Sasa pale pale ungemuuliza jamaa huyo ni nani wake ili ukipata jibu la jamaa kama ni mchumba umkabidhi rasmi pale pale ungetangaza waje wafuate nguo zake.
Ila katika maelezo umesema ni mpenzi wako, kwahiyo huna mamlaka yoyote juu ya huyo binti maana hata hatua ya uchumba bado, hana hata pete ya uchumba wako.
Pia tafakari uwezo wako wa kitandani inaonesha nesi haridhiki kabisa na wewe ndo maana anaenda kwa jamaa maana wewe ni kama kaka yake. Yaani kwa jamaa anapata raha zote hadi anaimba nyimba za mahaba na kuwa kero kwa majirani na akiwa kwako haumlizi hata mguno hakuna haojitambui bado?
Huyo nesi siyo saizi yako kabisa usipende kwa macho kaka angalia zana zako za kazi, tafuta saizi yako. Pia ni Mungu amekuonesha mapema kwamba huyo hafai kuwa mkeo, mwachie jamaa wala hiyo mimba si yako ukute wote wawili mliambiwa ana mimba na wote mnatunza mimba. Kama ulikuwa unaishi naye geto nakushauri mgawane vyombo kila mtu aanze upya.
Ukifanya ukorofi nakwambia utafanyiwa kitu mbaya na huyo dada na jamaa yake maana kama alikuwa anakudanganya anaenda semina kumbe semina ya kugegedwa, akirudi si huwa ana vizawadi na wewe unakula, huoni kwamba ulishalishwa na jamaa?
Baada ya hapo utapewa limbwata mapema ili aje apigwe ndani kwako ukiuliza unagombezwa kama shamba boy! Kwahiyo usiwaze kuhusu hiyo mimba wala si yako, pia Mtoto akizaliwa kama ni wako utajua baadaye.
Huu ni ushauri tu ila maamuzi ni yako, tafakari kwa kina, ufanye maamuzi. Usiwaze sana ukagongwa na gari, ni mambo ya kawaida hayajaanza kwako, we bado mdogo using'ang'anie Nesi, omba Mungu akupatie mke mwema!