanza ya kumtasmini mwenzio. Je! Tanzania chini ya Raisi Kikwete na Serekali ya ccm ilishawai kutoa tasmini kwa upande wa tanzania jinsi tunafanya ndani ya jumuiya?
Na hili ndilo tatizo kubwa ndani ya viongozi wa TZ, na pengine hii serikali haijui nini wanapaswa kufanya ndani ya shirikisho.
 
Back
Top Bottom