Nimemkumbuka Dr. Slaa

Hungeweza kuona Dr. Slaa akiokoteza maneno ya kihuni ya humu mitandaoni kama vile "jiwe, mshamba, chatle" nk kisha unaenda kuyaandikia hoja kama afanyavyo Lisu na wafuasi wengine wa chadema!

Slaa alikuwa anaibua hoja mpaka system inatetemeka.
Sujui alikua anapata wapi data? Na huyu katibu wa sasa sijui anafanya nini ofisini?
 
Alinyimwa kugombea ubunge akiwa CCM akahamia CDM,kanyimwa kugombea uraisi akiwa CDM akahamia CCM. Kwa hiyo yeye haoni wengine kufaa kugombea bali yeye tu!?
Shida yake kubwa hana maamuzi, maamzi hutoka kitchen.
Sijawahi kuona Askofu msaliti kama huyu!! Yeye anakula bata baada ya kuuza mechi na wenzake wanauguza majeraha ya marisasi....
 
aaah weee.
 
vipi yanayoendelea kwa sasa? Slaa aliondoka sababu lowasa na saiz lowasa yupo ccm ambako slaa yupo unadhani atatoka? Leo katiba ya nchi si lolote si chochite
rip nyerere

Your browser is not able to display this video.
 
Nami toka moyoni nimemkumbuka Dr Slaaa ndani ya upinzani wa sasa. Wakati mwingine hua nafikiri upinzani wa sasa wamerogwa kwani kazi yao kubwa ni kudandia dandia hoja nyepesinyepesi tu. Kila siku wanalalamika bila kuja na suluhu ya matatizo. Wanatafuta huruma ya walio madarakani.
 
Ninauhakika kama nawe ulikuwepo ndani ya siasa wakati wa ukatibu wa huyo Dr Slaa, utakua ume mmiss sana.
Alinyimwa kugombea ubunge akiwa CCM akahamia CDM,kanyimwa kugombea uraisi akiwa CDM akahamia CCM. Kwa hiyo yeye haoni wengine kufaa kugombea bali yeye tu!?
Shida yake kubwa hana maamuzi, maamzi hutoka kitchen.
 
Ujumbe wako umenitia huzuni Sana. Tuliiamini chadema, wao wakacheza na mioyo yetu, wakatugeuza ma toy kwamba wao ndio wanaamua sisi tufikirie Nini na kwa muda gani.
Mara fisadi, ghafla kamanda wa mabadiliko. Na matusi yasiyo na idadi kwa Dr Slaa.
Ila ndio ivo tena bado Kuna manyumbu wanawaamini wapinzani wa bongo. Nilimpa Magu kwasababu ya kauli mbiu CHAGUA MAGUFULI SIO CCM. Bila gia ya angani CCM walikuwa hawatoki 2015. Penye uzia penyeza rupia.
 
Hungeweza kuona Dr. Slaa akiokoteza maneno ya kihuni ya humu mitandaoni kama vile "jiwe, mshamba, chatle" nk kisha unaenda kuyaandikia hoja kama afanyavyo Lisu na wafuasi wengine wa chadema!

Slaa alikuwa anaibua hoja mpaka system inatetemeka.
Hayo yote ni kwasababu awamu iliyopita iliruhusu kazi za siasa zifanyike,haikuogopa kukosolewa,kusemwa vibaya wala kutukanwa,walikuwa waungwana.sio siasa za sasa ambapo hata mikutano ya ndani ya chama inazuiwa kwa mitutu ya bunduki kinyume cha katiba.hata huyo DR Slaa mwenyewe angekuwepo kipindi hiki asingekuwa na lakufanya.

Awamu hii imeamua CCM pekee ndio ifanye siasa,nafikiri wanavyofanya CHADEMA kukaa kimya kuwaacha CCM wafanye wanavyotaka wakati huo wakijipanga kwenda sawa na siasa za awamu hii ni sawa kabisa namimi nawaunga mkono,hakuna haja ya wanasiasa kujitolea kuumizwa,kuteswa,kuonewa,kwaajili ya watu ambao hawajatambua HAKI zao.
 
Ni kama wamepoteza Dira sijui kama wanajua wanapotaka kwenda...
 
Unachekesha, au unataka tukuwekee picha za mke Slaa akivuja damu iliyotokana na kupigwa wakati wakiandamana?

Subiri ccm iwaambie sasa anzeni kufanya siasa
 
Hakika mkuu, sie tuliwaza mabadiliko kumbe wenzetu ilikua fursa
 
Kuna mwingine wanataka wampitishe tena.
 
Ila pia Dr Slaa ana kipaji cha kujieleza kwa level nyingine. Ule mdahalo ITV ambao CCM walimkimbia alisimamisha nchi kwa hoja zilizopangwa na zinaelezwa kwa utulivu bila matusi wala mihemko.

Hata hotuba ya Serena alipindua upepo wote na hadi kesho itabakia kuwa hotuba bora sana. Acha apumzike zake tu kwa zile sarakasi alizofanyiwa na watu aliowaamini sana unaweza kufa kwa pressure.
 
amini nakuambia,HAZIKUWA siasa za kupigana RISASI mchana kweupe ndani ya eneo la serikali linalolindwa na askari.
Nini risasi usisahau mkutano wa chadema ambao ulipigwa bomu huko Arusha! Basically wengine tulijua nini kingetokea kwa Chadema baada ya kupoteza uchaguzi hasa kupoteza ushawishi.

Hata Mbowe alijua matokeo yake ndio maana alisema atajiuzuru akishindwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…