Nimekuwa Mtu mwenye wivu na mafanikio ya watu, naombeni ushauri

5997

JF-Expert Member
Jan 19, 2019
514
1,204
Mpaka najishangaa,

Baada ya mambo yangu kubuma nimekua naonea sana watu wivu,

Yaani kama kusoma nimesoma shahada ninayo lakini akitokea mtu akanielezea mafanikio yake roho inaniuma sana,

Yaani mtu nimesoma naye au nimemzidi elimu nikiona anamafanikio roho inaniuma

Jana jioni kwenye kijiwe cha kahawa kulikua bwana mdogo tu anasimulia kuwa yeye ni dereva na analipwa 1.2M per month dah niliposikia hivyo roho iliniuma sana. Nikataka hadi kumpiga,

Hii dunia bora iishe tu maana watu wengine tumekuja kama kutalii tu hatuna la maana,

Jana asubuhi nimekutana na jamaa nilisoma naye chuo lakini yeye alinitangulia mwaka mmoja chuoni,
Yule bwana alinipa story kua ameajiriwa kwenye shirika fulani analipwa 900k

Daah yaani iliniuma nyie. Yaani usiku mzima wa jana sijalala namuwaza jamaa ukizingatia mimi maisha yangu magumu tu!

Kitendo cha jamaa kuniambia analipwa 900k kimeniuma sana kwakweli

Ipo siku tu.
 
Ukiwa na wivu wa jinsi hiyo ni vigumu sana kupata Baraka mtu aliefanikiwa mwombee azidi kufanikiwa zaidi na Mungu atakuona na wewe huku ukijibidiisha
 
Mimi nafikiri ni namna ambavyo umeweka ufahamu wako na namna ambavyo umejipangia malengo yako hakuna jambo ambalo litakuumiza kama ukiwa mtu wa malengo

Yaani ukitoka hapa unaenda hapa ukitoka pale unafika pale
Baada ya wiki ntapata shingi flani au ntamaliza kazi flani

Na ukiweza kufanya hivyo hao watakao kwaambia Hiyo mishahara watakuwa wana kupata nguvu ya kuongeza zaidi malengo yako ufike kwa kiwango kikubwa zaidi ya kile ulichokisudia

#tatizo sio tatizo ila tatizo linakuja baada kulifikiria tatizo #
 
kizazi hiki, wasomi wote, watakuwa waajiliwa wa standard 7, wasomi watakuwa wanaongoza kwa umasikini, matajili ni watu simple na kawaida sana! elimu tanzania haina soko, unasoma na bado hujaelimika, pia, unasoma na bado masikini, sasa elimu hapo imekalia wapi!
 
Wivu wa hvyo ukupe motisha ya kupambana na ww, amini ipo siku utafikia pale unatamani ufike. Its just a matter of time na juhudi zako.

Pia acha tabia za kupigana zinaharibu CV yako maana mtu atashindwa hata kukupa connection akiogopa utadunda mtu tena huko.
 
Back
Top Bottom