Nimempa kipigo kizito Afisa wa benki hatakuja kunisahau

Huyo mfanyakazi wa benki amekosea sana kutaja salio lako mbele za watu, ethics za kazi hazipo hivyo,
Mkuu hasira zako zielekeze kwenye kutafuta pesa, tafuta pesa, narudia tena tafuta pesa, heshima itakuja tu na hautokua tena na tabia ya ugomvi ugomvi, nakukumbusha tafuta pesa mkuu.
Kabisaa yaani
 
Umeacha kazi ya ulinzi gard warda sikuizi umekuwa bondia wa kupiga piga watu.
 
Teh teh...

Kuna uwezekano mleta mada yupo nyuma ya nondo na buku 60 haikutosha kama dhamana
 
Kuna watu bwana wanachukulia kila mtu ni bwege bwege

Mimi nilikuwa nimeishaapa kutulia na kufanya mishe zangu niachane na mambo ya fujo fujo sasa kumbe bado kuna watu wanataka fujo,

Juzi nilienda benki ya NMB wilaya fulani hivi sitaitaja,

Nilienda kwa ajili ya kubadili kadi yangu kwani ilikuwa inakwisha muda wake

Mimi nimetoka zangu home nimevaa nimependeza nimechomekea shati na nimechana nywele vizuri

Nikafika benki jamaa wa benki anafanya kazi kwa uzembe uzembe mimi ananisimamisha dirishani yeye anapiga story na mwenzake?

Nikajisemea moyoni hivi huyu ananijua kweli au ananichukuliaje, nikawaza au nimfanyie kitu mbaya kama nilivyomfanya mfanyakazi wa NIDA?

Nikamwambia tafadhali naomba ufanye kazi iliyokuleta ofisini wateja wengi bado tuna kazi nyingi za kufanya

Jamaa kwa kiburi nae akaanza kunijibu jibu pale akaniambia kwa hasira eti kwanza katoe kopi kitambulisho chako ndio urudi, nikamwambia kopi ninayo, nikampa akanipa fomu nikajaza

Sasa basi nilivyorudisha ile fomu jamaa nikakuta amefyumu halafu alivyo na dharau anaongea kwa sauti,

Eti mtu mwenyewe haelewi, anatusumbua sumbua utadhani ana mamilioni kwenye akaunti,
Sasa kitu alichokuja kunifanya nipandishe mizimu ni pale alivyosema

Mtu kwenye akaunti ana elfu sitini halafu anatusumbua sumbua hapa!

Daaah niliaibika mbele za watu, nilitamani nimrukie jamaa palepale ning'oe korodani zake ila pale benki kulikuwa na polisi nikamuheshimu tu huyi polisi maana sikutaka kuanzisha tu vagi maana polisi mimi naonaga ni Raia wakakamavu tu!

Nikamwambia yule jamaa mdomo wako umekuponza nitadili na wewe personal!

Basi jana sikufanya kazi siku nzima ili nimfundishe jamaa kuwa mwenye elfu sitini kwenye akaunti anaweza kukutoa uhai

Jamaa jana nimemlia target ile saa 11 wanatoka benki nilimsindikiza nyuma nyuma alipofika mbali kidogo na benki nikamshika nikamwambia bro unanikumbuka mimi ndio yule mwenye elfu sitini kwenye akaunti nimekuja kuitoa!

Kabla hajaongea chochote nikamvuta mkono nikaunyonga,
Pale pale kwa spidi ya haraka kama umeme nikamtwisha ngumi nzito mgongoni,
Ile ngumi ikasindikizwa na head moja ya hatari nilimpa head nzito akahisi dunia inazunguka,
Kabla hajatua chini nikamzaba kofi moja matata sana

Nilimchakaza ndani ya dakika moja halafu nikamwambia
Kesho nakuja kutoa ile elfu sitini yangu tena naitolea ndani ,

Kwa jinsi alivyoniaibisha nahisi adhabu niliyompa haijamtosha niko nafikiria adhabu nyingine nzuri ya kumpa.

Ngoja nitafakari nimfanyeje ili nimalize hasira zangu huyu mtu naombeni ushauri jamani nimpe adhabu gani?

Maana kitendo chake cha kutaja salio langu la benki si cha kiungwana hata kidogo yaani nina hasira sana na huyu mpuuzi nitamfanyia kitu kikubwa nchi nzima itajua!

Tangu alivyoniaibisha mbele ya watu hata kula sili chakula hakipandi kabisa, yaani ngoja ntamuonesha kazi.

Stay tuned
Hahahaha
 
Kakosea sanaa ku expose details zako ambazo ni privacy yako tu...hapo ungeenda kwa meneja nafikir kama c kupewa barua ya onyo bac angekuwa terminated..na hapo nd ungetimiza msemo wako kuwa mdomo umemponza
 
Warumi 12:19 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.
 
Mkuu kwanini usingekuwa ulishaungana na kina Matumla au Mwakinyo?
Nafkikri wale ndi wanaotumia mikono yao kupiga kwa faida, hizo mambo zako zitakuja kukucost!
Kwanza nashauri usirudi tena kupigana nae, anaweza kukuaibisha zaidi kwa kipigo kizito maana utamkuta yupo well ;prepared!
Wakati unakimbilia kumdaka mkono unakutana na pepsi ya jino, unang'oka meno yote ya mbele alafu kabla hujakaa sawa anakushtukiza kofi zito la usoni, Hapo sasa badala ya kutema yale meno utajikuta unameza yote tumboni!
Nasisitiza ufuate ushauri mkuu hapo juu, pambana nae kisheria utanufaika zaidi, hizo hasira zako ni hasara!
 
Back
Top Bottom