Nimelia sana usiku wa leo, nipo katika kipindi kigumu sana cha maisha

Mimi ni Kijana wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 24(Leo ni kumbukizi yangu ya kuzaliwa), pia ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu Bachelor of Science with Education moja ya chuo kikubwa hapa jijini.

Kielimu mimi ni mtu pekee hadi sasa katika ukoo wa baba na mama kufika chuo kikuu, wote kwenye ukoo wa baba na mama walio soma sana wameishia kidato cha nne tena wameambulia four na sifuri.

Wakuu, naandika haya nikiwa na machungu, huzuni na hisia za maumivu makali sana moyoni na akilini mwangu, hasa napotazama familia na yotokea na hali ya uchumi wa familia yangu.

Sina tumaini tena la Maisha, kwa umri wangu huu madogo nimeyaoana maisha ya dhiki na shuruba za Kila namna, nimefanya kazi mbalimbali licha ya kuwa bado na soma Lakini neema ya mafanikio imekataa kabisa kuja upande wangu.

Hapa nilipo natamani japo, nifanye mpango ni ende Africa ya kusini japo kwa kufoji ili nikajaribu bahati yangu, huenda ipo huko, lakini moyo unakata kabisa kufanya maamuzi haya.

Wazazi wangu, siwezi kuwalaumu kwani mimi mwenyewe ni Shahidi wamepambana sana lakini neema na bahati ya mafanikio haijawa upande wao, baba yangu kajaribu Kila aina ya kazi lakini wapi, vilevile mama yangu kafanya bidii sana lakini mambo mabaya.

Nimesoma shule ya msingi hadi advance na badae chuo kikuu, nimesoma kwa tabu sana miaka yangu hiyo, hii ni kutokana na hali ya uchumi wa familia yangu.

Nawaza sana,mwezi mwaka huu namaliza masomo yangu, je kipi kitatokea, wadogo zangu watano Wana- nitazama kaka yao wakiwa na matumaini makubwa sana ndani yao juu Yangu

Stress zinataka kuni maliza, nipo scared sana wakuu
Aisee umezaliwa mwaka gani ?
 
Nawaza sana,mwezi mwaka huu namaliza masomo yangu, je kipi kitatokea, wadogo zangu watano Wana- nitazama kaka yao wakiwa na matumaini makubwa sana ndani yao juu Yangu

Stress zinataka kuni maliza, nipo scared sana wakuu
Acha upumbavu wewe kijana mdogo. Kwanza kinachokupa stress ni nini wakati hata hayo maisha hujaanza? Kama uko chuo soma kwa bidii furahia uanafunzi wako. Ukiendelea na huu upumbavu wa kujipa stress za kishamba utaishia pabaya.
 
Mheshimiwa Dr Samia Suluhu Hassan mama yetu....tunajua uliachiwa mzigo mkubwa wa mlundikano wa wasioajiriwa lakini tunaomba mama,jitahidi hivyohivyo uajiri vijana....jamani hali ni mbaya huku mtaani....vijana ambao ndiyo nguvu ya taifa Wamekosa matumaini ya nchi na kuishi
Huyo hata kuajiriwa hafai ataenda kufundisha stress watoto wetu tu mashuleni.

24 unapata stress za ugumu wa maisha ni upumbavu.

Hana mtoto wala mke anajiliza ugumu wa maisha !!!.

Maisha hayajawahi kuwa na huruma na watu dhaifu vichwani.
 
Brow, walau wewe una CV, Me mwenzako situation ya familia ipo kama yako na sina CV yoyote street toka 2017 hadi now nimeweza kujitegemea 100% na kidogo viteniteni naweza kutuma nyumbani wazazi wakilia and just imagine baba na mama walitengana hivyo na-manage pande mbili hivyohivyo Mungu anasaidia na makosa sitokuja kufanya ni kuleta mtoto duniani ikiwa Mungu hajanipa hela ya kufanya mwanangu asijekuomba asingezaliwa kama mimi.
 
Just Chill Son,,b'se GOD ABOVE ALL"Pambana usikate Tamaa,,Kama Wazazi wako Wamepambana na Kukupambania upo na wao bado wapo licha ya changamoto za kimaisha,,Nawe Sasa ni wakati wako wa kupambana na kuwapambania katika changamoto za kimaisha,,Hakuna asie kuwa na changamoto katika haya Maisha,,,Kama umekata tamaa nenda kawatembelee wagonjwa hospitali naamini Utamshukuru sana Mungu na utakuja nishukuru pia.
 
Mimi ni Kijana wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 24(Leo ni kumbukizi yangu ya kuzaliwa), pia ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu Bachelor of Science with Education moja ya chuo kikubwa hapa jijini.

Kielimu mimi ni mtu pekee hadi sasa katika ukoo wa baba na mama kufika chuo kikuu, wote kwenye ukoo wa baba na mama walio soma sana wameishia kidato cha nne tena wameambulia four na sifuri.

Wakuu, naandika haya nikiwa na machungu, huzuni na hisia za maumivu makali sana moyoni na akilini mwangu, hasa napotazama familia na yotokea na hali ya uchumi wa familia yangu.

Sina tumaini tena la Maisha, kwa umri wangu huu madogo nimeyaoana maisha ya dhiki na shuruba za Kila namna, nimefanya kazi mbalimbali licha ya kuwa bado na soma Lakini neema ya mafanikio imekataa kabisa kuja upande wangu.

Hapa nilipo natamani japo, nifanye mpango ni ende Africa ya kusini japo kwa kufoji ili nikajaribu bahati yangu, huenda ipo huko, lakini moyo unakata kabisa kufanya maamuzi haya.

Wazazi wangu, siwezi kuwalaumu kwani mimi mwenyewe ni Shahidi wamepambana sana lakini neema na bahati ya mafanikio haijawa upande wao, baba yangu kajaribu Kila aina ya kazi lakini wapi, vilevile mama yangu kafanya bidii sana lakini mambo mabaya.

Nimesoma shule ya msingi hadi advance na badae chuo kikuu, nimesoma kwa tabu sana miaka yangu hiyo, hii ni kutokana na hali ya uchumi wa familia yangu.

Nawaza sana,mwezi mwaka huu namaliza masomo yangu, je kipi kitatokea, wadogo zangu watano Wana- nitazama kaka yao wakiwa na matumaini makubwa sana ndani yao juu Yangu

Stress zinataka kuni maliza, nipo scared sana wakuu
Ningekuwa mimi ndiyo wewe, nisingelia usiku kucha kwa sababu kama hizi ulizozitoa hapa!

Badala yake ningejipiga kifua mara saba, na kujiambia kamwe sitakata tamaa! 😩 Na badala yake nitapambana mpaka mwisho 💪 ili kujikomboa mimi wenyewe, na pia familia yangu; kutoka kwenye hili lindi la umasikini wa kipato, kielimu, na pia kifikra.

Halafu kijana wa kiume unaanzaje kulia lia hovyo! Halafu ni nani aliye kudanganya ya kwamba huko Afrika ya Kusini kuna maisha ya maana?
 
Usiwaze dogo tulia bado mapema jichanganye na mtaa taratibu

jifunze ujuzi mbalimbali muda wako utafika na utaona mafanikio ndugu au wadogo zako sio jukumu lako ni la wazazi wako so tuliza akili

Anzisha njia Kisha utawainua mmoja mmoja

Stop having victim mentality
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom