Nimempa ujauzito Hataki kuniona

Nimempa ujauzito Hataki kuniona

Hataki kukuona kwasababu si mkuu wa mkoa yupo ataenda kumuona? sasa akuone wewe una nini
 
Jamani naomba mnisaidie, inawezekanaje binti ambaye umempa ujauzito ghafla anabadirika hataki kukuona Kabisa. Ni kweli nakuwa mhusika wa hiyo mimba au nakuwa nimebambikwa tu
subiri ataenda kumuona makonda
 
Mimi leo nimetoka kupigwa na vibakuli vya undongo hadi nikataka kumshushia kipondo,,,jana nivyofungua mlango tu mtu kakimbilia chooni kutapika, saasa alipomaliza akakaa huko huko hataki kutoka ikabidi nimfate kujua kulikoni?
Akanifukuza tokaaaa ukinisogelea najisikia kichefu chefu.

Hahaaaah hapa ndo naelewa tofauti ya mwanaume na mtoto wa kiume.
 
Ni rafiki yangu. Sio demu wangu

Mimba kwenye ile miezi 3 ya mwanzo inakuwa na kawaida ya kumkataa muhusika halisi.

Huwa nadhani ni zile swaga za yeye anahangaika halafu muhusika unatanua tu, kwa hiyo anatafuta style ya kukupa adhabu na wewe uteseke kidogo.

Ila ile miezi 3 ya mwanzo ikiisha ni raha sana kulea mimba, kuna phase flani anakuwa anataka mambo yetu sasa, pale ndo unatamani kila mara awe na mimba.
 
sio yako wewe huwezi kumpa mwanamke mimba
 
Mimi leo nimetoka kupigwa na vibakuli vya undongo hadi nikataka kumshushia kipondo,,,jana nivyofungua mlango tu mtu kakimbilia chooni kutapika, saasa alipomaliza akakaa huko huko hataki kutoka ikabidi nimfate kujua kulikoni?
Akanifukuza tokaaaa ukinisogelea najisikia kichefu chefu.

Hahaaaah hapa ndo naelewa tofauti ya mwanaume na mtoto wa kiume.
Hahahaaaaass umenipasua mbaya
 
Acha ujinga kijana fanya kazi tafuta pesa utabakia kulea watoto wa wanaume wenzako.
 
Jamani naomba mnisaidie, inawezekanaje binti ambaye umempa ujauzito ghafla anabadirika hataki kukuona Kabisa ni kweli nakuwa mhusika wa hiyo mimba au nakuwa nimebambikwa tu
Haya ndo mambo ya kiseng***e nisiyopenda kusikiaaa yaani una mimba yangu halafu hutaki kuniona

Halafu muda huo huo nikiwa mbali unanitumia text na kunipigia simu mara utaka hiki mara unataka kilee mara ohoo mimba ikoo mara vileee

Mwisho wa siku unakuja kugundua ulikuwa unahudumia tambalaa na ushapoteza muda mwingi kuwaza kutuma pesa,kufanya hivii kumbe mwenzio anaku enjoy tuu ama kweli
Anakuona weee boyaaa tuu.
 
Usishangae mkuu kwanza utaambiwa unachukiwa unatamani uweke sumu yote ni experience ya kusikia n akuona..mara msosi hustahili kula akipika etc...si ajabu akapendwa mwingie kabisa....mi nishapendwaga na mtu insta alikuwa mjamzito so akawa anapenda tunachat tu akawa hampendi baba mtu....niliahidi kumuoa na ashajifungua sema ndo napotezea tu naona sio ishu nisije ingiwa tamaa ya kukwichi nay etena..ila mimba ni balaa sipati picha....mimi mwenyewe nishaambiwaga natamani kumwagiwa maji ya mot yani acha...ni process tu...nasikia mwingine anaenda petroll station kunusa tu harufu au mletee kwenye dumu
 
Ni mabadiliko ya muda tu, yataisha akijifungua Mimba zinakuja na sarakasi nyingi sana. Hiyo ya mwenzako imekuja kihivyo wala hujaibiwa ni yako tu Pole sana najua unaumia maana unapenda uwe naye karibu.

Komaa tu, ila najua hata ukilazimisha utatukanwa tena matusi ya nguoni.

Wala usimfikirie tofauti.

Mkuu umeongea point kubwa sana. Nina rafiki yangu alioa ndoa takatifu kabisa kanisani. Mkewe alipopata mimba tuu vurugu zilianza. Mwanamke hataki kabisa kumuona jamaa, na jamaa kisaikolojia ndo alijipanga ndo muda wa kuonyesha anajali kila kitu anamfanyia mwanamke kawa malkia usipime. Lakini ndo hivyo hataki kumwona mpaka chumbani hataki walale wote. Ikafikia hatua wakaachana binti akaenda kwao kisa kamgogoro mdogo tu wa kujibizana. Kesi ilienda mpaka kwa wachungaji lakini ikaamuliwa wasubiri ajifungue kwanzaa ndo watajadili. Mara paaaaaaaap baada ya kujifungua mbona mwanamke ndo alikuwa wa kwanza kumtafuta mumewe.
 
Back
Top Bottom