Mkwaruzo
JF-Expert Member
- Feb 21, 2011
- 563
- 98
Sidiriki kuyapima machofu ya kazi yako, inayokupa usumbufu kutoka kwa mgambo wa jiji. Inayokupigisha virungu mkiwa mnkimbizana kama vile watoto wapo mchezoni. Au ile ya nyongeza ya kukesha na zege usiku mzima. Huku ukiwa umeniacha mpweke kitandani. Yote hayo uliyafanya kwa ajili yangu mimi na watoto. Nilikuhurumia na kukupenda sana, kufikia kiasi cha kukosa hata ladha ya chakula bila ya kula nawe. Tukiwa tunaishi kwa utaratibu huo, siwezi kuisahau siku hii, baada ya chakula kuwa tayari na kuwakogesha watoto, nilianza na simulizi nzuri ili kuufanya mlo kuwa wa furaha kwao. Mara Baba Chanja ukapiaga hodi, nami kwa heshima nilikuja kukufungulia na kukupokea huku nikikukaribisha ndani bila ya kuacha utani wa hapa na pale kukufanya uwe na furaha. Nilipaswa kuwa na kila sababu ya utiifu kwako kwani nawe ulinipenda na pia kunijali.
Basi nikakuandalia maji ya kukoga na kubaki nakusubiria kwa ajili ya kula. Haikupita muda, vishindo vya ajabu na moto mwingi uliweza kuonekana katika kila pembe ya mitaa yetu ya Gongolamboto. Wakati nikiwa sijuwi hata wapi pakuelekea, sikuamini macho yangu kukuona upo hoi umeshajeruhiwa na bomo. Nguvu ziliniishia,nikamua kumruhusu Farjala akimbie na wadogo zake watatu na waende wanapoweza. Bali mimi nilibaki nawe huku nikiwa na kichanga changu mgongoni ambacho kilikwisha kaukwa na sauti kwa kilio. Sauti ya simanzi iliyoambatana na maumivu, uliitoa kuleta ujumbe wa maagano kati yetu. Uchungu wa hayo maneno yako ya mwisho yananifanya nashindwa kufanya lolote pale yanapojireje akilini mwangu. Kwa sasa nimebaki nakukumbuka tu Baba Chanja na kukuombea makazi mema huko uliko. Ila sijuwi wapi naweza kumpata mwengine kama wewe wa kuwa farijiko la moyo wangu.