Nimemkumbuka Nasma Hamisi Kidogo aliyemtikisa Khadija Kopa kwenye taarabu

Uzi wa wahenga wanakumbushana nyimbo zao za kitambo.
b Khadija kopa ni mbishi kwenye taarab yupo kitambo sana.
mwenyewe anakwambia kuna kuzaa mtoto na kumnya mtoto
 
Sijui Koppa alimtibua nini maza maana kachana humu hatari

Ule wimbo wa Hadija Kopa: Jamani mambo leoooo ( Mambo iko huku) nao ulikua na michambo sana. Miaka ile ya 1999-2001 anaekumbuka African Bambataa huu wimbo ulikua hot sana. Ulichangia Nasma kutunga nyimbo hizo. Usikilize hapa(audio tu)

 
watu wanaosikiliza taarabu kwa wanawake naonaga kama mashangingi ya kimalaya yanayotoa mlango wa uwani, huwa nawadharau sana yaani. ila kwa wanaume naaminigi ni mashoga.

Miaka hiyo hakukua na namna. Radio zilikua chache, muziki kwa kiasi kikubwa ulikua ni muziki wa Dansi wa kizazi cha mwisho cha muziki wa dansi( Twanga, Muungano Band, T. O. T band, Tam Tam, Beta Musica, Diamond Musica, Dar Musica, FM Academia/ Musica, kutaja chache)hapo ni baada ya kizazi cha kati cha muziki wa dansi kufa( Vijana Jazz, Washirika, OSS, Bimalee, MCA International nk)

Wakati huo Bongo Flavor ilikua ndo inachipukia na iliwachukua muda mwingi sana muziki wa Bongo Flavor kukubalika. Kwenye hili kongole ziende kwa watu wa mwanzo mwanzo kabisa kama Mh Sugu, Mh Prof Jay, baadae Jay Moe, MwanaFa, AY, Juma Nature, Ins Haroun na Gangwe Mob, Mh Temba, Lady Jay Dee, Sister P, Ray C, Craz GK! Hao walitumia nguvu kubwa sana kulazimisha hadi Bongo Flavor kufika ilipo. Hiyo ni miaka ya angalau 1997-2002! Sote tunakumbuka Girl Friend ( sound track) ya Filam ya jina hilo hilo!

Kwa hiyo, kwa wakati huo, labda kana mdau ulikua mdogo, vyombo vya habari vilipiga sana nyimbo hizo na hakukua na namna utasikiliza tu kama siyo nyumbani basi kwenye daladala( wakati huo Hiace kwa asilimia 99)
Tumetoka mbali sana! Hata hawa wanabongo flavor wa kileo( ambao wamefanikiwa kiukweli, wanatakiwa wawashukuru sana hao wakubwa, wametumia nguvu kubwa sana hadi watu kuwaelewa kuwa nao ni muziki. Those days, Bongo flavor kwa watu wa makamo walichukulia ni uhuni tu na mambo ya ovyo, narudia tumetoka mbali sana
 
Mambo iko huku a.k.a mtu mzima hovyo aliyoimba Nasma Kidogo ilikuwa ni shida mjini kwa wakati ule kwa sababu Hadija Kopa na TOT yake walikuja na nyimbo mpya mfululizo zisizopungua tatu lakini walishindwa kulifunika hilo songi. Yaani ukisikia kupigwa na kitu kizito basi hapa TOT ndio walipigwa na kitu kizito toka Muungano. Pamoja na watu kumsifu mwimbaji bi Nasma Kidogo lakini sifa zimwendee mtunzi wa mashairi ya ule wimbo akiitwa mustafa ramadhani (sina uhakika na jina). Najua wapo wakongwe hapa watanisahihisha kama nimekosea jina la huyo mtunzi.

Kwa wakati ule upende usipende utasikiliza tu taarabu maana radio zote zilikuwa zinapiga muziki huo kwani muziki wa dansi ndio ulikuwa unaagaaga. Muda si muda taarabu nayo ikala za uso na bongo fleva ikashika chati.
 
Unakuta zee zima na tambi lake eti limekaa kabisa linasikiliza taarabu.Tanga kuna vituko sana for sure
 
Back
Top Bottom